King of De Docta Ignorantia; Hatuwezi kumpa FISI ulinzi wa BUCHA | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

King of De Docta Ignorantia; Hatuwezi kumpa FISI ulinzi wa BUCHA

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Juliana Shonza, Sep 21, 2015.

 1. J

  Juliana Shonza Verified User

  #1
  Sep 21, 2015
  Joined: Dec 19, 2012
  Messages: 2,007
  Likes Received: 533
  Trophy Points: 180
  Zipo juhudi kubwa za kuwapumbaza watanzania kwa kile kinachoitwa kuwaelewesha ili kufanya Informed Decision kwa kumchagua LOWASSA wa Ukawa dhidi ya MAGUFULI wa CCM..juhudi hizi zilizoimarika hivi karibuni zinatumia waandishi wa habari wa vyombo maalum na wale wa kujitegemea, lakini nguvu hiyo imesambaa zaidi mpaka kwenye mitandao ya kijamii..nguvu ya wanamabadiliko waliobadilika.

  Juzi niliandika nikimjibu PASCO wa JF kuhusu kile alichokiita Ujinga wa watanzania kwa kuichagua CCM, akiwa anawaelekeza watanzania kuamini na kumchagua EDWARD LOWASSA eti kwa madai yake HUYU NDIO MUSSA ATAKAYETUVUSHA BAHARI YA SHAMU..lakini hakuishia hapo amejitokeza tena kuendelea na msimamo wake ila kwa bahati mbaya ameacha maswali na hoja muhimu katika majibu yangu na kuhamia katika hoja zingine ambazo majibu yake ni Rahisi...maana amehamia kwenye hoja ya RUSHWA ambae huyo anayemnadi kuitokomeza RUSHWA hawezi hata kuizungumza kwenye majukwa yake ya kisiasa na anaamrisha wengine pia wasiizungumze..AJABU SANA.

  I don't believe on mistakes, hivyo siamini kuwa makosa katika nukuu ya PASCO yalikuwa ni BAHATI MBAYA...binafsi najua ni muendelezo wa De Docta Ignorantia, on learned ignorance ambayo PASCO ni mfalme akitaka tumchagua FISI akatulindie BUCHA kwa kigezo kuwa MLINZI wetu wa sasa anasinzia sinzia....Noooooo NEVER..!!

  Nitajinukuu;


  Kwenye RED ni maeneo ambayo nimeonyesha strength ya CCM ambayo PASCO kakimbia kuyajadili kwa hoja, kuwa CCM imeamua kujijenga UPYA na kufukuza manyang'au wote waliokuwa wanaharibu IMAGE ya Chama, manyang'au hayo yamenunua chaka jipya na wanalipa watu wawasafishe kwenye vyombo vya habari na mitandao ya kijamii...na bahati mbaya wamejitokeza watu waliojitoa ufahamu na kukubali kutumika..na hakika HAKUNA DENI BAYA KAMA DENI LA TUMBO linawatesa wengi katika watu hata wale wenye elimu zao.

  Kwenye KIJANI ni maswali ambayo PASCO kwa maksudi ameyakimbia, HASEMI lolote kuhusu UPINZANI, hasemi kuhusu THE DON na makando kando yake...anasema tu kuwa anachukia RUSHWA lakini hasemi DON LOWASSA amejiandaaje kupambana na Rushwa hata awe bora kuliko MAGUFULI wa CCM..

  1. LOWASSA wa CHADEMA na UKAWA ni kielelezo cha ubovu, uchafu na uovu uliokuwa unasababisha harufu mbaya ndani ya CCM kwa zaidi ya miaka 30 aliyokuwa anatumikia Serikali kupitia chama hicho. He re

  2. LOWASSA hawezi kuwa Kiongozi wa Mabadiliko (hayo ambayo PASCO) anawaaminisha Watanzania, kwani alikuwa katika mfumo huo kwa zaidi ya miaka 30 na hakubadilisha chochote, leo LOWASSA amebadilika nini..?

  3. LOWASSA ni MWIZI, NI MLA RUSHWA MKUBWA na nimeandika haya nikitumia ID yangu kamili, na nitasema haya popote pale..na kwa fedha zake za wizi amekuwa akinunua watu wa kumsafisha kila uchao, nina mashaka ndugu yangu PASCO is on the list.

  4. LOWASSA anasimama na mwenzie SUMAYE kukosoa Serikali ambayo maamuzi makubwa yaliyoangamiza TAIFA walishirikia kuyapitisha kama sio KUYASIMAMIA ili yapitishwe na Serikali..leo wamekuwa wasafi ghafla kwa kuwa wamehamia UPINZANI..kama sio UJUHA ni nini..?

  5. LOWASSA ameishi, ametenda na ameendelea kutetea IMANI kuwa pesa ndio kila kitu, imani ambayo PASCO and the TEAM MABADILIKO imeendelea kuamini, hawezi kuishi nje ya IMANI hiyo ambayo inapingana na IMANI ya UADILIFU...na tunachotaka watanzania ni MTU MUADILIFU ili akanyooshe mambo yaliyopinda ndani ya Serikali..

  5. HAKUNA ushahidi ama rekodi yeyote ambayo inaonyesha LOWASSA amebadilika, bali upo USHAHIDI na REKODI ambazo zinathibitisha kuwa LOWASSA ni MWIZI, MLA RUSHWA, MUONGO na FISADI PAPA..hana moral authority ya kukemea Rushwa.

  PASCO..,narudia tena kuwa WATANZANIA sio WAJINGA: tumekusikia, tumetafakari na tumeamua MAGUFULI ndio ajaye. Hatuko tayari kumpa FISI ulinzi wa BUCHA.

  VIDEO: KINANA na CCM MPYA

  https://youtu.be/bSG2TBeCS_A   
 2. nkulikwa

  nkulikwa JF-Expert Member

  #2
  Sep 21, 2015
  Joined: Jul 21, 2015
  Messages: 723
  Likes Received: 794
  Trophy Points: 180
  Hakunawa mwanasiasa ambaye si mwizi. CCM miaka Yao ya kutawala inatosha. Hawana jipya isipokuwa hadaa na uongo. Ni aibu kuzungumza Maji Leo na Umeme. Inatosha
   
 3. DALLAI LAMA

  DALLAI LAMA JF-Expert Member

  #3
  Sep 21, 2015
  Joined: Jan 31, 2012
  Messages: 8,614
  Likes Received: 402
  Trophy Points: 180
  Nani kauza nyumba za serikali kwa wake zake?

  Hasara kubwa fidia samaki wa magufuli?

  Mafisadi Chenge,Ngeleja,Tibaijuka ni vyoo vya ccm vyenye harufu kali waliopitishwa kuwania ubunge.

  Ccm imehusika na ESCROW.

  Lowassa taka usitake ndio chaguo letu walala hoi.

  Ikulu siyo ya mzee wako utunyime.
   
 4. nkasoukumu

  nkasoukumu JF-Expert Member

  #4
  Sep 21, 2015
  Joined: Nov 27, 2010
  Messages: 774
  Likes Received: 167
  Trophy Points: 60
  juliana shonza acha ubinafsi ccm ikiingiamadarakani mtanufaika kikundi cha watu wachache na matajiri voda fasta watazaliwa acha zamu hii tuchague mabadiliko dhidi ya ukale chama chenu kitaendelea kua cha upinzani vilevile huku safari hii kikitumika na chadema dhidi ya ccm
   
 5. T

  Tob0001 JF-Expert Member

  #5
  Sep 21, 2015
  Joined: Jul 26, 2015
  Messages: 333
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Tumesoma na tumeelewa
  Ila Mzee kaishatuingia kwenye mioyo yan katikati ya moyo hakuna namna tutampa Nchi tu
   
 6. Jay One

  Jay One JF-Expert Member

  #6
  Sep 21, 2015
  Joined: Nov 12, 2010
  Messages: 11,707
  Likes Received: 5,590
  Trophy Points: 280
  CCM ndio MAFISI na wezi wakubwa... tena wakubwa sana,

  Ona hapa chini hadi wako na FISI na huyo Kinana, kamaliza tembo wetu...!!!
   
 7. amilyroley

  amilyroley JF-Expert Member

  #7
  Sep 21, 2015
  Joined: Jun 23, 2015
  Messages: 621
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Jully Ndoa lin? Tuliona Pete tu na mida inakwenda. Angalia dada usisindikize siasa kutafuta shibe ya watoto wa vigogo ukaikosa ndoa yako takatifu
   
 8. Jay One

  Jay One JF-Expert Member

  #8
  Sep 21, 2015
  Joined: Nov 12, 2010
  Messages: 11,707
  Likes Received: 5,590
  Trophy Points: 280

  Umeona nani fisi sasa..?
   
 9. Ngalikihinja

  Ngalikihinja JF-Expert Member

  #9
  Sep 21, 2015
  Joined: Sep 1, 2009
  Messages: 17,559
  Likes Received: 5,123
  Trophy Points: 280
  Juliana Shonza

  Haupo tayari kumwachia fisi ulinzi wa bucha, lakini upo tayari kumfanya fisi kuwa mchungaji wa huo mfugo unaliochinjwa na kuletwa buchani, upo tayari kumafanya fisi kuwa mchinjaji wa huo huo mfugo na vile vile upo tayari kumpa fisi kuwa muuza bucha.... Hatariii ya ndorobo....

  Do you see chances mnazompa huyo mchungaji-fisi, mchinjaji-fisi na muuzaji-fisi..?? Kumbuka mlinzi-fisi, bucha linakuwa limefungwa na chances za kuibwa ni ndogo sana.

  Juliana Shonza

  Ahadi anazotoa Magufuli ni kwa namna nyingine kumpiga vijembe JK. Haiwezekani eti nimpe kura Magufuli, simply kashangaa hakuna kiwanza cha samaki Tanga hadi Mtwara, ANAMSHANGAA NANI..?? CCM, WANANCHI AU JK..?? Anashangaa habari ya dawa kukosekana hospitali, anashangaa watoto kukaa chini... HIVI ANAMSHANGAA NANI..??? Swezi ishi kwa ahadi.. Tena nyingine zimeshindikana kuzitekeleza miaka michache iliyopita..
  1. Ahadi ya GRIDI ya TAIFA Songea, Kigoma na Kagera... Hakuna hata anayechakata
  2. Meli ziwa victoria hakuna...
  3. Ahadi ya viwanja vya ndege hakuna...

  Siwezi kumchagua kwa ahadi anazotoa, ambazo nyingine mlitakiwa muwe mmeshazitekeleza ndani ya miaka 50 iliyopita....
   
 10. Capt Tamar

  Capt Tamar JF-Expert Member

  #10
  Sep 21, 2015
  Joined: Dec 15, 2011
  Messages: 7,435
  Likes Received: 4,474
  Trophy Points: 280
  Hoja zako ni nzito kichwani kwako mwenyewe,ila kwenye mizani ni nyepesi mno,na upande mwingine zinakuacha uchi kabisa!! Kwanza naomba nikutambue kama mpizani muasi uliyejiunga na ccm chafu huku ikiwa bado ni chafu!! Ningekuelewa walau kama ungerudi ccm kipindi hiki ambapo wale tuliowaita wachafu wameondoka huko(si kuondolewa)sasa leo unasimama kumtukana lowassa ambaye ulimfuata ccm na akakukimbia na kukuacha huko??absurd!! Pili nikuulize tu je chadema unayoichukia ni hii yenye lowassa na sumaye au ni ile ya slaa na zitto?maana uliikimbia ya slaa na unaitukana ya lowassa,unafiki ni kuichukia ukawa ya lowassa na kuipenda ccm ya chenge,
   
 11. telex

  telex JF-Expert Member

  #11
  Sep 21, 2015
  Joined: Apr 26, 2015
  Messages: 406
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 35
  anashangaa utadhani alikua haiishi tanzania.
   
 12. b

  bato JF-Expert Member

  #12
  Sep 21, 2015
  Joined: Dec 20, 2012
  Messages: 2,549
  Likes Received: 1,051
  Trophy Points: 280
  Kura yangu nitampa Magufuli. Lakini sioni vibaya UKAWA wakishinda kwa Urais,huku tukigawana viti vya ubunge na udiwani. Sifa kuu ya kuwa mgombea ni kuwa MTANZANIA. Tanzania ni yetu wote.
   
 13. wirewizard1

  wirewizard1 Senior Member

  #13
  Sep 21, 2015
  Joined: Jun 28, 2015
  Messages: 151
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Maneno mengi...!!!! ?CCM Wananchi wameshaochoka?....Ahadi za uongo kila leo....Its over kwa CCM....
   
 14. mpalu

  mpalu JF-Expert Member

  #14
  Sep 21, 2015
  Joined: Sep 15, 2010
  Messages: 2,494
  Likes Received: 81
  Trophy Points: 145
  Mafisi yashatulindia sana bucha letu....heri kumkabidhi bucha fisi mmoja kuliko kukabidhi kwa mamia ya mafisi......KURA YANGU KWA FISI MMOJA...........
   
 15. Mhandisi Mzalendo

  Mhandisi Mzalendo JF-Expert Member

  #15
  Sep 21, 2015
  Joined: Aug 23, 2010
  Messages: 3,099
  Likes Received: 2,130
  Trophy Points: 280
  Moyoni mwako ni dhahiri unajua unachotetea si sawa.... Mabadiliko ni lazima mwaka huu tumeamua kuchagua fisi mmoja tutajua jinsi ya kumtazama asile nyama buchani kuliko kuchagua mchungaji wa mafisi 300 atulindie bucha letu..... Mafisi yakipata njaa yatamla kuanzia mchungaji mpaka bucha zima....
  MABADILIKO NJE YA CCM NI LAZIMA....
   
 16. l

  logician mkuu JF-Expert Member

  #16
  Sep 21, 2015
  Joined: Jun 2, 2014
  Messages: 795
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
 17. U

  UGORO87 JF-Expert Member

  #17
  Sep 21, 2015
  Joined: Mar 7, 2014
  Messages: 702
  Likes Received: 200
  Trophy Points: 60
  Ivi shonza ufisadi wa nchi hi ni richmond tu?vp kuhusu ripot ya prof asad ya uuzaji wa nyumba za serikali.funga mdomo.
   
 18. Jp Omuga

  Jp Omuga JF-Expert Member

  #18
  Sep 21, 2015
  Joined: Jan 16, 2012
  Messages: 2,783
  Likes Received: 939
  Trophy Points: 280
  Juliana were you prematurely:

  ignorance.jpg
  Meanwhile you have got to understand that:
  143210_600.jpg
   
 19. a

  aiai654 JF-Expert Member

  #19
  Sep 21, 2015
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 3,860
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 133
  Mifisi inaendelea kula bucha hadi leo. Tusiichague tena Lowassa atosha
   
 20. J

  Jozi 1 JF-Expert Member

  #20
  Sep 21, 2015
  Joined: Aug 16, 2015
  Messages: 5,053
  Likes Received: 2,294
  Trophy Points: 280
  Nkulikwa,
  Nimepata fadhaa na andiko lako.
  Hakika umepotoka na umepotoka haswaa.

  Katika kumtetea Lowassa/Ukawa na tuhuma za rushwa/ufisadi unasema kirahisi tu kuwa hakuna mwanasiasa asiye kuwa mwizi kwa hiyo miaka ya ccm imekwisha. Waondoke.

  Kwa hoja yako hii, kwa kuwa hakuna wanasiasa ambao sio wezi basi ni wakati wa sisi kuchagua wezi wengine wachukue nchi ili nao wapate zamu yao ya kutuibia.

  Mawazo duni na potofu.
  Kwa hiyo mabadiliko unayoyataka wewe ni ya kutoa mwizi mmoja na kuleta mwingine kwa sababu tu yule aliyekuwepo keshatuibia kwa miaka mingi.

  Ni aibu sana.
   
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
Loading...