Kinga kwa Rais aliyeko madarakani na wastaafu ni kichocheo cha uvunjaji haki, Iangaliwe upya

Think like easy going woman,

Chanzo cha ufisadi wa mkapa ni nyinyi! mlioandika humu. Dharau ,uchoyo, ubinafsi, ubaguzi, umimi, visununu visivoisha,usengenyaji nk ndo vimefanya aibe! na wataiba saneni tu.
 
Kuondolewa kwa shria hii Fisadi, pia kutasaidia kupunguza idadi ya Wagombea urais ambayo wakati wa kinyam]ng'ang'anyioro cha kwenda kugombe Urasi huwa kunakuwa na orodha ndefu ya watu wanaotaka kuwa Marais maana wanajua fika kuwa wakipata nafasi hiyo Ufisadi wao hautakumbukwa milele. Hii itatusaidia kuwa na Wagombea safi na wnaojiamini kuwa ni Waadilifu na ni safi.
DRC wagonbea urais ni 120!tena hao ni rasmi. wamepitishwa na NEC

Wakati mwingine mnaweza kujikuta mnazalisha Rais anaeogopa kuachia madaraka kwa kuogopa kushitakiwa akistaafu
Marais na ni binadamu, tuwaunge mkono na kuwadhibiti kwa kutumia bunge
 
DRC wagonbea urais ni 120!tena hao ni rasmi.wamepitishwa na nec
Wakati mwingine mnaweza kujikuta mnazalisha Rais anaeogopa kuachia madaraka kwa kuogopa kushitakiwa akistaafu
Marais na ni binadamu,tuwaunge mkono na kuwadhibiti kwa kutumia bunge
Kwahiyo waendelee tu kuwa na kinga ili wapate moyo wa kuachia madaraka?
 
Acha tu Ben/Azory/Kanguye wame disappear and died simple tu na hakuna uchunguzi wowote. ICC is watching.
 
Naunga mkono raisi kuwa na kinga wakati akiwa madarakani ili kuondoa hathari za kuwa na unstable governments. Maana kuna watu watakuwa wanaendesha maisha yao kwa kushinda mahakamani kwa kumfungulia kesi hadi kesi ili hali mambo hayaendi.

LAKINI, akimaliza tu muda wake hiyo kinga nayo iwe imeiisha na awe anaweza kushitakiwa kwa aliyoyafanya akiwa madarakani. Yaani achukuliwe kama mtumishi mwingine yeyote tu wa umma, ambaye anaweza wajibishwa hata akiwa amestaafu kwa aliyoyafanya akiwa kazini.

Hii italeta nidhamu kwa hawa viongozi wetu

Inaniuma sana kuona watu wanasujudiwa kama maraisi wastaafu wakati wametuibia vyakutosha, na kusababisha vifo vya wananchi wengi kwa kutohakikisha hizo pesa na rasilimali walizoiba, zinaboresha miundombinu kama ya afya kwa ajili ya wananchi.

Sasa sijui tunakwama wapi kuwaondolea kinga ili hali wanasheria wetu wanajiita wasomi. Sasa sijui ni wasomi au wakariri? Maana nikama wamekariri tu toka vitabuni.
 
Hakuna anaeweza weka kitanzi shingoni mwake. Watawala nchi za dunia ya tatu ni miungu watu. Sheria wazitungazo ni kufanikisha mipango yao na makundi yao.
 
Take it as an hypothetical scenario/example.

Ikitokea akaja Rais mwingine akasema nami navunja sheria nakuondolea kinga ya kutoshitakiwa, akakupeleka mahakamani kwa kuvunja Katiba na sheria wakati wa utawala wako. Akatoa instaces ambazo umevunja Katiba na sheria, je utatafuta mawakili kupinga uamuzi wake huo?
Umekuwa ukivunja sheria, sasa na huyu Rais akivunja sheria hiyo ya kinga yako, utatafuta mawakili wa kukutetea?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hua marais hawawazi hayo mambo mpaka "LA MGAMBO LINAPOLIA".

Mfano, Rais wa Sudan, Omar Al Bashir alikua bandidu kinoma, watu walimsihi ajirekebishe ila akaona hakuna wakumfanya lolote, watu walivumilia wakachoka, wakaamua kumwaga kimapinduzi, then akavishwa bangiri mkononi na kuwekwa ndani kama mwari, halafu sinema haikuishia hapo maana hivi karibuni anapelekwa ICC (Mahakama Ya Kimataifa Ya Makosa Ya Jinai).
 
Nadhani mifano kama hii imfanye abadilike, lkn sikio la kufa.

Hua marais hawawazi hayo mambo mpaka "LA MGAMBO LINAPOLIA".

Mfano, Rais wa Sudan, Omar Al Bashir alivyomwagwa kimapinduzi, then akavishwa bangiri mkononi na kuwekwa ndani kama mwari, halafu sinema haikuishia hapo maana hivi karibuni anapelekwa ICC (Mahakama Ya Kimataifa Ya Makosa Ya Jinai).

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ha haha, wapambe wake watakuja na majibu yao yatakuwa na mwelekeo kuwa yeye haondoki pale kwani ndio amefika. Ila ni yeye mwenyewe alisema kuwa kama uhakika upo kuwa mtu kakamatwa na kosa (let say meno ya tembo au utakatishaji) basi wakili akijitokeza kumtetea kwa nini asiunganishwe naye kesi moja?

Hivyo atakaye jitokeza kumtetea ni bora naye atuambie tumuunganishe kwenye kosa la kuvunja katiba

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Umekumbusha jambo la muhimu sana.
Ha haha, wapambe wake watakuja na majibu yao yatakuwa na mwelekeo kuwa yeye haondoki pale kwani ndio amefika.
Ila ni yeye mwenyewe alisema kuwa kama uhakika upo kuwa mtu kakamatwa na kosa (let say meno ya tembo au utakatishaji) basi wakili akijitokeza kumtetea kwa nini asiunganishwe naye kesi moja?
Hivyo atakaye jitokeza kumtetea ni bora naye atuambie tumuunganishe kwenye kosa la kuvunja katiba

Sent using Jamii Forums mobile app

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Moja ya ishara ya wizi,ubadhirifu na matumizi mabaya ya madaraka ni binadamu anayeaminisha watu kwamba anapambana kila aina ya uovu HUKU AKIWA MWENYE ANA KINGA YA KWISHTAKIWA.

Janga la Taifa ni pale viongozi waandamizi wanaojitangaza kutuongoza kwa haki wanapojiwekea kinga yakushtakiwa huku wakiamru tuliopo chini yao tuishtakiwe wakadanganya sisi niwabadhirifu.

Hakuna mtu msafi anayetathmini nakujichukulia hatua mwenyewe, hakuna mtu msafi kisiasa anayeogopa kuishtakiwa.

Kama kweli hatufuji nakutumia Mali na nadaraka kinyume Cha sheria tukubali kuchunguzwa nakuchukuliwa hatua Kama nchi zilizoendelea zinavyofanya.

TUFUTE KINGA
 
Tangu Nyerere, Mwinyi, Mkapa,Kikwete na sasa Magufuli hakuna aliyethubutu kusema sheria hii inayonipa kinga ya kushitakiwa nikiwa madarakani au nikistaafu naifuta.

Yawezekana wote walikuwa hawana makosa ya kuweza kutiwa hatiani sasa hofu yao ni nini mpaka waliifumbia macho sheria hii ?
Je, kuna dhambi gani imejificha ndani yao?

Je, walikuwa na hakika gani kuwa viongozi wenzao wajao watakuwa watakatifu kama wao? Sheria hii isingekuwepo ningekuwa wa kwanza kumpeleka court Mh.Mkapa kwa Mauaji ya Wazanzibar 2020.
 
Katika nchi yetu kuna sheria za ajabu sana, mojawapo ni hii ya kumlinda Rais Mstaafu kutokana na makosa aliyoyafanya akiwa Rais. Habari juu ya Ufisadi uliofanyika katika awamu ya tatu ya Uongozi wa nchi yetu ni dira tosha ya kutufanya tufikirie upya juu ya Kinga ya Rais Mstaafu ya kutoshitakiwa...
Uzuri ni kuwa waliopitisha sheria hizo kwa kishindo na jeuri kubwa licha ya kuonywa na waliowaita wakwamisha maendeleo,umfumo umekataa na kuwatema.Hivyo wanajuta mioyoni mwao na wasijue lakufanya.
 
Ni kwanini viongozi wa Tanzania wanakinga ya kushtakiwa? Hadi Sasa viongozi wangapi Wana kinga hiyo? Wao wanautofauti gani na viongozi wa Mataifa mengine ambayo kila mtu anashtakiwa?

Je, tafsiri ya kikatiba kwamba kila mtu ana haki sawa inatekelezwaje katika mazingira haya ya kinga? Je utawala uliopo ukiondoka ukaja utawala mpya, unaweza futa hizi kinga na kuwachukulia hatua waalifu waliojificha kwenye mwamvuli wa kinga ya kushtakiwa?
 
Back
Top Bottom