Kinana na timu yake waingia kwenye Jimbo la Tundu Lissu na kuhutubia umati wa watu

IMG_2918.JPG

Kinana akilakiwa na ngoma ya asili alipowasili kwenye mkutano wa hadhara katika Kijiji cha Mukiungu, katika Jimbo la Singida Mashariki la Tundu Lissu wa Chadema.
05.JPG

Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akihutubia katika mkutano wa hadhara ulofanyika katika Kijiji cha Makiungu, wilayani Ikingu, Jimbo la Singida Mashariki la Mbunge Tundu Lissu wa Chadema. Kinana alimponda Mbunge wa Jimbo la Singida Mashariki kwa kitendo chake cha kuwakataza wananchi kuchangia fedha za miradi maendeleo na kusababisha jimbo hilo kudorora kimaendeleo tofauti ma majimbo mengine nchini. Alisema badala ya kuwasaidia wananchi badala yake anaendekeza masuala UKAWA
IMG_2924.JPG

Nape akihutubia katika mkutano wa hadhara katika Kijiji cha Mukiungu wilayani Ikungi.
IMG_2960.JPG

Kinana akihutubia katika mkutano wa hadhara mjini Ikungi, Jimbo la Singida Mashariki na kuwataka wananchi wamhoji kama kuna miradi aliyoitekeleza katika ahadi zake wakati wa awamu yake hii ya ubunge wa jimbo hilo.
IMG_2947.JPG

Nape akihutubia katika mkutano wa hadhara mjini Ikungi.
IMG_2976.JPG

Wananchi wakila kiapo ili kuwa wanachama wapya wa CCM katika mkutano hou.
IMG_2842.JPG

Mwenyekiti wa CCM, Mkoa, Msindai akimpatia tofari Kinana walipokuwa wakisaidia ujenzi wa Shule ya Msingi Unyaghumpi, katika Jimbo la Singida Mashariki la Mbunge Tundu Lissu. Mbunge huyo aliwakataza wananchi kuchangia fedha za kujengea vyumba vya madarasa katika shule hiyo. Lakini baada ya kuona watoto wao wanateseka kwa kukosa elimu wananchi wameamua kupuuza katazo hilo na kuanza kujitolea kujenga vyumba hivyo vya madarasa.
01.JPG

02.JPG

Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana na Katibu wa Umoja wa Wanawake wa CCM (UWT) Mkoa wa Singida, Sija Lukwale wakisaidia kuvuna mtama na uwele kwenye shamba bibi mjane asiye na mtoto, Mayasa Mkhandi katika Kata ya Unyaghumpi, Jimbo la Singida Mashariki, mkoani Singida.
IMG_2797.JPG

Kinana akikagua shamba la maharage akiwa na Mkurugenzi wa Kampuni ya Singida Agriculture, Ally Mohamed katika Kijiji cha Mkiwa, wilayani Ikungi. maharage hayo huuzwa nje ya nchi.
IMG_2787.JPG

Wafanyakazi wa shamba hilo, wakichuma maharage katika shamba hilo.
IMG_2808.JPG

Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nanuye akitumia treka kulima shamba la kampuni hiyo
IMG_2829.JPG

Nape akisaidia kuchambua maharage ili kuyaandaa kusafirishwa.
IMG_2830.JPG

Kinana akiangalia makasha yenye maharage yaliyohifadhiwa kwenye kontena lenye jokofu linalotumika kusafirishia nje
IMG_2852.JPG

IMG_2857.JPG

Picha juu ni Jengo la Zahanati ya Kimbwi, Kata ya Mungaa, ambayo ilikamilika wakati Kata hiyo ikiongozwa na Diwani wa CCM, lakini hadi sasa haitumiki baada ya Diwani wa sasa wa Chedema na Mbunge wa Jimbo la Singida Mashariki, Tundu Lissu kuwakataza wananchi kuchangia fedha za ujenzi wa nyumba ya madaktari. Kinana (kulia) na Nape pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Ikungi, Msambya wakiondoka baada ya kukagua zahanati hiyo isiyotumika
IMG_2860.JPG

Wananchi wakijitolea kukwatua nje ya vyumba vya madarasa ya Shule ya Msingi Unyaghumpi ambayo ujenzi wake ulikwamishwa na Tundu Lissu.
IMG_2866.JPG

IMG_2865.JPG

Wananchi wakiwa wamejipanga kusomba matori ya kujengea vyumba vya madarasa vya shule ya Unyaghumpi, wakati wa ziara ya Kinana wailayani Ikungi.

Hii ni gumu kuielewa Kinana na Nape wanakagua miradi mbalimbali jimbo ni kwa Lissu lakini CCM wanasema kuwa Lissu amewazuia watu kuchangia maendeleo na wanasema kuwa miradi hiyo ilijengwa kipindi kile ambacho CCM ilipokuwa inaongoza jimbo hilo.Ina maana kuwa CCM walisubiri waondolewe madarakani ndiyo waanze kuelezea maendeleo waliyoyafanya kwenye jimbo hilo?.
 
Unavyosema Singida
Mashariki ipo nyuma kimaendeleo kwa kuwa eti lipo chini ya Lissu,vp nyie
miaka 40 iliyopita mbona hamkuhamasisha maendeleo.

MBONA SINGIDA VIJIJINI,IRAMBA NA HANANG NA KWINGINE AMBAYO WAPO WABUNGE
WA CCM PIA HALI NI MBAYA SANA?

YAHITAJI UWE PUNGUANI KUWAELEWA CCM.

siasa bwana, hayo madarasa siyanajengwa hatakama anajenga kinana lakini yako jimboni kwake, na huo mwiko naona anatembea nao mfukoni, ila kujipendekeza kubaya yaani kinana fundi mwashi msindai kibarua wake ona anavyojikunja kubeba tofali, baba msindai mwenzio mjeda ohoo!
 
Hivi jukumu la kujenga maabara, shule na zahanati ni la nani. Kama watu wanalipa kodi serekalini halafu na huduma za kijamii wajifanyie wenyewe hapo inabidi serekali iaache uhuni wa kuwatoza watu kodi. Maana kodi ndio zinarudi kipitia huduma za kijamii.

Jukumu la kujenga maabara na zahanati ni la serekali lakini kwa mjibu wa Kinana ni kwamba Lissu amewazuia wananchi kuchangia maendeleo katika jimbo lake.Kwa mjibu wa Kinana huyohoyo Lissu ndiye aliyeizuia hata serekali kutekeleza majukumu yake katitika jimbo la Lissu.
 
Feedback nimelipenda jibu lako. Umasikini siyo uzalendo. Eti oooh! Kinana ala kwa mama ntilie, huyo mama kama maisha yangekuwa bora angekuwa na hoteli yake!!! Nani duniani anapenda kula vyakula kwenye mavumbi. Umasikini waukuze wenyewe aje kinafiki kututia moyo kwa chakula kupikiwa mazingira mabovu ni bora. HUYO KINANA AMEKUWA WAZIRI MIAKA MINGI MBONA HAKULAGA KWA MAMANTILIE. Kweli unafiki hauna kwao!!! Umasikini ni aibu siyo sifa na hauwezi kuwa uzalendo kamwe. Kujidai kupongeza mtu kwa kujipenyeza kwenye viashiria vya umasikini wa watanzani kutafuta huruma ya wananchi ni ulimbukeni uliopindukia.

Kuwa mwelewa ndugu, kila mama ntilie au mama lishe akiwa na hotel , hili linawezekana?, hebu fikiria kuna akina mama lishe wangapi Tanzania? Unajua sifa za "hotel"?, yawezekana kwa uelewa wako huwezi kutofautisha kati ya hotel na mghahawa yaani cafeteria. Kama hilo ni sahihi basi wewe unaweza kuwa na akili sawa na UKAWA.
 
Qoute ya zamani kidogo ya yaliyoongelewa JFlakini
Re: Abdul Rahman Kinana: Who is he?
A quote from Julius Nyerere " Kila nilipokuwa nikitaka kung'atuka, walikuwa wakiniambia Mwalimu andelea tu, hii nchi bado ni changa na umeitoa mbali, nchi haitaendelea bila wewe. Nami niliendelea, hadi pale nilipokuja kugundua kumbe nchi changa wanayoiongelea ni FAMILIA ZAO, na hazitaendelea bila mimi kuwepo madarakani, maana walikuwa hawana uhakika kama RAIS ajae atawaacha katika nafasi walizokuwa nazo" mwisho wa nukuu. Haya ndio maneno wasemayo viongozi wetu wa sasa, wanasema BILA CCM nchi haitaendelea, lakini ukweli ni kuwa BILA CCM ufisadi wao hautaendelea, maana hawan uhakika kama CHAMA kingine kikichukua nchi watabaki salama!


Nidhambi kubwa kupita kiasi kumnukuu kiongozi mahili kama nyerere na kuongezea ya kwako yaliyojaa uongo uliopitiliza! mfano eti nyerere alisema familia za viongozi zitashindwa kuendelea. huo ni uongo na uzandiki wa hali ya juu. Kumbuka tume ya kuangalia Watanzania wanataka vyama vingi au kimoja, 80% walitaka CCM iendelee, 20% ndiyo waliotaka vingi viwepo. Hivyo 80% bado inaendelea kufanya kazi, wazo la CCM kuitoa madarakani bado liko mbali sana kwavile utafiti uliofanywa na shirika la FIDHI baada ya chaguzi za Katta 27 na cdm kupata 3 pia Kalenga cdm kuambulia kura 5,000 tu dhidi ya 22,000 za CCM achilia mbali kufuru ya Chalinze. Majibu ya utafiti huo na matokeo hayo hivi sasa asilimia ya Watanzania wanaoitaka CCM iendelee kuongoza imefikia 90. Hivyo wewe umo kwenye asilimia 10 wanaodhani CCM imechukiwa. POLE SANA.
 
Back
Top Bottom