MwanaDiwani
JF-Expert Member
- Mar 22, 2013
- 5,536
- 2,264
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwahutubia wananchi wa Mbulu na kuwataka kutumia muda mwingi kwenye shughuli za kimaendeleo kwa kushirikiana na serikali kwa sababu serikali ndiyo yenye jukumu la kutekeleza kile ambacho wananchi wanakitaka katika maisha yao. Wasikubali malumbano ya kisiasa na wanasiasa wawe ndiyo chachu ya kukwamisha maendeleo kwa manufaa ya wanasiasa. Kuna wanasiasa wanafanya kila linalowezekana ili maendeleo yasiwepo kwa vile kutokuwepo maendeleo ndiyo mtaji wao katika kupata madaraka.
Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akihutubia wakazi wa Mbulu na kuwaambia vyama vingi vya upinzani vinakufa kwa sababu ya kuwa na sera zisizoaminika kwa Watanzania na ameshukuru kwa Watanzania wengi kuelewa hilo kiasi cha kurejea CCM. Kuna vyama vingine kwa sasa hata ukienda kwenye ofisi zao kuu, huwezi kukuta mafaili yenye jina la chama ambalo liko kwenye ofisi ya msajili wa vyama, kwa maana nyingine, vimepotea na kilichobaki ni maandishi kwenye kuta. Ulaghai wao unaelekea ukingoni.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akimsikiliza kwa makini Mkuu wa Wilaya ya Mbulu Anatory Choya akijibu maswali ya wananchi wa Yaeda Chini ambao wamekuwa wakivamiwa na kufukuzwa kwenye ardhi yao,Mkuu wa Wilaya alisema kwanza walishaweka mipango ya matumizi bora ya ardhi kuondoa migogoro ya wakulima na wafugaji, pili atafanya jitihada za dhati kuwakamata wale wote wanaofukuza na kunyanyasa wananchi wengine kwenye masuala ya ardhi.
Diwani wa Kata ya Eshkesh kutoka chama cha CUF Ndugu Naftal Kihandu akishukuru kwa Katibu Mkuu wa CCM, Ndugu Abdulrahman Kinana kwa kuwasikiliza wananchi wa kata yake na kufungua njia kwa kuchangia mabati na saruji kwa ajili ya ujenzi wa Zahanati.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiongea na watumishi na wanafunzi wa uuguzi wa Hospitali ya Hydom .Katibu Mkuu aliupongeza Uongozi pamoja na Watumishi wa hospitali hiyo kwa kazi nzuri wanayoifanya hasa katika kupunguza vifo vya mama na mtoto.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki ujenzi wa nyumba ya mwalimu wa shule ya sekondari Yaeda chini
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki ujenzi wakati wa ujenzi wa daraja la Qorong'aida linalounganisha Kilimapunda na Kidarafa na linategemewa kugharimu zaidi ya bilioni moja.