Kinana: Unayakumbuka haya maneno wakati unaga'atuka

Hapo ndo utakapo shangaa kuona ccm wote wakiweka matumaini yao kwa mtu ambaye kimsingi akili yake imeshastaafu.
 
Uamuzi wa CCM kuwateua makada wazee tena ambao walishaamua kwa hiari yao kuachana na siasa inaweza ukawa ni mtaji mzuri kwa vyama vya upinzani kama wataamua kuutumia vizuri.

Haiwezekani na wala haiingii akilini mtu kama Zakhia Meghji ama Kinana ambao walitangazia umma kuwa wanaachana na siasa ili wapumzike ama Mangula waliyemtosa tangu 2006, leo unaamua kuwatwisha mzigo mzito wa uongozi kwenye chama. Hivi waliomba wenyewe kurudi kwenye chama ama wameombwa kuokoa jahazi

CCM INAYOJIDAI KUWA INA HAZINA YA VIONGOZI IMEAMUA KUWARUDIA WAZEE AMBAO HATA DODOMA WALISHATANGAZA WAKATI FULANI KUWA WASTAAFU WATAACHWA ILI WAPUMZIKE.

KWELI SIKIO LA KUFA HALISIKII DAWA.
 
Karudi CCM kuficha madhambi yake. Si mnajua Tanzania ukiwa kiongozi hasa CCM unakuwa juu ya Sheria. Nani anaweza kumuuliza jina la mteja wake waliyepakia meno ya Tembo kwenye meli yake? Kinana anatwambia katika documents za meli yake (B/L) hazikuwa na jina la Shiper! Kweli Tanzania ni zaidi ya tuijuavyo.
 
Tatizo la ccm na watu wake wana ujinga wa kuamini kuwa hakuna chama kingine chenye uwezo wa kuongoza nchi hii isipokuwa ni ccm tu.ujinga ambao umejengeka hata kwa viongozi wa ndani ya chama chenyewe.wapo wanaoamini kuwa bila wao kuongoza hakuna mtu mwingine mwenye uwezo wa kuongoza isipo kuwa ni wao tu.ndiyo yaleyale ya kina Msekwa nimeng'atuka kwenye usipika baada ya muda nimeombwa na wananchi nigombee tena. wenye akiri wakagunduwa janja yake wakamubwaga chini.matokeo yake alikuja kupatikana sipika mzuri hata kuliko yeye mwenyewe.akina John samwel waling'ang'ana kuutaka urais wakatupwa nje na nyerere akapatikana rais mwingine tena mzuri tu.alipo kufa nyerere kwa sababu ya roho iliyowajaa viongozi wa ccm kuwa hakuna mtu mwingine mwenye uwezo wa kuongoza isipokuwa mimi tu.John akaibuka tena ni mimi tu ndiye ninayefaa kuwa rais wa nchi.kamwagwa na mkapa akapatikana rais mwingine mbali na John.pia wapo wengine kama akina Lowassa walikuwepo madarakani wakatimka kwa sababu ya wizi.lakini anavyo utafuta urais utafikiri hakuna mtu mwingine anaye weza kuongoza nchi hii isipokuwa ni yeye tu. yuko tayari kutoa roho ya mtu ili aupate urais.ccm wanashindwa kuelewa kuwa tz bila ccm inawezekana.viongozi wanaorudi madarakani mara mbilimbili wanashindwa kuelewa kuwa hata wasipokuwepo wao ccm itaendelea tu.mbona akina kingunge wameng'atuka ccm inaendelea.ni upuuzi kuamini kuwa bila mimi haiwezekani kama hungezaliwa au ungekufa au hata ukifa leo ina maana ccm nayo itakufa? au tz isingekuwepo? au tz tusingekuwa na rais? au tz tutakosa rais wa kutuongoza?.
 
waliokupo madarakani wameshindwa kuthubutu,ona walivyokuwa wanajigonga walipotangaza mkakati wa kujivua gamba wa siku tisini.
Mtuhumiwa wao no1 alivyomtolea jicho jk na kumuuliza "nini nilichofanya kuhusu richmond ambacho hukijui"Jk akabaki kabung'aa macho,Nape na Mukana wakafyata mkia,labda hawa wanaonekana wanaweza wakamvisha paka kengele.
Kinachonifanya nifuatilie kwa makini ni jinsi gani jini subiani atakavyomkamata makata.Au ndiyo tayari ufalme wao umefitinika?
 
I have no word......hivo ndo baadh ya vitu vinavotakiwa kuwekwa kwenye katiba maana watu hawashibi madaraka.....ooohhh toka jk mpaka jk.....aaaaahh this too much bana
 
1. Mjumbe wa CCM miaka 25
2. Kuachana Kweka na siasa hakutakuwa na madhara kwa chama chake, kwani CCM ina hazina kubwa ya viongozi ambao wana sifa na wanaweza kuongoza chama hicho kuelekea Uchanguzi wa 2015
3. "Uongozi ni kupokezana vijiti, wako wanaCCM wazuri, walio na uwezo mkubwa na sifa za kutosha kuongoza"
4. Anajivunia kufanya kazi na marais wote kuanzia mwalimu hadi JK kwa uadilifu mkubwa na kuheshimiana.

Ushauri wake kwa Viongozi wapya
1. Viongozi wapya ambao wanatarajia kuchaguliwa ndani ya chama chake, iwapo wataona upungufu wake wausahihishe
2. Viongozi wasiwaze nani anafaa kuwa mgombea urasi bali washughulikie kero za wananchi

Nini atafanya baada ya kustaafu
1. Kuona kama anaweza kufundisha
2. Kusoma katika mojawapo ya vyuo vikuu vyetu.

Sasa, imekuwa vipi tena unarudi Jukwaani na kuanza kutuhubiri ulichoamua kukiacha september 2012?

Kweli siasa tamu sana.

nicas kwanini unahangaika kubadilibadili majina hivi?kinana humuwezi mkuu
 
nicas kwanini unahangaika kubadilibadili majina hivi?kinana humuwezi mkuu

Nibadirishe majina kwa faida gani? kwani mimi mkimbizi?
Kama unalijua jila langu lingine si liweke wazi mkuu.

Tatizo la watu kama wewe hampendi kuelezwa ukweli pale unapokosea au kuropoka bila kuangalia mbele, Kinana alisema sana wakati anatoka madarakani leo kala matapishi yake.

Kama wananchi inabidi tujue why? nini kimemrudisha kwenye siasa baada ya kuaga kwamba anaondoka, thus all.

Kama Kinana ni ndugu yako mwamabie aje akanushe yale aliyosema alipokuwa anaachia ngazi.
 
1. Mjumbe wa CCM miaka 25
2. Kuachana Kweka na siasa hakutakuwa na madhara kwa chama chake, kwani CCM ina hazina kubwa ya viongozi ambao wana sifa na wanaweza kuongoza chama hicho kuelekea Uchanguzi wa 2015
3. "Uongozi ni kupokezana vijiti, wako wanaCCM wazuri, walio na uwezo mkubwa na sifa za kutosha kuongoza"
4. Anajivunia kufanya kazi na marais wote kuanzia mwalimu hadi JK kwa uadilifu mkubwa na kuheshimiana.

Ushauri wake kwa Viongozi wapya
1. Viongozi wapya ambao wanatarajia kuchaguliwa ndani ya chama chake, iwapo wataona upungufu wake wausahihishe
2. Viongozi wasiwaze nani anafaa kuwa mgombea urasi bali washughulikie kero za wananchi

Nini atafanya baada ya kustaafu
1. Kuona kama anaweza kufundisha
2. Kusoma katika mojawapo ya vyuo vikuu vyetu.

Sasa, imekuwa vipi tena unarudi Jukwaani na kuanza kutuhubiri ulichoamua kukiacha september 2012?

Kweli siasa tamu sana.

Aku! akae pembeni mwa siasa aumie? Lundo la meno ya tembo aloficha na wenzie atauzaje? huoni tu baada ya kuchaguliwa meno yakafika Hong Kong? TAFAKARI
 
3 Reactions
Reply
Back
Top Bottom