King of De Docta Ignorantia; Hatuwezi kumpa FISI ulinzi wa BUCHA | Page 3 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

King of De Docta Ignorantia; Hatuwezi kumpa FISI ulinzi wa BUCHA

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Juliana Shonza, Sep 21, 2015.

 1. J

  Juliana Shonza Verified User

  #1
  Sep 21, 2015
  Joined: Dec 19, 2012
  Messages: 2,007
  Likes Received: 533
  Trophy Points: 180
  Zipo juhudi kubwa za kuwapumbaza watanzania kwa kile kinachoitwa kuwaelewesha ili kufanya Informed Decision kwa kumchagua LOWASSA wa Ukawa dhidi ya MAGUFULI wa CCM..juhudi hizi zilizoimarika hivi karibuni zinatumia waandishi wa habari wa vyombo maalum na wale wa kujitegemea, lakini nguvu hiyo imesambaa zaidi mpaka kwenye mitandao ya kijamii..nguvu ya wanamabadiliko waliobadilika.

  Juzi niliandika nikimjibu PASCO wa JF kuhusu kile alichokiita Ujinga wa watanzania kwa kuichagua CCM, akiwa anawaelekeza watanzania kuamini na kumchagua EDWARD LOWASSA eti kwa madai yake HUYU NDIO MUSSA ATAKAYETUVUSHA BAHARI YA SHAMU..lakini hakuishia hapo amejitokeza tena kuendelea na msimamo wake ila kwa bahati mbaya ameacha maswali na hoja muhimu katika majibu yangu na kuhamia katika hoja zingine ambazo majibu yake ni Rahisi...maana amehamia kwenye hoja ya RUSHWA ambae huyo anayemnadi kuitokomeza RUSHWA hawezi hata kuizungumza kwenye majukwa yake ya kisiasa na anaamrisha wengine pia wasiizungumze..AJABU SANA.

  I don't believe on mistakes, hivyo siamini kuwa makosa katika nukuu ya PASCO yalikuwa ni BAHATI MBAYA...binafsi najua ni muendelezo wa De Docta Ignorantia, on learned ignorance ambayo PASCO ni mfalme akitaka tumchagua FISI akatulindie BUCHA kwa kigezo kuwa MLINZI wetu wa sasa anasinzia sinzia....Noooooo NEVER..!!

  Nitajinukuu;


  Kwenye RED ni maeneo ambayo nimeonyesha strength ya CCM ambayo PASCO kakimbia kuyajadili kwa hoja, kuwa CCM imeamua kujijenga UPYA na kufukuza manyang'au wote waliokuwa wanaharibu IMAGE ya Chama, manyang'au hayo yamenunua chaka jipya na wanalipa watu wawasafishe kwenye vyombo vya habari na mitandao ya kijamii...na bahati mbaya wamejitokeza watu waliojitoa ufahamu na kukubali kutumika..na hakika HAKUNA DENI BAYA KAMA DENI LA TUMBO linawatesa wengi katika watu hata wale wenye elimu zao.

  Kwenye KIJANI ni maswali ambayo PASCO kwa maksudi ameyakimbia, HASEMI lolote kuhusu UPINZANI, hasemi kuhusu THE DON na makando kando yake...anasema tu kuwa anachukia RUSHWA lakini hasemi DON LOWASSA amejiandaaje kupambana na Rushwa hata awe bora kuliko MAGUFULI wa CCM..

  1. LOWASSA wa CHADEMA na UKAWA ni kielelezo cha ubovu, uchafu na uovu uliokuwa unasababisha harufu mbaya ndani ya CCM kwa zaidi ya miaka 30 aliyokuwa anatumikia Serikali kupitia chama hicho. He re

  2. LOWASSA hawezi kuwa Kiongozi wa Mabadiliko (hayo ambayo PASCO) anawaaminisha Watanzania, kwani alikuwa katika mfumo huo kwa zaidi ya miaka 30 na hakubadilisha chochote, leo LOWASSA amebadilika nini..?

  3. LOWASSA ni MWIZI, NI MLA RUSHWA MKUBWA na nimeandika haya nikitumia ID yangu kamili, na nitasema haya popote pale..na kwa fedha zake za wizi amekuwa akinunua watu wa kumsafisha kila uchao, nina mashaka ndugu yangu PASCO is on the list.

  4. LOWASSA anasimama na mwenzie SUMAYE kukosoa Serikali ambayo maamuzi makubwa yaliyoangamiza TAIFA walishirikia kuyapitisha kama sio KUYASIMAMIA ili yapitishwe na Serikali..leo wamekuwa wasafi ghafla kwa kuwa wamehamia UPINZANI..kama sio UJUHA ni nini..?

  5. LOWASSA ameishi, ametenda na ameendelea kutetea IMANI kuwa pesa ndio kila kitu, imani ambayo PASCO and the TEAM MABADILIKO imeendelea kuamini, hawezi kuishi nje ya IMANI hiyo ambayo inapingana na IMANI ya UADILIFU...na tunachotaka watanzania ni MTU MUADILIFU ili akanyooshe mambo yaliyopinda ndani ya Serikali..

  5. HAKUNA ushahidi ama rekodi yeyote ambayo inaonyesha LOWASSA amebadilika, bali upo USHAHIDI na REKODI ambazo zinathibitisha kuwa LOWASSA ni MWIZI, MLA RUSHWA, MUONGO na FISADI PAPA..hana moral authority ya kukemea Rushwa.

  PASCO..,narudia tena kuwa WATANZANIA sio WAJINGA: tumekusikia, tumetafakari na tumeamua MAGUFULI ndio ajaye. Hatuko tayari kumpa FISI ulinzi wa BUCHA.

  VIDEO: KINANA na CCM MPYA

  https://youtu.be/bSG2TBeCS_A   
 2. Ngalikihinja

  Ngalikihinja JF-Expert Member

  #41
  Sep 22, 2015
  Joined: Sep 1, 2009
  Messages: 17,559
  Likes Received: 5,123
  Trophy Points: 280
  Juliana Shonza
  Hakuna mtu kuomba poo hapa.... Ni kuweka fact mezani... I will only potezea mtu kama fact ataziweka mezani na zitajadiliwa kwa mtazamo sahihi.... Hata uboe vipi, kama kuboa ni kwa fact I will shut my mouth up..!! lakini kwa mbwembwe na michezo ya maneno Nooooo.....

  Magufuli aliwahi kusema serikali yake mawaziri hawatakuwa wa kuchakata kama ni kuchakata wakachakatie nje ya uwazili... Sasa umemsikia alipokuwa anairudia ahadi ya Meli aliyoitoa JK..??? Kakubali MCHAKATO wa meli.. kwamba sasa mawazili watachakatia ndani ya serikali yake... KIFUPI KASHAANZA KUYAKANA MANENO YAKE ... No way.... KURA YANGU YA NOOOOOO LAZIMA AHUSIKE NAYO


   
 3. fugees

  fugees JF-Expert Member

  #42
  Sep 22, 2015
  Joined: Aug 13, 2012
  Messages: 2,614
  Likes Received: 410
  Trophy Points: 180
  The best dressed lie fro shonza! Hata form two nadhani alivuka kwa vibomu ha ha ha ha
   
 4. MC Chere

  MC Chere JF-Expert Member

  #43
  Sep 22, 2015
  Joined: Jun 29, 2015
  Messages: 588
  Likes Received: 356
  Trophy Points: 80
  Kwanza yeye siyo mwizi?
   
 5. J

  Juliana Shonza Verified User

  #44
  Sep 22, 2015
  Joined: Dec 19, 2012
  Messages: 2,007
  Likes Received: 533
  Trophy Points: 180
  Mhhhh ndugu yangu walimu wako wana kazi ngumu sana...no wonder karibuni utapewa uongozi BAVICHA.
   
 6. A

  Afixa0 JF-Expert Member

  #45
  Sep 22, 2015
  Joined: Jun 16, 2015
  Messages: 464
  Likes Received: 398
  Trophy Points: 80
  Leo TWAWEZA watatoa utafiti wao.. ambayo inaongozwa na miriam sarungi baada ya hapo siku zijazo REDET watatoa zao lkn nawaombeni mjue ni kwann JANUARY alitangaza asilimia zile,,,ule ulikuwa ni mpango ambao kwss utafuatiwa na TWAWEZA, halafu REDET yote yaki pendelea CCM na kutengeneza mazingira ya kuiba kura maana hawana namna nyingine. Kutokana hali hyo nawaombeni ndugu zangu msiwe na wasiwasi ppt ulipo endelea kupigana
  Taarifa za uhakika nilizopata CCM imeandaa utafiti feki kupitia Twaweza....watasema Magufuli ana asilimia 68% na Lowassa 22%

  Ripoti halali wanayo ya Lowassa kuongoza lakini watatoa ripoti Feki.

  Kwa huu muda wa asubuhi mpaka saa 4 pigeni kelele kupitia njia mbalimbali kulaani ushenzi huu.Tumieni JF,FB,tweeter,Instagram nk...
   
 7. Bongolander

  Bongolander JF-Expert Member

  #46
  Sep 22, 2015
  Joined: Jul 10, 2007
  Messages: 4,882
  Likes Received: 53
  Trophy Points: 135

  Tangu lini mwana CCM aende kuwa kiongozi BAVICHA? No way, not a way. I am just trying to think out of the box and call corruption CORRUPTION regardless of who bears the name.

  Given what you have written that is what i managed to glean. There is clear evidence ya wizi wa CCM (EPA, ESCROW, RICHMOND, Import support etc etc). Ndani ya CCM kuna baadhi tunapenda kumwita Kenge kwa jina lake halisi Kenge, na Mamba kwa jina lake halisi Mamba, na sio kuzungusha maneno. Tukisema eti chama kisafi hata mtoto atacheka.

  Kwa hiyo tukiangalia kwa vyama, no doubt kuwa CCM kiko juu kwenye wizi wa nyama. CDM, CUF, NCCR etc hatujui kwa kuwa hajiwahi kutawala.

  Tukiangalia kati wa wagombea wote mmoja mmoja bila kujali vyama vyao, tunaona kuwa Lowassa fisadi CCM tuna ushahidi huo, Magufuli fisadi pia ushahidi upo. Kwa hiyo hawafai kupewa bucha.

  Kama point yako ya msingi ni FISI hawezi kuaminiwa kwa ulinzi wa bucha, definitely CCM as part can not be trusted. CDM as the party we do not know yet, since they have not been in a position to loot the country.

  lakini kwa wagombea wote wawili sidhani kama kuna anayeweza kuaminiwa kulinda bucha.

  If we stand for principles, Chama cha ACT na mgombea wake, wanaqualify zaidi.

  Lakini swali ni kwanini the electorate does not seems to be enthusiastic with ACT na mgombea wake? Is it hard kwa walimu wangu kuelewa mantiki yangu? Kwanini Fisadi mmoja afae na mwingine asifae?
   
 8. Mzalendojr

  Mzalendojr Senior Member

  #47
  Sep 22, 2015
  Joined: Jul 29, 2015
  Messages: 171
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 35
  NA ikiwa Lowassa anaongoza kura za maoni ccm nao wasemeje. mbona cdm wanapenda kila kizuri kiwe upande wao. msiwafundishe Twaweza kazi
   
 9. b

  bea Senior Member

  #48
  Sep 22, 2015
  Joined: Oct 25, 2010
  Messages: 132
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 45
  Dada kama hujala CCM muda uliokuwepo angalau umeliwa na kuolewa so sasa jipange kurudi tena Ukawa maan sasa hivi hakuna jinsi
   
 10. j

  jabulani JF-Expert Member

  #49
  Sep 22, 2015
  Joined: Aug 1, 2015
  Messages: 3,166
  Likes Received: 4,149
  Trophy Points: 280
  Mpaka leo sielewi kaiba nini, hawasemi.
  Kama hawajamkamata basi sio mwizi ni propaganda tu za kisiasa. Kama wanang'ang'ania ni mwizi basi ina maana serikali yao ni dhaifu haiwezi kukamata wezi. Chama legelege huzaa serikali legelege. Tuchague ukawa mafisiccm wajulikane na hatua stahiki zichuliwe. Ajenda ya ufisadi ni ya cdm/ukawa, kama kawaida yao ccm hawana ubunifu tena wanakopi kila kitu ukawa na kusema ni cha kwao.
   
 11. W

  WATANABE JF-Expert Member

  #50
  Sep 22, 2015
  Joined: Apr 13, 2011
  Messages: 1,091
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 135
  NA MIMI NAKUBALIANA NA WEWE KUWA WATANZANIA SIO WAJINGA NA WAMESHATAMBUA KUWA HAKUNA MABADILIKO YA KWELI KUPITIA KWA KIONGOZI MMOJA MMOJA ANAYEONGEA KAMA CHIRIKU, KWA KUWA TUMEJARIBU NJIA HIYO KWA MIAKA 50; SASA WAMEAMUA WANATAKA MABADILIKO YA MFUMO HIVYO ILI KUBADILI MFUMO NI LAZIMA CCM IKAE PEMBENI KWANZA NDIPO KATIBA YENYE MAONI YA WANANCHI IWEZE KUPITISHWA; MAMBO MENGINE YATFUATA.

  SASA NAKUHOJI NI MSIMAMO WAKO KUHUSU KATIBA YA TANZANIA, JE UNAPENDELEA ILE YA WARIOBA ILIYOKUWA NA MAONI YA WANANCHI AU ILE YA FISADI PAPA CHANGE ILIYOCHAKACHULIWA NA CCM KWA MASLAHI YAKE?

  VIDEO: KINANA na CCM MPYA
   
 12. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #51
  Oct 8, 2017
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 25,639
  Likes Received: 23,822
  Trophy Points: 280
  Kiukweli tulikuwa tunaidharau jf, lakini amini usiamini, mabandiko kama haya, yamesaidia saidia, huwezi jua!. Zamani nilikuwa napitia mabandiko yako kwa dharau na kujibu kwa kejeli, lakini baada ya uteuzi, sasa napitia mabandiko yako yote kwa makini zaidi, heshima na adabu haswa kwa kuzingatia wewe sasa ndio bosi wangu kwenye tasnia ya habari.

  Karibu Boss, Mheshimiwa saba, Bi Juliana Shonza.

  Paskali.
   
 13. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #52
  Nov 27, 2017
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 25,639
  Likes Received: 23,822
  Trophy Points: 280
  Kiukweli nimekubali matokeo, fisi hawezi kukabidhiwa kuilinda bucha yetu na kwenye udiwani, nimeshuhudia!.

  Asante mama, (sio nakuzeesha bali sisi Wasukuma, kwa heshima ya mwanamke, kila mwanamke tunamuita mama!).

  Paskali
   
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
Loading...