Kinana unapuuzwa ama? ....,

Kigodoro

JF-Expert Member
Apr 25, 2014
1,660
1,679
Katibu mkuu wa ccm ulizunguka nchi nzima ukiimba kuwa mawaziri kadhaa wa rais wa awamu ya nne ni mizigo. Ninao wakumbuka ni Hawa Ghasia, Kawambwa, Christopher Chizza, prof. Maghembe, n.k. Rais Kikwete aliweka pamba masikioni hakusikiliza la muazini wala la mnadi swala. Kuna waliosema kuwa Kikwete aliendekeza uswahiba sana.
Sasa amekuja Magufuli amemteua prof. Maghembe. Na prof. Maghembe ametangaza vita na waliomuita mzigo. Bila shaka wizara yake una maslahi nayo sana. Hivyo anakugusa moja kwa moja. Na sina shaka prof. Maghembe alikulenga wewe. Maana bado tunakumbuka ulivyoikubali meli kuwa ni yako lkn ukaikana shehena ya meno ya tembo iliyobebwa na meli hiyo. Prof. Maghembe atatuthibitishia hilo.
Nahitimisha kwa kukuuliza mhe. Kinana hawa marais hawa wanakupuuza ama wanapuuza kauli zako? Kwanini? Utarudia kauli kama hizi?
 
ccm ni ileile na wanaccm ni wale wale. Wote sema Amina. Wastudanganye na hili changa la macho wakati tumewahi sana kubalehe.
 
Back
Top Bottom