Kinana yuko wapi na wakuu wenzie, wamuondolee January majukumu haya

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
33,463
39,929
Kuna masuala mazito na magumu ya Kitaifa. Hayapaswi kuzungumziwa na mtu wa wadhifa wa Makamba. Alifaa (kwa CCM) wakati wa kampeni zao, lakini sasa inabidi watu more authoritative and competent kuanza kuzungumzia haya.

Binafsi sijui ni kwa kiasi gani JM anazungumza kwa niaba ya uongozi wa chama au kampeni za Magufuli. Maana pia wakati mwingine amezungumza kama Naibu Waziri wa Mawasiliano...
 
wapo wamejifungia ofisini na kikwete wanachakachua matokeo hawajui kuna moto unakuja
 
huyu kijana asipothibitiwa na kina Kinana na Mangula anaweza kuliingiza taifa hili kwenye sintofahamu kwa kauli zake za kijinga...we need to stop this guy because this is too much now....anaongea kama yeye ndio amiri mkuu wa majeshi....January Makamba please stop this madness
 
Mzee mliona sisi wajinga ,tulioamua kutumia silaha yoyote kumpiga adui. Huu uchafu hauwezi kutoka kirahisi kwa sababu kuna watu hawawezi kuishi bila kuwa viongozi! CCM NI SHIDA,WATANZANIA NI SHIDA
 
Mzee unahangaika kweli dah. Pole sana mkuu. ccm ndo inakufa hivyo. watu wamestukia wakamsukumia makamba. hata hivyo kajitahidi dogo. sema wapikaji wa kura waliongeza chumvi nyingi.
 
MMM naona roho yako imetulia sasa... Binafsi naona turudi kwenye siasa za chama kimoja tu, Huu unaoendelea sasa ni unafiki
 
Nadhani mnataka aongee kauli zinazowafurahisha au zile ambazo zinaendana na fikra zenu!

Kama mliweza kumsema Kikwete hafai wakati ndiye mwenye nguvu ya kisiasa kama Mwenyekiti wa chama na pia nguvu ya kijeshi kama Amiri Jeshi Mkuu. Itakuwa huyu Makamba Jr?

Hata Kama Kinana angekuwa ndiye anayesimama mbele ya media, nafahamu mngesema pia hafai.

Kama CCM haifai kama mnavyotueleza na kutuaminisha, sasa unategemea viongozi wake ndiyo watafaa?

Hebu tuache unafiki.
 
Nina maumivu kweli, yaani watanzania bado wanaipa ccm ushindi mkubwa! Hivi hawajui kuwa mgema akisifiwa tembo hulitia maji! Sasa ngoja muone ccm itakavyolewa sifa hawatajali sana matatizo ya wananchi, sasa ni mwendo wa miposho na mishangingi. Kule Antony Diallo sasa ana uhakika wa ku clear madeni yake yote bank na kwingine anakodaiwa.
 
Mzee Mwanakijiji,
Mimi nafikiri kuwa kwa sehemu kubwa JM amebeba nafasi ya Nape na hii inaweza tokana na uzito wa kampeni, labda Jimbo la January lilikuwa na nafuu kidogo ukilinganisha na Nape, Hivyo basi ikapelekea yeye kuchukua nafasi hiyo, Hapo kwenye nyekundu sijaelewa kwanini unafikiri anazungumza kama waziri kwa masuala yanayohusiana na CCM?

Sidhani kama kuisemea CCM kuna tatizo lolote na hasa kama wao watakuwa wamekaa vikao na kukubaliana aende akaseme nini.
 
Mwanakijiji nakusubiri uanze kuilalamikia na kuiponda serikali ya magufuli uliyempigia debe.
 
Ni kweli huyu Januari Makamba ni janga. Siajaelewa huyu bwana mdogo anaongea kama nani hasa? Je, ni kama Campaign Manager wa Magufuli, Naibu Waziri wa Mawasiliano au Mbunge mteule wa Bumbuli au msemaji wa CCM?

Wako wapi watu wazito ndani ya CCM kina Kinana, Mangula au Vuvuzela wao a.k.a Nepi Nauye? CCM inaonekana hamjitambui, hamjielewi, mmelewa madaraka na kwa kweli mnahitaji ushauri nasaha! Bila hivo hii nchi mnataka kuitumbukiza kwenye janga la kitaifa!
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom