Kinana: Mchungaji Msigwa ni muungwana, aliniomba radhi baada ya kushindwa kunilipa fidia baada ya kutiwa hatiani nami nimemsamehe

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
83,903
141,850
Katibu mkuu mstaafu wa CCM Mzee Kinana amemsifu Mchungaji Msigwa kwa uungwana wa kuomba radhi kwa uzushi aliomzushia.

Kinana anasema baada ya uzushi huo alimshtaki Msigwa Mahakama Kuu ambapo alikutwa na hatia na kutakiwa kumlipa fidia Mzee Kinana.

Baada ya hukumu mchungaji Msigwa alimtafuta Mzee Kinana kupitia kwa rafiki zake ndipo akamkubalia waonane na walipokutana Msigwa aliomba radhi kwa uzushi ule na Mzee Kinana akamsamehe kwa sharti moja tu kwamba kama alivyomchafua kwa kuutangazia umma basi aurudie umma ule ule na kuujuza kuwa taarifa zile zilikuwa uongo mtupu.

Mchungaji Msigwa alikubali na kiungwana kabisa akaongea na taifa na kulijuza juu ya upotoshaji alioufanya hapo nyuma.

Maendeleo hayana vyama!

Pia soma:

1) Mchungaji Msigwa akiri kumsingizia Kinana ujangili, amwangukia na kumwomba radhi

2) HOTUBA ya Kambi ya Upinzani Bungeni, Maliasili na Utalii na Peter Msigwa (FULL TEXT)

3) Kinana kupitia Wanasheria amuandikia Msigwa kumtaka amuombe radhi

4) Mchungaji Msigwa (CHADEMA) amtaka Kinana awahi kortini

5) Kinana amburuza Msigwa kortini

6) Msigwa amuomba mzee Mtei akaongee na Kinana ili wayamalize!

7) Mahakama kuamua kesi ya Kinana leo
 
Kumbe ile taarifa ya Msigwa nilijua ameokoka na kumuomba Kinana msamaha on the "contrary' kumbe ilikuwa ni shinikizo la Kinana baada ya kuingilia muhimili wa Mahakama akashinda kesi!!
 
Kuomba msamaha Ni uungwana.kama kinana alivyomwomba jpm kwa kumwambia kwamba ame changanyikiwa.
 
Mkuu si useme ukweli tu!kuwa huyu ndie mgombea uraisi zanzibar??au kaogopa kuwekwa kwenye kiroba na kutoswa majini???maana ccm ya jiwe haina huruma!!
 
Katibu mkuu mstaafu wa CCM Mzee Kinana amemsifu Mchungaji Msigwa kwa uungwana wa kuomba radhi kwa uzushi aliomzushia.

Kinana anasema baada ya uzushi huo alimshtaki Msigwa Mahakama Kuu ambapo alikutwa na hatia na kutakiwa kumlipa fidia Mzee Kinana.

Baada ya hukumu mchungaji Msigwa alimtafuta Mzee Kinana kupitia kwa rafiki zake ndipo akamkubalia waonane na walipokutana Msigwa aliomba radhi kwa uzushi ule na Mzee Kinana akamsamehe kwa sharti moja tu kwamba kama alivyomchafua kwa kuutangazia umma basi aurudie umma ule ule na kuujuza kuwa taarifa zile zilikuwa uongo mtupu.

Mchungaji Msigwa alikubali na kiungwana kabisa akaongea na taifa na kulijuza juu ya upotoshaji alioufanya hapo nyuma.

Maendeleo hayana vyama!

Pia soma:

1) Mchungaji Msigwa akiri kumsingizia Kinana ujangili, amwangukia na kumwomba radhi

2) HOTUBA ya Kambi ya Upinzani Bungeni, Maliasili na Utalii na Peter Msigwa (FULL TEXT)

3) Kinana kupitia Wanasheria amuandikia Msigwa kumtaka amuombe radhi

4) Mchungaji Msigwa (CHADEMA) amtaka Kinana awahi kortini

5) Kinana amburuza Msigwa kortini

6) Msigwa amuomba mzee Mtei akaongee na Kinana ili wayamalize!

7) Mahakama kuamua kesi ya Kinana leo
Mbona kama kuna pembe tatu hapo imefanyika yule kamuomba huyu msamaha na huyu kumuomba mkwe wake huyu msamaha kulikoni 😎
 
Mzee anajikosha baada ya kulainika kwa jiwe kama Big G iliyotafunwa na karanga. Hata huo msamaha kaombwa na Msigwa ambaye yuko njiani kwenda kuunga mkono juhudi. Huyo Msigwa alitaka kulipiwa faini na jiwe kwa kisingizio cha ushemeji sijui ukwe.
 
Bwashee haya mambo yalishapita, sasa mjipange na uchaguzi msijepigwa muanze kulia lia.
 
Back
Top Bottom