Kinana na timu yake waingia kwenye Jimbo la Tundu Lissu na kuhutubia umati wa watu

Kuwa mzalendo hakukuzuii kula bata, uzalendo sio lazima uvae kandambili za kisanii kama anavyofanya Kinana.

Feedback nimelipenda jibu lako. Umasikini siyo uzalendo. Eti oooh! Kinana ala kwa mama ntilie, huyo mama kama maisha yangekuwa bora angekuwa na hoteli yake!!! Nani duniani anapenda kula vyakula kwenye mavumbi. Umasikini waukuze wenyewe aje kinafiki kututia moyo kwa chakula kupikiwa mazingira mabovu ni bora. HUYO KINANA AMEKUWA WAZIRI MIAKA MINGI MBONA HAKULAGA KWA MAMANTILIE. Kweli unafiki hauna kwao!!! Umasikini ni aibu siyo sifa na hauwezi kuwa uzalendo kamwe. Kujidai kupongeza mtu kwa kujipenyeza kwenye viashiria vya umasikini wa watanzani kutafuta huruma ya wananchi ni ulimbukeni uliopindukia.
 
Ndugu, Mlidhani kazi za Mzee Kinana ni nguvu ya soda au ya ndege wa angani kama wanavyofanya baadhi ya viongozi wa upinzani wanaorusha helikopta ikiwa na chama kwenye mafaili waliyobeba.

Wakishuka kwenye helikopta wanashuka na chama chote na wakipanda kwenye helikopta kuondoka, wanaondoka na chama chote.

Tulifahamu mtashangaa kwa sababu mlizoea siasa za mazoea ambazo hazina ajenda za kitaifa ambazo ni endelevu. Katika mshangao wenu mmeanza kutafuta mchawi kama walivyo viongozi wa vyama vya upinzani wanakimbia vivuli vyao na kuilalamikia CCM pale wanaposhindwa katika harakati zao za siasa za zimamoto.

Tunasikia kwa sasa kile kikundi kinachojiita UKAWA kimebadilisha ajenda ya mizunguko yao waliyodai ni Katiba na kwa sasa Mzee Kinana ndiyo ajenda.

Soma hapa wewe: https://www.jamiiforums.com/jukwaa-la-siasa/661405-ccm-yameguka.html?highlight=Kinana+Nape
 
Ndugu, Wewe unaamini kazi ya hirizi?. Kama huamini, kwa nini unaweka mfano wa hirizi ujenge mantiki ya hoja?.

Mimi nimeweka hotuba ninayoifahamu, kama unadhani kuna hotuba nyingine, unaweza kuweka kwa sababu Jukwaa nila kila mwanaJF

Qoute ya zamani kidogo ya yaliyoongelewa JFlakini
Re: Abdul Rahman Kinana: Who is he?
A quote from Julius Nyerere " Kila nilipokuwa nikitaka kung'atuka, walikuwa wakiniambia Mwalimu andelea tu, hii nchi bado ni changa na umeitoa mbali, nchi haitaendelea bila wewe. Nami niliendelea, hadi pale nilipokuja kugundua kumbe nchi changa wanayoiongelea ni FAMILIA ZAO, na hazitaendelea bila mimi kuwepo madarakani, maana walikuwa hawana uhakika kama RAIS ajae atawaacha katika nafasi walizokuwa nazo" mwisho wa nukuu. Haya ndio maneno wasemayo viongozi wetu wa sasa, wanasema BILA CCM nchi haitaendelea, lakini ukweli ni kuwa BILA CCM ufisadi wao hautaendelea, maana hawan uhakika kama CHAMA kingine kikichukua nchi watabaki salama!

Tunafahamu kwa sasa mko kama fisi anayesubili mkono udondoke. Kila siku mnaota ndoto za mchana.

CCM kwa sasa iko imara zaidi ya ilivyowahi kutokea baada ya uchaguzi Mkuu. Tunafahamu kwa sasa mnamuomba hata shetani ili CCM iwe kwenye mgogoro. Haiwezi kutokea kwa sababu CCM siyo chama cha kwenye makabrasha ya viongozi wakuu.
CHADEMA’s earlier vibrancy was a case of taking advantage of CCM’s weaknesses and disunity to spread it wings, Mr Kinana added. “We have to be honest. There was a time we spent most of our time and resources dealing with leadership problems in our party instead of reaching out to wananchi, hear their problems and find ways to solve them. Our unity was affected. We stopped addressing issues touching the people’s lives such as employment, land and availability of essential social services. We devoted our time to resolving intra-party conflicts. That is how Chadema came in.”

Mr Kinana says the main secret of CCM’s survival for over 50 years is that it has a genuine internal mechanism to assess itself. “What has been helping us is a mechanism to assess ourselves from time to time, which we have cherished for decades,” says Mr Kinana. “If you don’t have a genuine self assessment mechanism, you are definitely going to collapse like CHADEMA today.”

Mr Kinana added: “It (CHADEMA) is an event-oriented party. They are always jumping from one agenda to another or reacting to sporadic events to keep their party afloat. They have no national agenda and that picture is becoming clearer to Tanzanians today more than ever before. Today their agenda is the new constitution. Now everything is around Katiba. Their plans are not long-term, objective and sustainable. Whatever they take on is short term and sporadic.” Blaming CCM and its government for the party’s troubles, the CCM secretary-general said, was escapism and an attempt to hide their weaknesses in managing internal politics.

Chadema changes tack amid CCM onslaught - National - thecitizen.co.tz
 
Kwa hakika Lissu ni miongoni mwa wabunge ambao hata YESU akirudi hawezi kupita tena. Amekwamisha miradi mingi ya maendeleo na wananchi wamekuwa wakihangaika Usiku kucha!

Lissu alihamasisha kufukia visima vitano vilivyojengwa na wafadhili na kuwaambia atawajengea yeye hadi Leo na wananchi wake wakitaabika yeye akiendelea kunywa maji ya chupa ya Kilimanjaro!

Wilaya ya Ikungi ni ya mwisho kwa kila kitu Mkoa wa Singida, wapo nyuma kwa ujenzi wa zahanati na vituko vya afya, ujenzi wa vyumba vya madarasa, nyumba za walimu, maabara katika shule za sekondary, maji, umeme nk!

Anasema wananchi walale hata Uniform za watoto wao serikali itawapatia bure wanafunzi na chakula majumbani Kwao!

Tusubiri 2015....

Sikuwa najua mpaka leo katika tarifa ya habari ITV kumbe mzee wa tembo a.k.a Tusker Lager Kinana na timu yake ya CCM kwamba wako Singida eti kule kwa Tundu Lissu.It was very funny kwamba kila aliyekuwa anasimama (viongozi wote wa CCM; Kinana,Nnape na wale wa palepale Singida kama Mwenyekiti wa CCM (M) yule mwenye tumbo kubwa mpaka anashindwa kutembea sijui ni shibe ya rushwa au utapia mlo anaitwa Mgana Msindai) mdomoni ilikuwa Tundu Lissu,Tundu Lissu eti anazuia wananchi wake kushiriki shughuli za maendeleo.........very cheap propaganda!!

Ukistaajabu ya Mussa utayaona ya Firauni, hata wale wana CCM waliopangwa katika Camera za Tv, nao wanasema eti Mbunge wao anawazuia kuchangia na kushiriki shughuli za maendeleo halafu wakati huohuo unawaona wanabeba matofali na maguo yao ya kijani "alama ya ufisadi wa CCM" na eti sasa wamefunguka na wanashiriki na kuchangia shughuli za maendeleo!!...Mimi inanishangaza na kujiuliza sana kwamba hivi huyu Tundu Lissu aliwakusanya wanyaturu wote wa jimbo lake na kuwafunga mikono na akili hata wana CCM wenyewe ili wasichangie/wasifanye shughuli za maendeleo na kwamba wamemwona Kinana na Nape mikono yao ikafunguka!???....This is very,very,very funny na kwa vyovyote vile ni unafiki na ujinga wa hali ya juu wa wana CCM uliovuka mipaka!!

Na kwa mtindo huu wa propaganda za Nnape na wenzake; kama CCM wataweza kuchukua jimbo hilo toka CHADEMA/UKAWA na toka kwa Tundu Lissu mwaka 2015, basi mimi mwaka huohuo nitakuwa mwana siasa halisi na tena mwana CCM!!
 
CCM wanachotaka kuwafundisha watu hapa ni kwamba wananchi wa jimbo la Lissu wanamtii mbunge wao hata katika mambo ya kipumbavu ambayo hayawasadii.Kwa maana nyingine ni kwamba CCM wasahau kulipata jimbo la Lissu kwa sababu Lissu atawaagiza wapiga kura wa jimbo lake wasiipigie CCM kura na kwakuwa maagizo ya Lissu ndiyo yanayofuatwa na wapiga kura wa jimbo la Lissu basi CCM hawataambulia hata kura moja.
 
Unajua nini? Hawa viongozi na wana CCM wao ni vituko sana!!...Logic iliyoko katika hoja zao ni kuwa Tundu Lissu ana ushawishi na nguvu sana kuliko kawaida!!

Kwa sababu haingii akilini eti mtu mmoja tu awazuie wananchi wote wa eneo flani msishiriki au kuchangia shughuli zenu za kimaendeleo na ninyi mkakubali bila kuwa na sababu na leo watu na akili zao timamu wanapaza sauti zao kupitia tv kwamaba mbunge wao anawazuia, tena wanaozuiwa wana CCM wenyewe!!... Wana akili timamu kweli hawa?

Tunauliza hivi kwa sababu kama Tundu Lissu ana nguvu kubwa kiasi hiki basi, ni wazi hawana ubavu wa kumshinda katika uchaguzi wowote ulio huru na wa haki!!..

Kichekesho kingine cha hawa jamaa ni hiki; Kwamba kama kikwazo cha maendeleo yao ni Tundu Lissu, kwa nini wasinge kuwa wanamvizia kama ilivyo sasa hivi hayupo jimboni,yuko Dodoma katika kikao cha Bunge la Bajeti, wanatumia kutokuwepo kwake kujenga hata madarasa na zahahati,na malambo na nyumba nzuri zile sa kisasa kwa fujo ili mara arudipo jimboni kwake na kukuta wananchi wake (hasa wana CCM wanaoishi jimboni kwake) wamefanya hayo,awacharaze viboko kwa sababu wanakuwa wamefanya mambo ambayo mbunge kawakataza!!..

Kama ndivyo sivyo,hakuna namna ingine yoyote unavyoeleza hiki wanachokifanya CCM na mawakala wao ktika mitandao zaidi ya propaganda za kipuuzi na za kijinga ambazo kwa namna yoyote haziwezi ku - work katika zama hizi za kizazi cha shule za kata za Lowassa!!
 
CCM wanachotaka kuwafundisha watu hapa ni kwamba wananchi wa jimbo la Lissu wanamtii mbunge wao hata katika mambo ya kipumbavu ambayo hayawasadii.Kwa maana nyingine ni kwamba CCM wasahau kulipata jimbo la Lissu kwa sababu Lissu atawaagiza wapiga kura wa jimbo lake wasiipigie CCM kura na kwakuwa maagizo ya Lissu ndiyo yanayofuatwa na wapiga kura wa jimbo la Lissu basi CCM hawataambulia hata kura moja.

Hivi jukumu la kujenga maabara, shule na zahanati ni la nani. Kama watu wanalipa kodi serekalini halafu na huduma za kijamii wajifanyie wenyewe hapo inabidi serekali iaache uhuni wa kuwatoza watu kodi. Maana kodi ndio zinarudi kipitia huduma za kijamii.
 
Kinana mpaka sasa amepoteza dira hajui aelekee wapi.Kila kitu kwake hakifai.Serekali kwake anaiona haifai ndiyo maana ana zunguka nchi nzima kuwatangaza viongozi wenzake kuwa hawafai kwa kuwaita kuwa ni mizigo na ni wazembe.Huku akisahau kuwa hao anaowaita mizigo na wazembe wameteuliwa na mwenyekiti wake kwa maana hiyo kama wateuliwa ni mizigo basi aliyewateua ni mzigo ambao hata kubeba hauweziukabebeka.Pia ana shindwa kuelewa kuwa serekali anayoisema kuwa viongozi wake ni mizigo ni serekali ambayoimetokana na CCM na huwezi ukaitenganisha serekali ya CCM na CCM yenyewe.Wapinzani nao ana waona kuwa hawafai.Serekali ya CCM inaongozwa na viongozi mizigo CCM ndiyo inayotoa viongozi hao mizigo na wazembe kwa hiyo ana manisha kuwa CCM yenyewe ndio mzigo zaidi ya mizigo yote ndiyo maana inazalisha viongozi mizigo.Kwa wapinzani nako anaona viongozi wake hafai kama kwake hakufai na kwa wapinzani hakufai huyu Kinana ana taka kuleta serekali inayoongozwa na chama gani?au ana taka serekali inayoongozwa na serekali inayotokana na chama pamoja na viongozi wake wanaotoka Somalia ndiyo aridhike?.
 
nape msanii,nlidhani gitaa tu hadi trekta???? Huku magufuli pale nape
 
Back
Top Bottom