Kinana na timu yake waingia kwenye Jimbo la Tundu Lissu na kuhutubia umati wa watu

MwanaDiwani

JF-Expert Member
Mar 22, 2013
5,535
1,195

Kinana akilakiwa na ngoma ya asili alipowasili kwenye mkutano wa hadhara katika Kijiji cha Mukiungu, katika Jimbo la Singida Mashariki la Tundu Lissu wa Chadema.

Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akihutubia katika mkutano wa hadhara ulofanyika katika Kijiji cha Makiungu, wilayani Ikingu, Jimbo la Singida Mashariki la Mbunge Tundu Lissu wa Chadema. Kinana alimponda Mbunge wa Jimbo la Singida Mashariki kwa kitendo chake cha kuwakataza wananchi kuchangia fedha za miradi maendeleo na kusababisha jimbo hilo kudorora kimaendeleo tofauti ma majimbo mengine nchini. Alisema badala ya kuwasaidia wananchi badala yake anaendekeza masuala UKAWA

Nape akihutubia katika mkutano wa hadhara katika Kijiji cha Mukiungu wilayani Ikungi.

Kinana akihutubia katika mkutano wa hadhara mjini Ikungi, Jimbo la Singida Mashariki na kuwataka wananchi wamhoji kama kuna miradi aliyoitekeleza katika ahadi zake wakati wa awamu yake hii ya ubunge wa jimbo hilo.

Nape akihutubia katika mkutano wa hadhara mjini Ikungi.

Wananchi wakila kiapo ili kuwa wanachama wapya wa CCM katika mkutano hou.

Mwenyekiti wa CCM, Mkoa, Msindai akimpatia tofari Kinana walipokuwa wakisaidia ujenzi wa Shule ya Msingi Unyaghumpi, katika Jimbo la Singida Mashariki la Mbunge Tundu Lissu. Mbunge huyo aliwakataza wananchi kuchangia fedha za kujengea vyumba vya madarasa katika shule hiyo. Lakini baada ya kuona watoto wao wanateseka kwa kukosa elimu wananchi wameamua kupuuza katazo hilo na kuanza kujitolea kujenga vyumba hivyo vya madarasa.

Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana na Katibu wa Umoja wa Wanawake wa CCM (UWT) Mkoa wa Singida, Sija Lukwale wakisaidia kuvuna mtama na uwele kwenye shamba bibi mjane asiye na mtoto, Mayasa Mkhandi katika Kata ya Unyaghumpi, Jimbo la Singida Mashariki, mkoani Singida.

Kinana akikagua shamba la maharage akiwa na Mkurugenzi wa Kampuni ya Singida Agriculture, Ally Mohamed katika Kijiji cha Mkiwa, wilayani Ikungi. maharage hayo huuzwa nje ya nchi.

Wafanyakazi wa shamba hilo, wakichuma maharage katika shamba hilo.

Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nanuye akitumia treka kulima shamba la kampuni hiyo

Nape akisaidia kuchambua maharage ili kuyaandaa kusafirishwa.

Kinana akiangalia makasha yenye maharage yaliyohifadhiwa kwenye kontena lenye jokofu linalotumika kusafirishia nje

Picha juu ni Jengo la Zahanati ya Kimbwi, Kata ya Mungaa, ambayo ilikamilika wakati Kata hiyo ikiongozwa na Diwani wa CCM, lakini hadi sasa haitumiki baada ya Diwani wa sasa wa Chedema na Mbunge wa Jimbo la Singida Mashariki, Tundu Lissu kuwakataza wananchi kuchangia fedha za ujenzi wa nyumba ya madaktari. Kinana (kulia) na Nape pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Ikungi, Msambya wakiondoka baada ya kukagua zahanati hiyo isiyotumika

Wananchi wakijitolea kukwatua nje ya vyumba vya madarasa ya Shule ya Msingi Unyaghumpi ambayo ujenzi wake ulikwamishwa na Tundu Lissu.

Wananchi wakiwa wamejipanga kusomba matori ya kujengea vyumba vya madarasa vya shule ya Unyaghumpi, wakati wa ziara ya Kinana wailayani Ikungi.
 
MwanaDiwani

JF-Expert Member
Mar 22, 2013
5,535
1,195
Ifuatayo ni sehemu ya hotuba ya Mwalimu Nyerere kwa waandishi wa habari mwaka 1995 hasa kuhusu mustakabali wa muungano:

"Watu wamezungumza Uzanzibari, baadhi ni viongozi wetu wanajivunia Uzanzibari. Nadhani wengine wanafikiria hata kujitenga, sio wengi, lakini wapo.

Kujitenga maana yake ni kuvunja nchi, kusiwe na nchi moja bali mbili. Hili ni jambo linazungumzwa.

Tunataka viongozi, kiongozi wanaoelewa hilo. Kuzungumza Uzanzibari si jambo la fahari. Hatima yake utavunja nchi. Mtu mwenye akili, Mzanzibari ana akili hawezi akautuza Uzanzibari wa kujiita sisi Wazanzibari na wao Watanganyika.

Na adhani ile ina usalama ndani yake. Kufanya hivyo, hatima yake Zanzibar itajitenga.

Zanzibar ikijitenga, kutokana na ulevi tu…sisi Wazanzibari wao Watanganyika…sisi si wamoja. Ulevi tu…ulevi hasa ulevi wa madaraka.

Ikitokea hivyo, sisi Wazanzibari wao Watangayika. Wakumbuke kwamba muungano ndio unaowafanya waseme sisi Wazanzibari wao Watanganyika.

Nje ya muungano hawawezi kusema hivyo, nje ya muungano hakuna Wazanzibari. Nje ya muungano kuna wao Wapemba sisi Waunguja. Nataka mjue hivyo… nataka mjue hivyo.

Nje ya muungano hakuna sisi Wazanzibari wao Watanganyika. Hakuna… hakuna. Kinachowafanya sasa wajiite sisi ni ubaguzi wa kuwabagua Watanganyika.

Wakishakuwabagua Watanganyika, ile dhambi ya ubaguzi haifi, inaendelea. Dhambi ya ubaguzi ukishakuitenda inaendelea, ni sawa na kula nyama ya mtu, ukila nyama ya mtu utaendelea tu. Mtamaliza, mtatengana na Watanganyika halafu mara mtakuta kumbe sisi si Wazanzibari…kuna Wapemba na kuna Waunguja.

Wapemba watapata msukosuko kidogo au aaah. Mtakuta kumbe kuna Wazanzibari na Wazanzibara. Hamtakaa salama… hamtakaa salama.

Hamuwezi kukaa salama baada ya kutenda dhambi ya kubagua watu wa nchi yenu ile ile moja, mkawaita wale wao na hawa sisi. Dhambi ile haishii hapo, ndiyo historia ilivyo, ni sheria ya historia sio sheria ya Mwalimu Nyerere.

Huwezi kufanya ubaguzi wa namna hiyo halafu dhambi ile ikuache hapo hapo. Hapana, itakuandama. Ninalolisema kwa Wazanzibari nalisema kwa Watanganyika.

Zanzibar wanaweza kujitenga kwa ujinga, kwa ulevi na hasa ujinga wa viongozi wao na Watanganyika wakabaki wameduwaa.

Wazanzibari hawa wanafanyaje? Wanatuacha hawa wenzetu jamani wanakwenda zao wenzetu!

Watanganyika walioachwa wameduwaa kwa kitendo cha Wazanzibari kuwakimbia, watabaki wamoja, hawataparaganyika.

Narudia…Wazanzibari wanaweza wakatoka, wakajitenga wenyewe tu…sasa wengine wana bendera sisi hatuna kwanini, wengine wana wimbo wa taifa sisi hatuna wimbo wa taifa kwanini?

Basi wakajitenga, si wote wanaosema hivyo ni viongozi wanaosema… basi wakajitenga, wakawaacha Watanagnyika wameduwaa…hivi wenzetu kweli wanatuacha!

Wakiwaacha Watanganyika walio katika hali hiyo, Watanganyika wanaowashanga Wazanzibari katika kuwaacha, Watanganyika hawa watakuwa salama.

Watanganyika wakiwakataa Wazanzibari kwa tendo la dhambi ile ile, sisi Watanganyika wao Wazanzibari… wakautukuza usisi Tanganyika na kwa ajili hiyo wakawafukuza Wazanzibari, hawabaki salama.

Hapatakuwa na Tanganyika… wakishakujitenga tu Wazanzibari wale wako kando hivi… mmewafukuza mnajidai wakubwa ninyi… hawa nani hawa… wao wana rais sisi hatuna rais kwanini… watimue.

Mkawatimua, mkapata rais wenu hapa akawatimua. Hambaki… hambaki. Kwani mtasemaje, mtakuwa mmeishasema sababu ya kuwafanya wale wao na ninyi ni ninyi… wao vipi?

Wazanzibari… halafu mbaki ninyi? Maana wako watakaosema Wazanzibari tu… Wazanzibari kana kwamba kuna kabila Wazanzibari, mmewabagua.

Mtaanza nyumba za Wapemba, mtaziingilia pale sasa hivi. Viko vijumba vya Wapemba humu baadhi yao walikimbia wakati uleeee, vijumba vya kwanza vitapitiwa… Wapemba… Wapemba, mtamaliza vya Wapemba.

Halafu mtakuta ninyi mliokuwa mnajiita sisi… sisi Watanganyika, mtakapoanza kuchoma nyumba za Wapemba zile mtakuta aah si sisi… sisi hawa wote si wamoja.

Mbona za Wapemba tunachoma za Wachaga hatuchomi kwanini. Kwani Wachaga si wazawa bwana, hapa kuna wazawa hapa, sasa mnachoma za Wachaga mnaacha?

Mtakuta hakuna watu wanaitwa Watanganyika, mtakuta mlijidanganya mnadhani kuna watu wanaitwa Watanganyika, hakuna.

Kuna Wagogo, kuna Wanyamwezi, kuna Wasukuma, kuna Wazanaki, kuna Wakurya, kuna Wamwera… wengi sana, siwezi kuwataja wote.

Mtakuta hakuna kitu kizima hivi kinaitwa sisi Watanganyika… hata kidogo. Na madhali mmefanya dhambi ya kusema wao Wazanzibari si wenzetu… dhambi ile ile itawatafuna nyinyi.

Na mimi nasema Mwenyezi Mungu anisamehe, mnastahili iwatafune. Hamuwezi kutenda dhambi kubwa namna hiyo bila adhabu… na dhambi nyingine zimo mle mle ndani ya kitendo hazisubiri."
 
DALLAI LAMA

JF-Expert Member
Jan 31, 2012
8,614
2,000
Vp wamekunywa tena gongo kama huko Tabora?

Pili..hapo hakuna watu zaidi ya wanachama wa ccm waliozombwa na mabasi ya Mtei toka jimbo la NYALANDAU na MJINI KWA UFADHILI WA DEWJI.

TAARIFA ZOTE TUNAZO.
 
DALLAI LAMA

JF-Expert Member
Jan 31, 2012
8,614
2,000
Unavyosema Singida Mashariki ipo nyuma kimaendeleo kwa kuwa eti lipo chini ya Lissu,vp nyie miaka 40 iliyopita mbona hamkuhamasisha maendeleo.

MBONA SINGIDA VIJIJINI,IRAMBA NA HANANG NA KWINGINE AMBAYO WAPO WABUNGE WA CCM PIA HALI NI MBAYA SANA?

YAHITAJI UWE PUNGUANI KUWAELEWA CCM.
 
Arushaone

JF-Expert Member
Mar 31, 2012
14,944
2,000
Reveald: Kinana na timu yake wamekomba pesa nyingi Lumumba wakitafutia umaarufu na Kinana anapima upepo kwani anataka kugombea urais. Waliwapiga marufuku kina Lowassa kwa lengo hilo.

CC: DALLAI LAMA.
 
Last edited by a moderator:

DALLAI LAMA

JF-Expert Member
Jan 31, 2012
8,614
2,000
Reveald: Kinana na timu yake wamekomba pesa nyingi Lumumba wakitafutia umaarufu na Kinana anapima upepo kwani anataka kugombea urais. Waliwapiga marufuku kina Lowassa kwa lengo hilo.

CC: DALLAI LAMA.

Wanywaji wa gongo hawa.

Urais umekuwa mwepesi kweli!

Eti Kinana,Membe,Wassira ,Kigwangalah wanautaka.

Bora Ningezaliwa Eritrea kwa Ushombe wangu.
 
Last edited by a moderator:

mangimeza

Senior Member
May 13, 2011
189
225
Reveald: Kinana na timu yake wamekomba pesa nyingi Lumumba wakitafutia umaarufu na Kinana anapima upepo kwani anataka kugombea urais. Waliwapiga marufuku kina Lowassa kwa lengo hilo.

CC: DALLAI LAMA.

Hapo itabidi biashara ya pembe za ndovu ihalalishwe
 
Last edited by a moderator:

Simiyu Yetu

JF-Expert Member
Apr 29, 2013
18,939
2,000
Kinana ni muuaji wa vyama vya upinzani sijui kama vitabaki salama kwa kasi hii ya kinana.
 
Simiyu Yetu

JF-Expert Member
Apr 29, 2013
18,939
2,000
Reveald: Kinana na timu yake wamekomba pesa nyingi Lumumba wakitafutia umaarufu na Kinana anapima upepo kwani anataka kugombea urais. Waliwapiga marufuku kina Lowassa kwa lengo hilo.

CC: DALLAI LAMA.
Nakuona kwenye akili yako kama unaandamwa na wimbi la ukabila vile hebu jitazame kwanza vizuri,halafu usirudie tena kusema mambo ambayo huyajui wala huna uhakika nayo.
 
Mhabarishaji

JF-Expert Member
Oct 5, 2010
1,005
2,000
Ifuatayo ni sehemu ya hotuba ya Mwalimu Nyerere kwa waandishi wa habari mwaka 1995 hasa kuhusu mustakabali wa muungano:

“Watu wamezungumza Uzanzibari, baadhi ni viongozi wetu wanajivunia Uzanzibari. Nadhani wengine wanafikiria hata kujitenga, sio wengi, lakini wapo.

Kujitenga maana yake ni kuvunja nchi, kusiwe na nchi moja bali mbili. Hili ni jambo linazungumzwa.

Tunataka viongozi, kiongozi wanaoelewa hilo. Kuzungumza Uzanzibari si jambo la fahari. Hatima yake utavunja nchi. Mtu mwenye akili, Mzanzibari ana akili hawezi akautuza Uzanzibari wa kujiita sisi Wazanzibari na wao Watanganyika.

Na adhani ile ina usalama ndani yake. Kufanya hivyo, hatima yake Zanzibar itajitenga.

Zanzibar ikijitenga, kutokana na ulevi tu…sisi Wazanzibari wao Watanganyika…sisi si wamoja. Ulevi tu…ulevi hasa ulevi wa madaraka.

Ikitokea hivyo, sisi Wazanzibari wao Watangayika. Wakumbuke kwamba muungano ndio unaowafanya waseme sisi Wazanzibari wao Watanganyika.

Nje ya muungano hawawezi kusema hivyo, nje ya muungano hakuna Wazanzibari. Nje ya muungano kuna wao Wapemba sisi Waunguja. Nataka mjue hivyo… nataka mjue hivyo.

Nje ya muungano hakuna sisi Wazanzibari wao Watanganyika. Hakuna… hakuna. Kinachowafanya sasa wajiite sisi ni ubaguzi wa kuwabagua Watanganyika.

Wakishakuwabagua Watanganyika, ile dhambi ya ubaguzi haifi, inaendelea. Dhambi ya ubaguzi ukishakuitenda inaendelea, ni sawa na kula nyama ya mtu, ukila nyama ya mtu utaendelea tu. Mtamaliza, mtatengana na Watanganyika halafu mara mtakuta kumbe sisi si Wazanzibari…kuna Wapemba na kuna Waunguja.

Wapemba watapata msukosuko kidogo au aaah. Mtakuta kumbe kuna Wazanzibari na Wazanzibara. Hamtakaa salama… hamtakaa salama.

Hamuwezi kukaa salama baada ya kutenda dhambi ya kubagua watu wa nchi yenu ile ile moja, mkawaita wale wao na hawa sisi. Dhambi ile haishii hapo, ndiyo historia ilivyo, ni sheria ya historia sio sheria ya Mwalimu Nyerere.

Huwezi kufanya ubaguzi wa namna hiyo halafu dhambi ile ikuache hapo hapo. Hapana, itakuandama. Ninalolisema kwa Wazanzibari nalisema kwa Watanganyika.

Zanzibar wanaweza kujitenga kwa ujinga, kwa ulevi na hasa ujinga wa viongozi wao na Watanganyika wakabaki wameduwaa.

Wazanzibari hawa wanafanyaje? Wanatuacha hawa wenzetu jamani wanakwenda zao wenzetu!

Watanganyika walioachwa wameduwaa kwa kitendo cha Wazanzibari kuwakimbia, watabaki wamoja, hawataparaganyika.

Narudia…Wazanzibari wanaweza wakatoka, wakajitenga wenyewe tu…sasa wengine wana bendera sisi hatuna kwanini, wengine wana wimbo wa taifa sisi hatuna wimbo wa taifa kwanini?

Basi wakajitenga, si wote wanaosema hivyo ni viongozi wanaosema… basi wakajitenga, wakawaacha Watanagnyika wameduwaa…hivi wenzetu kweli wanatuacha!

Wakiwaacha Watanganyika walio katika hali hiyo, Watanganyika wanaowashanga Wazanzibari katika kuwaacha, Watanganyika hawa watakuwa salama.

Watanganyika wakiwakataa Wazanzibari kwa tendo la dhambi ile ile, sisi Watanganyika wao Wazanzibari… wakautukuza usisi Tanganyika na kwa ajili hiyo wakawafukuza Wazanzibari, hawabaki salama.

Hapatakuwa na Tanganyika… wakishakujitenga tu Wazanzibari wale wako kando hivi… mmewafukuza mnajidai wakubwa ninyi… hawa nani hawa… wao wana rais sisi hatuna rais kwanini… watimue.

Mkawatimua, mkapata rais wenu hapa akawatimua. Hambaki… hambaki. Kwani mtasemaje, mtakuwa mmeishasema sababu ya kuwafanya wale wao na ninyi ni ninyi… wao vipi?

Wazanzibari… halafu mbaki ninyi? Maana wako watakaosema Wazanzibari tu… Wazanzibari kana kwamba kuna kabila Wazanzibari, mmewabagua.

Mtaanza nyumba za Wapemba, mtaziingilia pale sasa hivi. Viko vijumba vya Wapemba humu baadhi yao walikimbia wakati uleeee, vijumba vya kwanza vitapitiwa… Wapemba… Wapemba, mtamaliza vya Wapemba.

Halafu mtakuta ninyi mliokuwa mnajiita sisi… sisi Watanganyika, mtakapoanza kuchoma nyumba za Wapemba zile mtakuta aah si sisi… sisi hawa wote si wamoja.

Mbona za Wapemba tunachoma za Wachaga hatuchomi kwanini. Kwani Wachaga si wazawa bwana, hapa kuna wazawa hapa, sasa mnachoma za Wachaga mnaacha?

Mtakuta hakuna watu wanaitwa Watanganyika, mtakuta mlijidanganya mnadhani kuna watu wanaitwa Watanganyika, hakuna.

Kuna Wagogo, kuna Wanyamwezi, kuna Wasukuma, kuna Wazanaki, kuna Wakurya, kuna Wamwera… wengi sana, siwezi kuwataja wote.

Mtakuta hakuna kitu kizima hivi kinaitwa sisi Watanganyika… hata kidogo. Na madhali mmefanya dhambi ya kusema wao Wazanzibari si wenzetu… dhambi ile ile itawatafuna nyinyi.

Na mimi nasema Mwenyezi Mungu anisamehe, mnastahili iwatafune. Hamuwezi kutenda dhambi kubwa namna hiyo bila adhabu… na dhambi nyingine zimo mle mle ndani ya kitendo hazisubiri.”

"Msimtumie Nyerere kama hirizi" - Jaji Joseph Sinde Warioba. <> Weka hapa na ile hotuba ambayo Nyerere alizungumzia rushwa, pale aliposema, "Anayecheza na rushwa anatakiwa kucharazwa viboko kabla hajaingia gerezani, halafu wakati anapotoka gerezani, anatakiwa acharazwe viboko vingine vya nguvu, ambavyo vitaacha alama ambazo atakwenda kumwonyesha mke wake nyumbani." Angekuwepo Nyerere leo, safu yote ya uongozi wa CCM mngecharazwa viboko!!! Mbona hili hamlisemi ????????
 
LOVI MEMBE

JF-Expert Member
Mar 16, 2012
1,122
1,250
Ccm hutumiahotuba pale zinapowafeva otherwise hawa manyangau anchana nao.muone nape anavyojifanya kuwa dereva wa trekta. Hii ni aibu kwao kuzunguka nchi nzima wakizugazuga watu.
 
measkron

JF-Expert Member
Apr 11, 2011
3,784
2,000
Reveald: Kinana na timu yake wamekomba pesa nyingi Lumumba wakitafutia umaarufu na Kinana anapima upepo kwani anataka kugombea urais. Waliwapiga marufuku kina Lowassa kwa lengo hilo.

CC: DALLAI LAMA.

Usishangae ukisikia kinana anagombea urais 2015... Hii ziara ya kila upande wa nchi una jambo nyuma ya pazia... This is introduction kwa wananchi
 
Last edited by a moderator:

habariyamujini

JF-Expert Member
May 16, 2013
3,094
1,225
Kwa hakika Lissu ni miongoni mwa wabunge ambao hata YESU akirudi hawezi kupita tena. Amekwamisha miradi mingi ya maendeleo na wananchi wamekuwa wakihangaika Usiku kucha!

Lissu alihamasisha kufukia visima vitano vilivyojengwa na wafadhili na kuwaambia atawajengea yeye hadi Leo na wananchi wake wakitaabika yeye akiendelea kunywa maji ya chupa ya Kilimanjaro!

Wilaya ya Ikungi ni ya mwisho kwa kila kitu Mkoa wa Singida, wapo nyuma kwa ujenzi wa zahanati na vituko vya afya, ujenzi wa vyumba vya madarasa, nyumba za walimu, maabara katika shule za sekondary, maji, umeme nk!

Anasema wananchi walale hata Uniform za watoto wao serikali itawapatia bure wanafunzi na chakula majumbani Kwao!

Tusubiri 2015....
 
habariyamujini

JF-Expert Member
May 16, 2013
3,094
1,225
Lissu ni mzigo usiobebeka hata kidogo! Huyu ni miongoni mwa wabunge wa CDM ambao wameprove failure kwa 100%. Ni mtu mwenye ulaghai uliokithiri!

Uzuri wake anajua fika kuwa come 2015 hawezi kurudi na mwenyewe anasema hawezi kugombea tena na ana mawazo ya kugombea Singida Mjini na Dewji! Huko ndiko atakapopata kipigo cha paka mwizi mchana kweupe!

Kwa hakika Lissu ni zaidi ya mzigo!
 
habariyamujini

JF-Expert Member
May 16, 2013
3,094
1,225
Lissu ndio maana Ana diwani mmoja Kati ya madiwani 29! Ni balaa kubwa! Musiojua siasa za singida endeleeni kushangilia lakini Uzuri wake mwenyewe anajua Hali yake Jimboni
 
MwanaDiwani

JF-Expert Member
Mar 22, 2013
5,535
1,195
Reveald: Kinana na timu yake wamekomba pesa nyingi Lumumba wakitafutia umaarufu na Kinana anapima upepo kwani anataka kugombea urais. Waliwapiga marufuku kina Lowassa kwa lengo hilo.

CC: DALLAI LAMA.
Ndugu, Mlidhani kazi za Mzee Kinana ni nguvu ya soda au ya ndege wa angani kama wanavyofanya baadhi ya viongozi wa upinzani wanaorusha helikopta ikiwa na chama kwenye mafaili waliyobeba.

Wakishuka kwenye helikopta wanashuka na chama chote na wakipanda kwenye helikopta kuondoka, wanaondoka na chama chote.

Tulifahamu mtashangaa kwa sababu mlizoea siasa za mazoea ambazo hazina ajenda za kitaifa ambazo ni endelevu. Katika mshangao wenu mmeanza kutafuta mchawi kama walivyo viongozi wa vyama vya upinzani wanakimbia vivuli vyao na kuilalamikia CCM pale wanaposhindwa katika harakati zao za siasa za zimamoto.

Tunasikia kwa sasa kile kikundi kinachojiita UKAWA kimebadilisha ajenda ya mizunguko yao waliyodai ni Katiba na kwa sasa Mzee Kinana ndiyo ajenda.
 
MwanaDiwani

JF-Expert Member
Mar 22, 2013
5,535
1,195
"Msimtumie Nyerere kama hirizi" - Jaji Joseph Sinde Warioba. <> Weka hapa na ile hotuba ambayo Nyerere alizungumzia rushwa, pale aliposema, "Anayecheza na rushwa anatakiwa kucharazwa viboko kabla hajaingia gerezani, halafu wakati anapotoka gerezani, anatakiwa acharazwe viboko vingine vya nguvu, ambavyo vitaacha alama ambazo atakwenda kumwonyesha mke wake nyumbani." Angekuwepo Nyerere leo, safu yote ya uongozi wa CCM mngecharazwa viboko!!! Mbona hili hamlisemi ????????
Ndugu, Wewe unaamini kazi ya hirizi?. Kama huamini, kwa nini unaweka mfano wa hirizi ujenge mantiki ya hoja?.

Mimi nimeweka hotuba ninayoifahamu, kama unadhani kuna hotuba nyingine, unaweza kuweka kwa sababu Jukwaa nila kila mwanaJF
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom