Kinana na ziara za kuongeza ahadi juu ya ahadi

cj21125

JF-Expert Member
May 12, 2013
2,040
2,000
Kabla ya uchaguzi mkuu 2010 CCM waliwaahidi wananchi kutatua kero zao ikiwa ni pamoja na kutafuta soko lenye tija kwa korosho za Mtwara na Lindi. Leo hii miaka 5 inaisha bado hakuna kilichotekelezwa. Bado Katibu Mkuu wa CCM anafanya ziara mikoani ya kulaumu Mawaziri wa chama chake kuhusu huduma mbovu kwa wananchi. Mfano anamlaumu Mwakyembe kwenye majukwaa kwamba ni kwa nini bandari ya Mtwara haisafirishi mazao kutoka mikoa ya kusini. Mwakyembe ameteuliwa na mwenyekiti wa CCM na CCM hiyo hiyo ndio iliahidi maisha bora kwa Watanzania. Leo hakuna kilichofanyika na tena hali imezidi kuwa mbaya ikiwemo ukosefu wa dawa hospitalini. Hii ni ishara gani kwa katibu mkuu wa chama tawala kuendelea kutoa ahadi kwa wananchi kulaumu na kulalamikia mawaziri walioshindwa kuwaletea wananchi maendeleo? Kila mtu nchi hii analalamika kuanzia rais mpaka mlala hoi. Ni nani aliyeiloga Tanzania?
 

Tuko

JF-Expert Member
Jul 29, 2010
11,181
2,000
Hii dhana kuwa chama ni kizuri ila watendaji ndo wabaya ni ulaghai wa hali ya juu
Au tuseme siku nikikuta mahali uchaguzi unahusisha vyama tu na hakuna watu wanaogombea then nitaipigia ccm. Ila kwa kuwa siku zote viongozi wanaotokana na ccm ni wabovu then sitawapigia kura!
 

kinauche

JF-Expert Member
Oct 17, 2012
7,683
2,000
Niliwahi kuuliza lengo la ziara za Kinana lakini sikupata majibu. Ni nini maana ya katibu wa chama kinachotawala kuzunguka nchi nzima kuinanga serikali yake? Hivi huku siyo kumdhalilisha rais na waziri mkuu? Hivi unahitaji kuwa profesa kuligundua hilo? Anapouliza ni kwanini korosho haziondokei Mtwara ana uhakika serikali ya chama chake ilishatoa fedha? Hawa watu si wana party caucus? Kwa nini hawazungumzi haya mambo? Nadhani anafanya makusudi kumdhalilisha rais baada ya kukataa kuwawajibisha wale mawaziri aliowaita mizigo. Kweli Kinana na Nape ni majanga.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom