Kinga ya Kutoshtakiwa Spika na Naibu Spika na Utamaduni wa Mabunge ya Commonwealth

dudus

JF-Expert Member
Feb 28, 2011
21,985
48,939
Wadau!

Kama mjuavyo, kikatiba ni Mh. Rais wa nchi pekee aliyekuwa na kinga ya kutoshtakiwa. Lakini kwa siku za hivi karibuni listi imeongezwa kidogo ambapo MR, WM, JM, Spika na NS nao wana kinga ya kutoshtakiwa hata watakapokuwa wamestaafu. In short, ni "kinga ya maisha".

Kama tunavyojua, Bunge la JMT ni mwanachama mtiifu wa mabunge ya Commonwealth na huzingatia sana mila, desturi, na miiko ya mabunge hayo hasa pale jambo husika linapokuwa na maslahi kwa wabunge, Spika na NS.

Kwa kuwa "kinga ya kutoshtakiwa" ina maslahi ya moja kwa moja kwa wahusika (Spika na NS), na kwa kuwa ni jambo zito lenye athari nyingi kwa nchi, kwa mwenye ufahamu, tafadhali atujuze ni bunge lipi lingine lenye mila, desturi, na miiko ya kutoshtakiwa maspika na manaibu-spika wake ambako Bunge la JMT limerithi utamaduni huo?
 
Hakuna ni hili tu, na hili lilikuja awamu ya tano.
... at least Bunge letu limekuwa so innovative! Hope mabunge mengine yataiga utamaduni huu mzuri! KATIBA, KATIBA, KATIBA!
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom