Kinana na timu yake wamaliza ziara wilayani Mbulu kwa kuhutubia umati wa watu

MwanaDiwani

JF-Expert Member
Mar 22, 2013
5,535
1,195

Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwahutubia wananchi wa Mbulu na kuwataka kutumia muda mwingi kwenye shughuli za kimaendeleo kwa kushirikiana na serikali kwa sababu serikali ndiyo yenye jukumu la kutekeleza kile ambacho wananchi wanakitaka katika maisha yao. Wasikubali malumbano ya kisiasa na wanasiasa wawe ndiyo chachu ya kukwamisha maendeleo kwa manufaa ya wanasiasa. Kuna wanasiasa wanafanya kila linalowezekana ili maendeleo yasiwepo kwa vile kutokuwepo maendeleo ndiyo mtaji wao katika kupata madaraka.

Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akihutubia wakazi wa Mbulu na kuwaambia vyama vingi vya upinzani vinakufa kwa sababu ya kuwa na sera zisizoaminika kwa Watanzania na ameshukuru kwa Watanzania wengi kuelewa hilo kiasi cha kurejea CCM. Kuna vyama vingine kwa sasa hata ukienda kwenye ofisi zao kuu, huwezi kukuta mafaili yenye jina la chama ambalo liko kwenye ofisi ya msajili wa vyama, kwa maana nyingine, vimepotea na kilichobaki ni maandishi kwenye kuta. Ulaghai wao unaelekea ukingoni.

Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akimsikiliza kwa makini Mkuu wa Wilaya ya Mbulu Anatory Choya akijibu maswali ya wananchi wa Yaeda Chini ambao wamekuwa wakivamiwa na kufukuzwa kwenye ardhi yao,Mkuu wa Wilaya alisema kwanza walishaweka mipango ya matumizi bora ya ardhi kuondoa migogoro ya wakulima na wafugaji, pili atafanya jitihada za dhati kuwakamata wale wote wanaofukuza na kunyanyasa wananchi wengine kwenye masuala ya ardhi.

Diwani wa Kata ya Eshkesh kutoka chama cha CUF Ndugu Naftal Kihandu akishukuru kwa Katibu Mkuu wa CCM, Ndugu Abdulrahman Kinana kwa kuwasikiliza wananchi wa kata yake na kufungua njia kwa kuchangia mabati na saruji kwa ajili ya ujenzi wa Zahanati.

Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiongea na watumishi na wanafunzi wa uuguzi wa Hospitali ya Hydom .Katibu Mkuu aliupongeza Uongozi pamoja na Watumishi wa hospitali hiyo kwa kazi nzuri wanayoifanya hasa katika kupunguza vifo vya mama na mtoto.

Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki ujenzi wa nyumba ya mwalimu wa shule ya sekondari Yaeda chini

Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki ujenzi wakati wa ujenzi wa daraja la Qorong'aida linalounganisha Kilimapunda na Kidarafa na linategemewa kugharimu zaidi ya bilioni moja.
 
MwanaDiwani

JF-Expert Member
Mar 22, 2013
5,535
1,195
SERIKALI imesema itachukua hatua kali kwa baadhi ya Watanzania, ambao watabainika kutoa siri za nchi kwa ajili ya manufaa binafsi.
Kauli hiyo ilitolewa bungeni jana na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Benard Membe, alipokuwa akijibu hotuba ya Kambi ya Upinzini iliyosomwa na Mbunge Ezekiel Wenje (Nyamagana-CHADEMA).

Katika hotuba yake, Wenje ambaye ni Waziri Kivuli wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, alidai kuwa Membe, anachochea vita kati ya Rwanda na Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo (DRC).

Membe alisema ni aibu kwa mbunge kusimama ndani ya bunge kutetea maslahi ya Rwanda na kuonya kuwa hatua hiyo ni hatari kwa mustakabali wa nchi.
Alisema ameshangazwa na kauli ya Wenje kwamba Serikali ya Tanzania inaibeba DRC katika vita kati ya nchi hiyo na Rwanda.

Akionekana kukerwa na kauli ya Wenje, Membe alisema mbunge huyo hana nia njema na mustakabali wa wananchi wa Tanzania na lengo lake ni kutaka kuchochea mgogoro kati ya Tanzania na Rwanda.

"Ni aibu kwa Mbunge Wenje kusimama bungeni macho yamemtoka, akiitetea Rwanda. Mtu wa aina hii ni msaliti mkubwa na hafai kuwa kiongozi.

"Kwa nini Wenje anatetea nchi jirani? Mtu makini ni lazima apiganie nchi yake hata kama serikali yake inafanya mabaya au mazuri. Mtu wa aina hii ni rahisi kutumika au kutoa siri za nchi," alisema Membe.
Huu ni mwendelezo wa kile ambacho kimeridhiwa kwa manufaa ya kisiasa za kibinafsi ambazo hazina maslahi ya taifa endelevu.

Kumbuka kuna kipindi gari la kazi za KUB ambalo anatumia Mh. Mbowe lilipata matatizo Kenya na katika safari hiyo, Mh. Mbowe alikuwa ameambatana na guess who?. Mh. Wenje.

Gari waliamua kuiacha Mombasa wakaamua kumalizia safari zao kwa usafiri mwingine. guess walikuwa wanaenda kukutana na nani? kwa faida ya nani?.

Haya mambo hayatokei kwa bahati mbaya. Hata Rais Paul Kagame alishawahi kutumia reference ya msimamo wa CHADEMA katika hotuba yake.

Rais Kagame said last year, "he will wait for the right moment and hit Kikwete hard." This is the moment!

We knew it was coming!

Rais Kikwete husema, akili za kuambiwa changanya na zako kwa maana kwamba, tumesikia Mh. Wenje alichosema, na sasa tunafahamu sababu zake.
 
Chinga One

JF-Expert Member
May 7, 2013
10,545
2,000
CCM ni chama kinacho undwa na majangiri,wauza unga,waiba madini,na Waropokaji.
 
Haji Salum

JF-Expert Member
Nov 27, 2013
1,022
0

Rubbish!!
 
habariyamujini

JF-Expert Member
May 16, 2013
3,094
1,225
Km kinana ameenda hadi yaeda chini basi ccm ni expired

Sikakuelewa mkuu what do you mean when your say expired? Inamaana Yaeda chini hakuna watu?

CCM ni moto wa kuotea mbali nyie UKAWA mpo busy na katiba wakati Kinana yu busy na matatizo ya wananchi na kukagua uhai wa chama ikiwemo kupanga mikakati ya serikali za mitaa!

CCM nchi nzima wanajiandaa na uchaguzi wa serikali za mitaa imebaki miezi 4 tu kuanzia sasa na kwa hakika tutashinda kwa kishindo!
 
MwanaDiwani

JF-Expert Member
Mar 22, 2013
5,535
1,195
CCM ni chama kinacho undwa na majangiri,wauza unga,waiba madini,na Waropokaji.
Ndugu, Kama ni kweli CCM umeundwa na watu wa aina hii unayoitaja ambao kwa kupitia kwao chama kimeendelea kuaminiwa na kupewa uongozi ndani ya multiparty politics tokea 1992, basi wale ambao wako kwenye vyama vingine watakuwa ndiyo hovyo kabisa (inutile) kwa sababu wameendelea kukataliwa na wananchi wengi kuongoza taifa tokea 1995.
 
theki

JF-Expert Member
Nov 1, 2013
2,724
1,195
Hebu ngoja kwanza ni kwamba kinana kaona waliotumwa na JK imekuwa mizigo au ?Kuna picha naona sare za vitenge hiyo kwaya ya wapi tena?
 
Chinga One

JF-Expert Member
May 7, 2013
10,545
2,000
Ndugu, Kama ni kweli CCM umeundwa na watu wa aina hii unayoitaja ambao kwa kupitia kwao chama kimeendelea kuaminiwa na kupewa uongozi ndani ya multiparty politics tokea 1992, basi wale ambao wako kwenye vyama vingine watakuwa ndiyo hovyo kabisa (inutile) kwa sababu wameendelea kukataliwa na wananchi wengi kuongoza taifa tokea 1995.

Hakuna anae waamini zaidi ya familia zenu tu,mnaingia madarakani kwa kuiba kura mkisaidiwa na TISS na policcm....tunataka tume huru.
 
MwanaDiwani

JF-Expert Member
Mar 22, 2013
5,535
1,195
Hakuna anae waamini zaidi ya familia zenu tu,mnaingia madarakani kwa kuiba kura mkisaidiwa na TISS na policcm....tunataka tume huru.
Ndugu, Hizi kelele tumeanza kuzisikia tokea 1995 kwa maana nyingine, unachokisema ni marudio yaleyale, yanayosemwa na walewale kwa manufaa yale yale.

Hii ni sawa na kwenda vitani zaidi ya mara tano na kila ukishindwa unaanza kusema, isingekuwa zile silaha, basi tungeshinda.e bo, mara tano na hujatafuta njia nyingine ya kupambana na hizo silaha. Wewe ndiyo utakuwa una matatizo!
 
JGG

JF-Expert Member
Dec 20, 2012
324
225
Sikakuelewa mkuu what do you mean when your say expired? Inamaana Yaeda chini hakuna watu?

CCM ni moto wa kuotea mbali nyie UKAWA mpo busy na katiba wakati Kinana yu busy na matatizo ya wananchi na kukagua uhai wa chama ikiwemo kupanga mikakati ya serikali za mitaa!

CCM nchi nzima wanajiandaa na uchaguzi wa serikali za mitaa imebaki miezi 4 tu kuanzia sasa na kwa hakika tutashinda kwa kishindo!

Uko sahihi kabisa, endeleeni kuwekeza katika ujinga na umaskini wa watz ili mbaki ikulu kwa mda ila jua iko siku sisi wachache tunaoelewa kwamba nyinyi ni genge la watu wachache mnaofuja raslimali za nchi at the expense of ignorance tutachukua nchi kwa njia yoyote n trust me you will account for everything if at all you will be alive
 
Honolulu

JF-Expert Member
Jan 20, 2012
5,649
1,225
this is fun, nadhani uelewi hata maana ya hii picture naona unatembea nayo tangu juzi
Mkuu hiyo, this is fun ndiyo utumbo wa mnyama gani? Au ulitaka kusema this is funny? Na hiyo uelewi ndiyo mzoga wa mdudu gani? Au ulitaka kusema: huelewi? Na wewe naye ni great thinker hapa Jukwaani?
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom