MsemajiUkweli
JF-Expert Member
- Jul 5, 2012
- 13,171
- 23,991
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Omari Kinana ameyasema hayo wakati akiongea na vyombo vya habari Ikulu baaada ya kupokelewa ripoti ya uchunguzi wa Tume ya pili iliyoundwa na Rais wa Tanzania, John Magufuli kuchunguza sekta ya madini.
Kinana amesema kitendo anachokifanya Rais Magufuli cha kuita watu na vyombo vya habari Ikulu na kusoma mapendekezo ya Tume mbali mbali anazoziunda amekipongeza na kimemfurahisha sana kutokana na sababu kuu tatu.
Sababu ya kwanza, watanzania wanajua kuna nini kilichoko kwenye taarifa/ripoti.
Sababu ya pili, Rais mwenyewe anajiwajibisha kwa sababu taarifa inajulikana na kila mtu. Kwa hiyo basi, atasimamia kuhakikisha anatekeleza yote.
Sababu ya tatu, Rais ameunda tume katika dhamira ya kusahihisha makosa ya nyuma lakini amefanya hivyo katika msingi wa kufuata katiba, sheria na taratibu. Tume inaundwa, inaleta mapendekezo halafu anagawa majukumu katika vyombo mbali mbali vya serikali na bunge ili kuhakikisha serikali inasahihisha makosa iliyofanya ili watanzania waweze kupata maslahi wanayostahili.
Kinana amemaliza kwa kusema, hashangazwi na utendani wa kijasiri wa Rais Magufuli kwa sababu anamfahamu vizuri.
Kwa maelezo zaidi ya Kinana angalia video kuanzia dakika ya 1:25.

VIDEO.