Kinana: Hakuna Waziri mwenye ubavu wa kukataa nikimtuma Jambo

Boniphace Kichonge

JF-Expert Member
Jul 31, 2017
1,606
1,956
Wadau,
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana amesema kuwa hakuna Waziri mwenye ubavu wa kukataa jambo akimtuma. Amesema kuwa CCM ndiyo chama kilichoshika dola hivyo kama kuna changamoto yoyote basi anamuita Waziri na kumuagiza atatue changamoto hiyo.

Ametoa kauli hiyo leo tarehe 24/11/2017 kwenye mkutano wa kampeni kumnadi mgombea wa udiwani wa chama hicho Kata ya Moita Bwawani, Ndugu Prosper Damuni huko Wilayani Monduli.

========

Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana amesema hakuna waziri mwenye ubavu wa kukataa akimtuma jambo.

Amesema hayo leo Ijumaa Novemba 24,2017 katika mkutano wa hadhara uliofanyika Kijiji cha Moita Bwawani akimnadi mgombea wa CCM wa Kata ya Moita wilaya ya Monduli, Prosper Damuni.

"CCM ndiyo chama kilichoshika dola kama kuna changamoto sehemu yoyote namwambia waziri anayehusika anafika haraka eneo hilo kusikiliza na kutatua changamoto hiyo, hakuna waziri mwenye ubavu wa kukataa nikimtuma," amesema Kinana.

Katibu mkuu huyo amewaomba wananchi katika kata 43 zinazofanya uchaguzi mdogo wa udiwani kuwachagua wagombea wa CCM akisema ndicho chama kinachoongoza dola na ahadi zinazotolewa zinatekelezeka.

Kinana amewaomba wananchi hao akisema ni wakati muafaka kwao kuacha kupiga kura kwa ushabiki.

Amesema wilaya hiyo inakusanya mapato ya ndani ya Sh2 bilioni kwa mwaka wakati bajeti yao kwa mwaka ni Sh49 bilioni kwa mwaka fedha ambazo zinatolewa na Serikali Kuu hivyo ni muhimu kuwa na diwani anayetoka chama hicho ili kurahisisha maendeleo ya wananchi.

Kinana amesema anafahamu wilaya hiyo ina changamoto mbalimbali ambazo zinahitaji kutatuliwa.

"Nataka nimpe mbinu mgombea wenu akichaguliwa anatakiwa kuwa karibu sana na mkurugenzi mtendaji wa wilaya na kwa kuwa anatokana na CCM atakuwa na uwezo wa kuingia na kutoka kwenye ofisi za Serikali kutafuta fedha za maji, barabara, afya na elimu hiyo ndiyo kazi ya diwani si kukaa tu kusubiri maendeleo yaje," alisema Kinana

-Mwananchi-
 
Sasa ole sendeka kafuata nin huko tena
Watu wanapenda kujipendekeza kama nin sijui kaacha mkoa wake huku Njombe kaenda huko
Au naye anataka uwaziri
Hao ndo akina grace,mtaja olewa bure
 
CCM watueleze kama sisi kama watanzania mafanikio yao ya kutuletea maendeleo na sio nao wanakuja kwa wananchi na siasa kama za upinzani kwa kutoa ahadi ambazo wameshindwa kuzitekeleza yaani watia aibu hadi kuleta kinyaa.
 
Mkuu, labda kwa hao mawaziri, anaweza kuthubutu kwa bashite? Mziki wake toka kwa mkulu atauweza? Mwenzake Nape alithubutu na kubaki kulalama pembeni. Kuna wakuguswa na wakuto kuguswa.
Je 2nd 1st L. !?
 
Amechomekea ili ofisi kuu ikijubu iwe double impact... Ila akiwa mjanja akawa cool ameshinda mtihani akijibu rudia msg hii
 
Ahadi zipi wakati huduma za jamii mbovu...

Ona Wananchi wanavyokimbilia Matibabu kwenye Meli ya Wachina...

Kuna mahali mambo hayako sawa...
 
Back
Top Bottom