Kinana: Wanaotaka urais 2015 wamvuruga Kikwete | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kinana: Wanaotaka urais 2015 wamvuruga Kikwete

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Msharika, Jan 27, 2012.

 1. M

  Msharika JF-Expert Member

  #1
  Jan 27, 2012
  Joined: May 15, 2009
  Messages: 936
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Palipo na Moshi ndani kunawaka moto.

  Kama Kinana naye amefika mahali pa Kusemea adharani ujue kuwa kuna mambo ndani ya cham achetu hayaendi vizuri.
  Wanachama tuombe kuonanan na mwenyekiti wetu hatutolee haya matatizo.

  Source: Kinana: Wanaotaka urais 2015 wamvuruga Kikwete
   
 2. a

  adobe JF-Expert Member

  #2
  Jan 27, 2012
  Joined: May 6, 2009
  Messages: 1,666
  Likes Received: 290
  Trophy Points: 180
  ni kwa kiasi gani jk,el na wengineo walivuruga uongozi wa mkapa hadi kupelekea kifo cha mwalim.mkapa alikuwa na wakati mgumu sana.maana hawa jamaa walimlazimisha hata kutoa pesa kwenye akaunt ya epa na kusababisha kumhamisha gavana balali na badae kumzushia kifo
   
 3. mbogoshi ya boganga

  mbogoshi ya boganga Member

  #3
  Jan 27, 2012
  Joined: Jan 24, 2012
  Messages: 33
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  ya magamba mwachie magamba
   
 4. Ringo Edmund

  Ringo Edmund JF-Expert Member

  #4
  Jan 27, 2012
  Joined: May 10, 2010
  Messages: 4,895
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 0
  uaneni sisi tutakuja kuzika.
   
 5. Lyceum

  Lyceum JF-Expert Member

  #5
  Jan 27, 2012
  Joined: Oct 1, 2009
  Messages: 915
  Likes Received: 265
  Trophy Points: 80
  Haha ah ahaha hatuna muda huo mkuu. Wataliwa na tai tu hawa. Wanatudhalilisha sana hawa magamba. Wanataka tukose hata nguo za ndani kwa wizi wanalifanyia taifa. Naomba futa kauli kuwa tutawazika mkuu. Nakuheshimu sana
   
 6. Graph Theory

  Graph Theory JF-Expert Member

  #6
  Jan 27, 2012
  Joined: Jul 2, 2011
  Messages: 3,803
  Likes Received: 1,115
  Trophy Points: 280
  CCM oyeeee!!! Zidumu fikira za mwenyekiti.
   
 7. M

  MAMENGAZI JF-Expert Member

  #7
  Jan 27, 2012
  Joined: Dec 31, 2010
  Messages: 781
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 35
  what goes around comes around, ni wakati wake wa kuonja joto ya jiwe!!!! si aliwaendekeza hao washkaji zake sasa ataona rangi zote, aendelee kuwachekea tu watampanda kichwani.
   
 8. M

  MAMENGAZI JF-Expert Member

  #8
  Jan 27, 2012
  Joined: Dec 31, 2010
  Messages: 781
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 35
  Wee Ringo, nani anamuda huo, wauane wazikane wenyewe
   
 9. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #9
  Jan 27, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  [TABLE="class: contentpaneopen"]
  [TR]
  [TD="class: contentheading"][/TD]
  [TD="class: buttonheading, align: right"][/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  [TABLE="class: contentpaneopen"]
  [TR]
  [TD="class: createdate"]Thursday, 26 January 2012 21:16[/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD]
  ASEMA WANAVURUGA UTENDAJI WA SERIKALI KUTEKELEZA AHADI ZAKE

  Na Leon Bahati

  ALIYEKUWA Mkurugenzi wa Kampeni za Rais Jakaya Kikwete wakati akigombea urais kwa CCM katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2010, Abdulrahman Kinana, amesema vigogo wa chama hicho walioanza kampeni za urais sasa wanavuruga utendaji wa serikali.Akizungumza jana katika ziara yake ya kutembelea matawi ya CCM mkoa wa Dar es Salaam, Kinana alisema vigogo hao ni wabinafsi, wanaivuruga nchi na hawana lolote wanalolifanya kwa maslahi ya chama hicho tawala.


  "Sasa hivi Rais Kikwete ana miaka mingine minne mbele kabla ya kumaliza uongozi wake na CCM ina kero nyingi za kushughulikia ili kutekeleza ilani yake, halafu wengine wanazungumzia urais sasa," alisema Kinana

  Kinana alizitaja kero hizo kuwa ni elimu, afya, maji, barabara, mazingira, maisha magumu yanayosababishwa na mfumuko wa bei na kushuka kwa thamani shilingi.

  Kauli hiyo ya Kinana ambaye ni mlezi wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam, imekuja katika kipindi ambacho baadhi vigogo wa CCM wamekuwa wakipigana vikumbo kuwania nafasi hiyo ya juu ya uongozi wa nchi, huku wakitumia majukwaa mbalimbali ikiwemo vyombo vya habari, makanisa na misikiti kujipigia kampeni.

  Akizungumzia harakati za vigogo hao kugombea Urais ndani ya CCM Kinana alisema; "Wote wanaozungumza kwenye vyombo vya habari, hawasemi kwa manufaa ya wananchi wala maslahi ya wanachama bali kwa maslahi yao binafsi."


  Alifafanua kwamba, masuala ya kuutaka urais siyo ya kuzungumzia sasa kwani bado Rais Kikwete ana miaka minne ya kuwa madarakani huku akikabiliwa na kazi kubwa ya kutatua matatizo ya wananchi katika kipindi hiki ambacho taifa linakabiliwa na hali mbaya kiuchumi.

  "Je, huu kweli ni wakati wa kuyazungumzia hayo? (masuala ya kuwania urais)," alihoji Kinana.

  Kinana alitahadharisha kuwa mazingira wanayoyajenga vigogo hao yatawafanya wanachama na wananchi kwa ujumla, wawachukie utakapowadia wakati wa uchaguzi mwingine.

  Alisema anasikitishwa na hali hiyo hasa ikizingatiwa kuwa wanaoanza kupiga kampeni za urais ni watu wazito ndani ya nchi na ni wajumbe wa vikao vikuu ndani ya CCM, lakini wanaona kusema kupitia vyombo vya habari watasikika nchi nzima.

  "Hao mnaowasikia wakisema kwenye vyombo vya habari ni wajumbe wa vikao tena vikubwa na hakuna anayewazuia. Wanaona wakisema kwenye vikao, wananchi hawatasikia," alifafanua.

  Kinana alisema hayo akijibu swali aliloulizwa na mmoja wa wanachama wa CCM tawi la Buguruni, aliyetaka kujua kwa nini vigogo wa chama hawaonyeshi mshikamano kwa kutotumia vikao vya chama kujali masuala mazito kama hayo, badala yake wanakwenda kwenye vyombo vya habari?

  "Viongozi wa juu muwe na mshikamano, nendeni kwenye vikao, mna vikao vya kusemea, acheni kusema kwenye vyombo vya habari," alionya Kinana

  Kinana aliwahakikishia wana CCM mkoa wa Dar es Salaam kwamba, suala hilo atalifikisha kwenye chama ili lifanyiwe kazi kulingana na taratibu zake.
  Katiba mpya

  Kuhusu mchakato wa mabadiliko ya Katiba, Kinana alisema Rais Kikwete amekuwa akifanya kazi yake vizuri ikiwemo kuwashirikisha wadau mbalimbali kuhusu jambo hilo na amekuwa akikutana nao Ikulu ili kujenga amani na utulivu nchini.

  Aliwataja wadau hao kuwa ni pamoja viongozi wa vyama vya upinzani.
  Alisema Rais ni kiongozi wa nchi na anatumia nafasi hiyo kupata maoni kutoka kwa watu mbalimbali ili kuwa na katiba mpya iliyo bora.

  Kwa mujibu wa Kinana, Rais Kikwete amekutana na viongozi wa vyama vya upinzani na tayari amepata maoni ya CCM, kupitia Kamati yake Kuu (CC).Hivyo, alisema Rais anakutana na makundi yote ya watu bila upendeleo ili kujenga mshikamano katika kuandika katiba mpya.

  Alifafanua kwamba, kinachofanyika sasa ni kuunda mchakato wa namna maoni ya katiba hiyo yatakavyochukuliwa kutoka kwa wadau mbalimbali.

  Hata hivyo, alisema kwa sasa Rais anasubiri wabunge wafanyie marekebisho baadhi ya vipengele vya Sheria ya Mchakato wa Mabadiliko ya Katiba ya mwaka 2011.Kinana alisema baada ya marekebisho hayo, Rais ataunda tume ya kukusanya maoni itakayojumuisha watu wa kada zote bila kujali itikadi za vyama vyao vya siasa.

  Akerwa na 'uheshimiwa'
  Katika hatua nyingine Kinana alisema amekuwa akikerwa na tabia ambayo katika siku za karibuni imeshika kasi, kwa viongozi ndani ya chama kuitwa "waheshimiwa."

  Alisema hata kwenye mikutano yake na wanachama jijini Dar es Salaam amekuwa akiitwa "mheshimiwa" ambalo hakubaliani nalo na kushauri neno kuwa sahihi linalopaswa kutumika ni "ndugu."

  Rushwa ndani ya CCM
  Kinana alisema kuwapo kwa vitendo vya rushwa ndani ya chama ni tatizo linachangia kwa kiasi kikubwa kupata viongozi wasiofaa ndani ya chama, hivyo kusisitiza kuwa safari hii, wameamua kulivalia njuga.


  Alisema wanaotaka uongozi kwa rushwa hawafai kwa sababu hawana malengo mazuri ya chama bali binafsi.

  Kinana alionya kwamba, kuna baadhi ya wanachama ambao huwashawishi wagombea ili wawape fedha kwa ajili ya kuwapigia kampeni na kuhakikisha kuwa wanashinda.

  Alisema mwanachama anayetaka fedha ili amchague kiongozi hana malengo mazuri na chama hicho, hivyo naye anapaswa kuchukuliwa hatua kwa vile kufanya hivyo ni kukisaliti chama.

  CCM kufuta unafiki
  Katika hatua nyingine, CCM mkoa wa Dar es Salaam umesema katika uchaguzi ndani ya chama na jumuia zake unaotarajia kufanyika mwezi ujao, wamepania kuondoa aina zote za unafiki.

  Katibu wa CCM mkoa wa Dar es Salam, Said Mihewa alisema katika kuchuja wagombea, watahakikisha haki inatendeka na kipaumbele kitatolewa kwa wanachama kufanya uamuzi.

  Alisema iwapo vikao vya chini, tawi na kata vitamwelezea mwanachama yeyote kwamba hafai kuwa kiongozi, watawaita na kuwakutanisha ana kwa ana na wanayemtuhumu ili wafafanue jinsi asivyofaa.

  "Tutawaita na kuwakutanisha na mnayesema hafai, mseme mbele yake kuwa hafai! Na yeye ajieleze kwa nini anasema anafaa?" alisema Mihewa.

  Mchakato wa uchaguzi wa ndani wa CCM unatarajiwa kuanza mwezi ujao na kumalizika Oktoba mwaka huu.


  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
   
 10. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #10
  Jan 27, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  Wakati Wa Rais Mkapa mbona hakukuwa na watu kama hawa wa kusema hayo?

  CCM Unafiki ni sababu ya Ulaji wote walikuwa Wajamaa sasa ni makambale
   
 11. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #11
  Jan 27, 2012
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 308
  Trophy Points: 180
  Kikwete asitafute Mchawi wala visingizio..
  Afanye kazi na kutekeleza ahadi za Trilioni 90 alizoahidi Watanzania!...
  Jee ni ngapi zimetekelezwa, na huku akiwa amebakiza less than miaka 3 ?

  AHADI - ALIZOTOA Kikwete KWA WATANZANIA 2010...


  1. Kujenga reli mpya kutoka Dar es Salaam mpaka mikoa ya Kanda ya ziwa - Nzega, Tabora
  2. Mkoa wa Tanga kuwa Jiji la Viwanda - Tanga mjini
  3. Tabora kutumia maji ya Ziwa Victoria - Igunga
  4. Kulipa madeni ya chama cha Ushirika mkoa wa Shinyanga (SHIRECU) - Shinyanga
  5. Kumaliza migogoro ya Ardhi nchini - Dodoma
  6. Wakulima kuacha kutumia jembe la mkono - Dodoma mjini
  7. Kuwapatia trekta wakulima - Kata ya Mrijo, Dodoma
  8. Wananchi kutoondolewa kwenye Ranchi ya Misenyi - Kagera
  9. Kujenga Uwanja wa Ndege Misenyi - Kagera
  10. Kupanua Uwanja wa Ndege Bukoba - Bukoba Mjini
  11. Kujenga uwanja wa ndege mkubwa Kigoma - Kigoma Mjini
  12. Mtukula kupatiwa umeme kutoka Uganda - Kagera
  13. Mikoa ya Kagera, Kigoma, Lindi, Rukwa na Ruvuma kuunganishwa katika gridi ya taifa ya umeme - Kagera
  14. Kuimarisha Takukuru kwa miaka mitatu - Kagera
  15. Hukumu kwa waliopatikana na hati ya kuua albino - Mbeya
  16. Kununua meli kubwa kuliko MV Bukoba - Kagera
  17. Kuanzisha benki ndogondogo kwa ajili ya wajasiriamali
  18. Serikali kuvisaidia vyama vya ushirika - Mwanza
  19. Kuimarisha usalama Ziwa Victoria na Ziwa Tanganyika kwa kupeleka kikosi maalum chenye vifaa kupambana na wahalifu - Mwanza
  20. Wilaya ya Geita kuwa hadhi ya mkoa Januari mwakani - Geita
  21. Kulinda muungano kwa nguvu zote - Pemba
  22. Kuwajengea nyumba waathirika wa mafuriko Kilosa - Morogoro
  23. Kununua meli mpya kubwa Ziwa Nyasa - Mbeya mjini
  24. Kujenga bandari Kasanga – Rukwa
  25. Kumaliza tatizo la walimu miaka mitano ijayo - Songea
  26. Kufufua mgodi wa makaa ya mawe Kiwira - Mbeya
  27. Kuzuia hatari ya kisiwa cha Pangani kuzama - Tanga
  28. Kununua bajaji 400 kwa ajili ya kubeba wajawazito hasa vijijini - Iringa
  29. Kujenga barabara yenye kiwango cha lami kutoka Same mpaka Kisiwani – Kihurio na kuiunganisha na barabara kuu ya Moshi - Dar es salaam - Same mkoani Kilimanjaro
  30. Kumaliza tatizo la maji katika wilaya ya Same - Same Mjini
  31. Kuboresha barabara za Igunga - Tabora
  32. Kusambaza walimu 16,000 katika shule za sekondari zenye upungufu makubwa wa walimu - Kisesa Magu
  33. Kununua vyandarua viwili kwa kila kaya - Mbeya Mjini
  34. Kuzipandisha hadhi hospitali maalumu saba nchini kuwa za rufaa ili kuipunguzia mzigo Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MHN) - Hydom Manyara
  35. Kulinda amani nchini kwa kuzuia chokochoko za kidini, kikabila na kisiasa - Musoma
  36. Kulinda haki za walemavu - Makete
  37. Kujenga baabara ya Njombe - Makete kwa kiwango cha lami,urefu wa kilomita 109 - Iringa mjini
  38. Kujenga barabara Musoma – Mto wa Mbu Arusha - Arusha
  39. Kuanzisha jimbo la Ulyankulu- Shinyanga Mjini
  40. Kujenga barabara ya lami Manyoni-Kigoma – Kaliua,Tabora
  41. Kukarabati barabara ya Arusha Moshi - Arusha Mjini
  42. Kuboresha barabara ya Handeni, Kondoa, mpaka Singida - Dodoma
  43. Kuwafidia wanakijiji ng'ombe waliopotea wakati wa ukame mwaka 2009 - Longido
  44. Vijiji vyote vilivyoko kilomita 15 kutoka kwenye bomba kuu la mradi mkuu wa maji wa Ziwa Victoria - Shinyanga-Kahama kuunganishiwa maji - Shinyanga
  45. Tatizo la umeme kufikia kikomo Novemba mwaka huu mkoani Arusha – Arusha mjini
  46. Kukopesha wavuvi zana za kilimo - Busekera, Wilaya ya Musoma
  47. Kuwapatia maji wakazi wa Wilaya ya Longido - Longido
  48. Kujenga barabara ya lami kupitia pembezoni mwa Hifadhi ya Taifa ya Seregenti – Ngorongoro
  49. Utekelezaji wa mpango wa maendeleo ya kilimo kuwasaidia wafugaji kuweza kupata na kutunza mifugo yao vizuri - Mbulu mkoani Manyara
  50. Kusambaza maji nchi nzima - Babati vijijini
  51. Kusambaza umeme, utoaji wa huduma za afya, na uboreshaji wa kilimo cha umwagiliaji na utoaji ruzuku kwa wakulima. mwaka 2010-2015 - Babati vijijini
  52. Kuongeza mara tatu idadi ya wananchi wanaonufaika na ruzuku ya pembejeo za kilimo kwa mfumo wa vocha - Iringa
  53. Kuhakikisha Isimani inapata maji ya uhakika - Iringa
  54. Kuiwekea lami barabara inayokwenda katika Hifadhi ya Taifa ya Ruaha, ambayo ndiyo hifadhi kubwa kuliko zote Tanzania - Iringa
  55. Kulinda usalama wa wananchi kwa ujumla ili kudumisha amani na sifa ya nchi -Ifunda
  56. Kutokomeza malaria 2015 - Bunda, mkoa wa Mara
  57. Kuwapa wanawake nafasi zaidi - Kilolo, Iringa
  58. Ahadi kuisadia Zanzibar kuendeleza miradi mbalimbali ya kijamii - Kibandamaiti Mjini Zanzibar
  59. Kuipandisha hadhi hospitali ya Mnazi Mmoja Zanzibar kuwa ya rufaa - Kibandamaiti mjini Zanzibar
  60. Kuisaidia Zanzibar kila panapohitajika msaada - Kibandamaiti
  61. Serikali kujenga upya bandari ya Mbambabay - Ruvuma
  62. Ununuzi wa Meli mpya yenye uwezo wa kubeba tani 400 - Mbambabay Ruvuma
  63. kufufua chama kikuu cha ushirika cha wakulima wa Mbinga (MBICU) – Ruvuma
  64. Ahadi Rais wa Marekani Barack Obama kuimwagia misaada Tanzania – Ruvuma
  65. Ahadi hakutakuwa na umwagaji wa damu baada ya uchaguzi-Dar es Salaam
  66. Mtwara kuwa mji wa Viwanda – Mtwara
  67. Ahadi ujenzi wa kwanda cha dawa ya kuua viluilui vya mbu - Kibaha
  68. Hospitali ya Tumbi kuwa ya mkoa - Kibaha
  69. Halmashauri ya manispaa ya Kibaha kutenga eneo maalumu la viwanda - Kibaha
   
 12. W

  WildCard JF-Expert Member

  #12
  Jan 27, 2012
  Joined: Apr 22, 2008
  Messages: 7,477
  Likes Received: 70
  Trophy Points: 145
  Kikwete hakuacha kuusaka Urais tangu mwaka 1995. Alitumia nyenzo za kila namna vikiwemo vyombo vya habari, mtandao hatari na katili sana, mapesa machafu kabisa,... Hatukusikia Kinana akiyasema haya na baadae akawa meneja wa kampeni isiyo rasmi ya Urais wa KIkwete. Waliyaanzisha haya wakidhani yataisha kirahisi?
   
 13. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #13
  Jan 27, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  Sasa 'Urais 2015' umekuwa wimbo wa taifa.

  Nchi hii ina matatizo lukuki yanayohitaji kuongelewa.


  Mwanachama kuonyesha dhamira ya kugombea nafasi fulani katika chama sio kosa, unless kama mnabadilisha katiba ya chama sasa.

  Kila kiongozi sasa amekuwa akicopy hili la 'Urais 2015'kama vile ni kosa la jinai.

  Watanzania msidanganyike sio kinana wala pinda wanaamini wanayoyasema, hii yote ni uwoga kwamba pengine mtu ambae si wa kambi yao

  huenda akachukua nafasi hiyo na wao kuwa na wakati mgumu katka sera zao za kifisadi.
   
 14. HISIA KALI

  HISIA KALI JF-Expert Member

  #14
  Jan 27, 2012
  Joined: Oct 26, 2010
  Messages: 694
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kuwa na mipango ya maisha ni kitu cha kawaida. Binafsi sina tatizo na mtu kutamani kuwa rais wa Tanzania.

  Tatizo ni pale watu wanaanza kupiga kampeni za waziwazi na kuacha kushughulika na matatizo yanayowakabili wananchi kwa sasa.

  Miaka minne ni muda mrefu sana. Kwa kweli ni kitu cha kushangaza kuona watu wanafanya kampeni za kuutaka urais sasa wakati uchaguzi utakaofanyika miaka minne ijayo. Sijui wanataka huo urais kwa faida ya nani? Kama ni kwa faida ya wananchi wa Tanzania nadhani hawako sahihi. Wananchi wametoka kupiga kura mwaka mmoja uliopita, sasa wanataka kuona maisha yao yanaboreshwa sio kupigiwa kelele za kuchagua rais tena wakati muda wake bado ni mrefu.

  Mimi naona kuna tatizo hapa.

  Sasa hivi hakuna wa kumwambia mwenzake acha hiyo hoja kwani muda wake bado.

  Hii ina maana hakuna leadership kwenye chama cha mapinduzi. Lazima kuwa na kiongozi mkuu wa chama ambaye akisema haya ni mapanya hakuna mtu mwingine wa kusema hapana sio mapanya.

  nidhamu ndani ya chama cha mapinduzi na serikali imepungua sana. Na taasisi yoyote ambayo haina nidhamu tusitegemea chochote cha maana.

  Hata familia ikiwa haina nidhamu kutakuwa na matatizo tu kwani baba atasema hili, mama naye atakuja kusema lile, na watoto wakiona hivyo basi na wao kila mmoja anafanya inavyoona inafaa.

  Uongozi wa juu lazima uwe imara na uwezo wa kukemea utovu wa nidhamu. Kwa maana kwamba uwezo wa kuchukua hatua kali kwa mtu anayekwenda kinyume na taratibu.


   
 15. HISIA KALI

  HISIA KALI JF-Expert Member

  #15
  Jan 27, 2012
  Joined: Oct 26, 2010
  Messages: 694
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  nyingi ya hizi ahadi ni hewa na watu wengi walisema hivyo wakati zilipokuwa zinatolewa.
   
 16. Crashwise

  Crashwise JF-Expert Member

  #16
  Jan 27, 2012
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 22,172
  Likes Received: 862
  Trophy Points: 280
  baada ya kuisingizia chadema kuwa inaifanya serika ishindwe kutekeleza ahadi zake sasa wamegeukiana....
   
 17. p

  petrol JF-Expert Member

  #17
  Jan 27, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 322
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 45
  Kuna jamii ya Watanzania inamheshimu sana mzee Kinana. Wengine wanayao mawazo tofauti maana ndio ubinadamu wenyewe. Lakini katika suala la viongozi wanotaka kuwania uongozi hasa nafasi nyeti na nzito kama Urais ni busara wakajitokeza mapema ili tupate fursa ya kufahamu watakavyoweza kutuondolea umasikini wetu. Kizuri zaidi wangeanza kueleza sera zao. Tusiwavunje mioyo kwa kurejea zama za zidumu fikra. Katika karne ya 21 hatutaki kuuziwa mbuzi ndani ya gunia la kisiasa.
   
 18. OSOKONI

  OSOKONI JF-Expert Member

  #18
  Jan 27, 2012
  Joined: Oct 20, 2011
  Messages: 10,793
  Likes Received: 3,880
  Trophy Points: 280
  kama mlijua ni hewa kura mlimpa za nini????
   
 19. t

  timbilimu JF-Expert Member

  #19
  Jan 27, 2012
  Joined: Sep 2, 2010
  Messages: 4,779
  Likes Received: 151
  Trophy Points: 160
  waulize akina Makame,Kiravu na TISS.
   
 20. Ndallo

  Ndallo JF-Expert Member

  #20
  Jan 27, 2012
  Joined: Oct 1, 2010
  Messages: 7,129
  Likes Received: 1,083
  Trophy Points: 280
  PJ umesahau pia aliwaahidi kule Kigoma kua ataigeza kua Dubai!
   
Loading...