Kinana kukutana kwenye kikao cha faragha na wabunge wa CCM

MwanaDiwani

JF-Expert Member
Mar 22, 2013
5,536
2,264
KATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Abdulrahman Kinana anatarajiwa kukutana na wabunge wa CCM mwishoni mwa wiki hii mjini Dodoma. Mkutano huo kati ya Kinana na wabunge wa chama chake, utatanguliwa na kikao cha Kamati Kuu (CC), itakayokutana Ijumaa chini ya Mwenyekiti wake, Rais Jakaya Kikwete.

Kwa mujibu wa chanzo cha kuaminika kutoka ndani CCM na kuthibitishwa na watendaji wa ngazi ya juu, kilisema mkutano wa Kinana na wabunge hao umelenga kuwapa meno ya kuibana Serikali na mawaziri mizigo ambao wamekuwa wakilalamikiwa na wananchi.

"Kamati Kuu ya CCM itakutana Ijumaa wiki hii, chini ya Mwenyekiti wake Rais Jakaya Kikwete, Jumamosi Kinana atakutana na wabunge wote wa CCM ambao wengi wapo hapa mjini Dodoma wakiendelea na vikao vya Bunge.

"Ndugu yangu unajua Kinana amebadili sura ya CCM, kuna hofu huenda katika kikao cha CC mambo mazito yakaibuka ikiwemo kuwajibishwa kwa baadhi ya mawaziri ambao wameonekana wakiiangusha Serikali kutokana na utendaji wao kuwa duni," kilisema chanzo hicho.

Kutokana na hali hiyo, RAI ilimtafuta Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye ambaye alithibitisha kuwepo kwa kikao hicho.

"Ni kweli CC itakutana wiki hii mjini Dodoma na itajadili masuala mbalimbali, ila kinachojadiliwa ni siri ya kikao kwa sasa, kwani hakiwezi kuwa wazi kwa kipindi hiki.

"Suala tunajadili nini subiri baada ya kikao, mambo yote tutayaweka wazi, CCM hatuna utamaduni wa kuwaficha mambo," alisema Nape.

Hata hivyo alipoulizwa kuhusu kuhojiwa kwa mawaziri ‘mizigo' na CC alisema hayuko tayari kuzunngumzia jambo hilo ila sekretarieti ndiyo yenye wajibu wa kuandaa ajenda ambazo zitawasilishwa.

Hivi karibuni, Kinana alitangaza kuwajibishwa kwa mawaziri watatu ambao huenda wakawajibishwa na CC kutokana na kushindwa kutatua kero za wananchi.

Mawaziri wanaolalamikiwa ni pamoja na Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika, Mhandisi Christopher Chiza na Naibu wake, Adamu Malima, Waziri wa Fedha, Dk. Wiliam Mgimwa.

Wengine ni Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Dk. Shukuru Kawambwa na Waziri wa Maji, Profesa Jumanne Maghembe.

Hata hivyo, Waziri Chiza na naibu wake, Adamu Malima wanadaiwa tangu walipoteuliwa kushika madaraka hayo, wameshindwa kutekeleza wajibu wao wa kuongoza wizara hiyo ambapo inaelezwa kuwa hawajawahi kutembelea Mkoa wa Ruvuma ambao ni ghala la chakula.

Wakati huo huo Wenyeviti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wa mikoa mbalimbali nchini, wametoa tamko la kuwataka mawaziri na viongozi wote wa serikali waliotakiwa kuripoti mbele ya Kamati Kuu ya chama hicho, kufanya hivyo kwa ajili ya kuchukuliwa hatua za kisheria.

Tamko hilo lilitolewa jijini Dar es Salaam jana na wenyeviti hao kupitia viongozi wao, wakati wakizungumza na waandishi wa habari juu ya kuunga mkono jitihada zilizoonyeshwa na Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana na sekretarieti ya chama hicho.

"Viongozi na watendaji wengine wote wa serikali walioonyesha udhaifu mkubwa katika kutekeleza majukumu yao na ambao walipewa wito wa kuhudhuria mbele ya Kamati Kuu ya CCM, wachukuliwe hatua zinazostahili," alisema Mgana Msindai, ambaye ni Mwenyekiti wa Wenyeviti wa CCM Mikoa nchini na kuongeza:

"Tunawakumbusha viongozi wa serikali watambue kuwa Chama Cha Mapinduzi, kinaisimamia serikali kwa mujibu wa Ilani ya CCM ya mwaka 2010 hadi 2015, sura ya tisa. Tunaitaka serikali kuchukua hatua za haraka kurekebisha udhaifu huo."

Msindai alisema Kinana amekuwa akikemea kwa nguvu zote udhaifu mbalimbali ambao umekuwa ukifanywa na baadhi ya watendaji wa serikali kama vile ubadhirifu wa mali za umma na utekelezaji duni wa miradi ya maendeleo.

Wenyeviti hao walisema wanamuunga mkono Kinana na sekretarieti ya CCM kwa msimamo huo, kwani tangu alipopewa wadhifa huo wa Ukatibu Mkuu, ameonyesha uwajibikaji mkubwa ambao umekiwezesha chama hicho kupata uhai mpya na kuamsha ari na matumaini kwa Watanzania.

Wenyeviti hao pia waliwataka viongozi wote ndani ya chama hicho ambao hawatekelezi majukumu yao kikamilifu kwamba bora waondoke na wawachie Chama chao.

Chanzo: Gazeti la Rai na Nipashe.
 
..

.....Dhu!!! maigizo bado yanaendelea!!!!

jamani wakati mwingine kuweni na aibu.....
 
Kinana kama anaipenda ccm katika kuutumikia umma, awaambie wabunge wa ccm wawatimue mawaziri wafuatao,mizengo pinda, Hawa ghasia, shukuru kawambwa, matayo david, filipo mulugo, na sofia simba. Nje ya hapo bado ccm itaendelea kuwa chama cha mafisadi na kulindana!
 
Hamna jipya miaka yote yamekuwa yakijadiliwa hayo na cc lakni sikio lakufa halisikii dawa
 
Kinana kama anaipenda
ccm katika kuutumikia umma, awaambie wabunge wa ccm wawatimue mawaziri
wafuatao,mizengo pinda, Hawa ghasia, shukuru kawambwa, matayo david,
filipo mulugo, na sofia simba. Nje ya hapo bado ccm itaendelea kuwa
chama cha mafisadi na kulindana!

Mbona cdm hawaja wafukuza wanao kopeshana ruzuku ya serikali akina babu slaa?au NITONYE.
 
KATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Abdulrahman Kinana anatarajiwa kukutana na wabunge wa CCM mwishoni mwa wiki hii mjini Dodoma. Mkutano huo kati ya Kinana na wabunge wa chama chake, utatanguliwa na kikao cha Kamati Kuu (CC), itakayokutana Ijumaa chini ya Mwenyekiti wake, Rais Jakaya Kikwete.

Kwa mujibu wa chanzo cha kuaminika kutoka ndani CCM na kuthibitishwa na watendaji wa ngazi ya juu, kilisema mkutano wa Kinana na wabunge hao umelenga kuwapa meno ya kuibana Serikali na mawaziri mizigo ambao wamekuwa wakilalamikiwa na wananchi.

“Kamati Kuu ya CCM itakutana Ijumaa wiki hii, chini ya Mwenyekiti wake Rais Jakaya Kikwete, Jumamosi Kinana atakutana na wabunge wote wa CCM ambao wengi wapo hapa mjini Dodoma wakiendelea na vikao vya Bunge.

“Ndugu yangu unajua Kinana amebadili sura ya CCM, kuna hofu huenda katika kikao cha CC mambo mazito yakaibuka ikiwemo kuwajibishwa kwa baadhi ya mawaziri ambao wameonekana wakiiangusha Serikali kutokana na utendaji wao kuwa duni,” kilisema chanzo hicho.

Kutokana na hali hiyo, RAI ilimtafuta Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye ambaye alithibitisha kuwepo kwa kikao hicho.

“Ni kweli CC itakutana wiki hii mjini Dodoma na itajadili masuala mbalimbali, ila kinachojadiliwa ni siri ya kikao kwa sasa, kwani hakiwezi kuwa wazi kwa kipindi hiki.

“Suala tunajadili nini subiri baada ya kikao, mambo yote tutayaweka wazi, CCM hatuna utamaduni wa kuwaficha mambo,” alisema Nape.

Hata hivyo alipoulizwa kuhusu kuhojiwa kwa mawaziri ‘mizigo’ na CC alisema hayuko tayari kuzunngumzia jambo hilo ila sekretarieti ndiyo yenye wajibu wa kuandaa ajenda ambazo zitawasilishwa.

Hivi karibuni, Kinana alitangaza kuwajibishwa kwa mawaziri watatu ambao huenda wakawajibishwa na CC kutokana na kushindwa kutatua kero za wananchi.

Mawaziri wanaolalamikiwa ni pamoja na Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika, Mhandisi Christopher Chiza na Naibu wake, Adamu Malima, Waziri wa Fedha, Dk. Wiliam Mgimwa.

Wengine ni Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Dk. Shukuru Kawambwa na Waziri wa Maji, Profesa Jumanne Maghembe.

Hata hivyo, Waziri Chiza na naibu wake, Adamu Malima wanadaiwa tangu walipoteuliwa kushika madaraka hayo, wameshindwa kutekeleza wajibu wao wa kuongoza wizara hiyo ambapo inaelezwa kuwa hawajawahi kutembelea Mkoa wa Ruvuma ambao ni ghala la chakula.

Wakati huo huo Wenyeviti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wa mikoa mbalimbali nchini, wametoa tamko la kuwataka mawaziri na viongozi wote wa serikali waliotakiwa kuripoti mbele ya Kamati Kuu ya chama hicho, kufanya hivyo kwa ajili ya kuchukuliwa hatua za kisheria.

Tamko hilo lilitolewa jijini Dar es Salaam jana na wenyeviti hao kupitia viongozi wao, wakati wakizungumza na waandishi wa habari juu ya kuunga mkono jitihada zilizoonyeshwa na Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana na sekretarieti ya chama hicho.

“Viongozi na watendaji wengine wote wa serikali walioonyesha udhaifu mkubwa katika kutekeleza majukumu yao na ambao walipewa wito wa kuhudhuria mbele ya Kamati Kuu ya CCM, wachukuliwe hatua zinazostahili,” alisema Mgana Msindai, ambaye ni Mwenyekiti wa Wenyeviti wa CCM Mikoa nchini na kuongeza:

“Tunawakumbusha viongozi wa serikali watambue kuwa Chama Cha Mapinduzi, kinaisimamia serikali kwa mujibu wa Ilani ya CCM ya mwaka 2010 hadi 2015, sura ya tisa. Tunaitaka serikali kuchukua hatua za haraka kurekebisha udhaifu huo.”

Msindai alisema Kinana amekuwa akikemea kwa nguvu zote udhaifu mbalimbali ambao umekuwa ukifanywa na baadhi ya watendaji wa serikali kama vile ubadhirifu wa mali za umma na utekelezaji duni wa miradi ya maendeleo.

Wenyeviti hao walisema wanamuunga mkono Kinana na sekretarieti ya CCM kwa msimamo huo, kwani tangu alipopewa wadhifa huo wa Ukatibu Mkuu, ameonyesha uwajibikaji mkubwa ambao umekiwezesha chama hicho kupata uhai mpya na kuamsha ari na matumaini kwa Watanzania.

Wenyeviti hao pia waliwataka viongozi wote ndani ya chama hicho ambao hawatekelezi majukumu yao kikamilifu kwamba bora waondoke na wawachie Chama chao.

Chanzo: Gazeti la Rai na Nipashe.
Chiza na wahandisi wenzake wameteka miradi yote ya wizara ya kilimo, kuanziaa pembejeo hadi ujenzi wa miradi, hi ndio serikaki ya Chukua Chako Mapema CCM ukoo wa panya wooote wezi
 
Chiza na wahandisi wenzake wameteka miradi yote ya wizara ya kilimo, kuanziaa pembejeo hadi ujenzi wa miradi, hi ndio serikaki ya Chukua Chako Mapema CCM ukoo wa panya wooote wezi
Mie najiuliza sasa kinana akiulizwa kuhusu meno
ya tembo atasemaje? Kweli huo ni ukoo wa panya
 
Mie najiuliza sasa kinana akiulizwa kuhusu meno
ya tembo atasemaje? Kweli huo ni ukoo wa panya
Yaani, bila kuipumzisha Ccm hamna lamaana litafanyika, wameshafanya hii nchi kama nyumba yao, leo nimeshangaa sana hata fisadi Chenge ati ana huruma na Watanzania, aibu tupu magamba
 
Back
Top Bottom