Kinana: Elimu ya Bure Mpaka Kidato cha Sita Inawezekana Kabisa

Dr. Slaa hana uwezo wa kuitekeleza hii ahadi naamini hata yeye anajua hilo. Wanasiasa ni waongo!

Mpe kura yako uone!! Kwani CCM wanaweza wenyewe!! Mkuu siasa za chama hazina uhusiano na serikari. Kwa hali ya kwaida serikari si chama kabisa. So chama chochote chaweza kuchukua drivers' seat na kiakongoza!!! lol! Ndo maana hairuhusiwi kutumia rasilimali ya serikari kwenye kampeni. Chama hakishiki hatamu tena yalikwisha haya!!

Acha fikra mgando mkuu. Tunaomba kura yako kwa Dr. W. Slaa. Asante.
 
Chadema kwenye ilani yao wameweka mipango ya mara moja ndani ya siku 100,kati na ya muda mrefu kwa hiyo inawezekana kabisa kwa kutumia raslimari lukuki za nchi hii na udhibiti wa ufujaji wa mapato ya serikali,lazima chama kiwe na dira hatuwezi kusemasema tu bila kuwa na ndoto,hiyo ndiyo ndoto safi


Froida na Wana JF Wengine,

Hoja zenu ni za msingi sana. Nami nawashukuru sana kwa hilo. Kwa kweli inatia sana uchungu. Ila CCM hawana njia lazima wabadilike na kujirekebisha na njia bora zaidi ni kuwatoa madarakani mwaka huu kupitia sanduku la kura. Hakuna kisichowezekana.
 
Tatizo ni kuwa CCM inadhani watu tunaona mwisho ndani ya mipaka ya yetu. Ameelezwa serekali ya chadema itapunguza baraza la mawaziri na vyeo vingine kama wakuu wa mikoa sasa huyu haoni kuwa ukishapunguza hizo nafasi utakuwa na fedha za zaidi. Watupishe waone.
 
tatizo lao hawa jamaa ni wezi wa kubwa.
wataiba mpaka ilani hii ya uchaguzi.
 
Hata walioendelea sana kuliko sisi wameshindwa kutoa elimu ya bure kwa kila mtu mpaka form six ndio tuwe sisi?

Hii ahadi haina tofauti na zile za JK kujenga viwanja vya kimataifa kila mkoa. Badala ya kutengeneza vizuri uwanja JK Nyerere wao wanakuja na ahadi mpya kila siku.

Dr. Slaa hana uwezo wa kuitekeleza hii ahadi naamini hata yeye anajua hilo. Wanasiasa ni waongo!

Kama nani walioendelea kuliko sisi wameshindwa kutoa elimu ya bure? Hebu toa mfano mmoa wa nchi iliyoendelea inayoshindwa kutoa elimu ya bure? Taja tu nchi moja kaka, sio unatoa maneno usiyokuwa na uhakika nayo, kutoka kwenye mdomo wako unaonuka u-ccm. Mijitu mingine bana, inajiandikia tu bila kuwa na concrete proof.Marekani imeendelea sana kuliko sisi, public school ambazo zinaweza kuwa na hadhi kuliko vyuo vyetu vikuu hapo Tanzania, elimu ni bure bure!!! with high standard na vifaa vya kutisha, computer kial kona. Sikutaka kusema marekani kwa sababu tupo mbali kimaendeleo lakini kwa kuwa ndugu ulisema wanzetu waliondelea sana nimeona nikupe top hiyo
 
CHADEMA ina sera nzuri sana, and well writen and prioritized though too aggressive& optimistic lakini there is something to take from!!!

Najua hawatashinda maana naona ametishia watu ambao ndio haswa wanauwezo wa kuwapa kura... ukiwatishia kuwapunguza wakuu wa mikoa na wilaya automatically unatengeneza upinzani mkali sana! Hawa watafanya kila mbinu kuhakikisha kwamba hawaondoki.

Lakini chama chochote kitakachoshinda ni lazima nitatekeleza at least kila sehemu ya ilani za wenzako. Nakumbuka Ilani ya CHADEMA ya 1995 ndio iliyoleta UDOM.
 
Duh! Ina maana Kinana Haamini kwamba Elimu inaweza kuwa Bure Mpaka Kidato Sita? Duh Kaaazi kweli kweli!

Jamani Mimi siyo Mchumi but I happened to know mathematics

Take a simple assumption kwamba katika mwaka mmoja Shule zetu zina accomodate jumla ya wanafunzi Milioni Mbili ( 2M, hili ni kadirio la juu sana) kuanzia Form one mpaka form six

Inafahamika kwamba wanafunzi wa Boarding wanlipa 70,000 kwa mwaka na wale wa day wanalipa 20,000 kwa mwaka. To make things easy ili hata akina Kinana waelewe:

Let us assume kwamba kwa wastani kila mwanafunzi analipa 40,000 bila kujali kama ni wa boarding au wa day ( Of course day students a big in number than Boarding student) so hili ni kadirio la juu sana.

Hii ina maana kwamba katika mwaka wa Fedha Serikali kupitia Shule zake inakusanya Shilingi 40,000 kwa kila mwanafunzi wa Sekondari kwa mwaka

Kwa hiyo kwa jumla kiasi cha

40,000 Ths * 2000,000 students = 80,000,000,000 yaani bilioni Themanini

Sasa nauliza hivi Je Serikali yetu haina Uwezo wa Kuwaambia Wazazi Jamani kaeni na hizo 80 billions Serikali itazilipa? Je Serikali haipotezi pesa Nyingi kuliko hizi Bilioni 80?

Naamni mmenipata
 
Kutoa elimu bure kuanzia chekechea hadi kidato cha sita inawezekana kabisa! Hakuna serekali inayoshindwa kufanya hivyo kama nia ya kweli ipo. Kwa wale viongozi wa CCM na wafuasi wao wanosema haiwezekani,

wametusaidia kuwafahamu vizuri kuwa ni watu wasiofikiria, na wasio na upeo au hata kuwa na mawazo mapya ya kuwaletea Watanzania maisha bora. CCM inafanya kila kitu na kila uamuzi ni siasa, na hii imedhibitika katika ahadi zao mbovu na ambazo hazijatimia au sio zenye tija kwa taifa.

Kwanini nasema elimu bure kwa kiwango hicho inawezekana. Kwanza kama viongozi wetu walio madarakani walisoma bure sio tu mpaka kidato cha sita bali hadi chuo kikuu na wengine walipelekwa nje ya nchi kusoma na serekali ambayo ilikuwa masikini kuliko ilivyo sasa serekali makini inaweza. Tuwaulize hao wanaobeza wao nani aliwalipia shule?

Serekali makini inaweka vipaumbele. Kama ilivyo kwenye ilani za Chadema na CUF, imewekwa wazi kabisa kuwa elimu ndio mzingi wa maendeleo. Taifa letu limejaa watu walioishia darasa la saba, je hawa wataleta mapinduzi ya KIUCHUMI? Vyama hivi vimeweka kipaumbele kwanza kupata taifa lenye nguvu kazi ya hali ya juu. Hili linawezekana kwa kukata matumizi kwenye mambo mengine yasiyo ya lazima kwa sasa kama kuwa na serekali kubwa, matumizi ya anasa na vitu kama hivyo.

Ni dhahiri kabisa kuwa baada ya miaka kadhaa taifa likiwa na nguvu kazi makini, ikavutia uwekezaji na ukuaji wa uchumi, Watanzania watakuwa matajiri na uwezo wa kujisomesha. Wakati huo sasa kipaumbele kitakuwa ni kwenye sector nyingine kama Ulinzi, Mahusiano ya kimataifa, na mambo mengine.

Hivyo watanzania tusidanganyike na hawa wanaosema hili haliwezekani, bali tufurahi kwa kuwa tumewajua kwa rangi zao halisi kuwa hawaingii madarakani kwa ajili ya kuwatetea Masikini na wale waliokosa nafasi sawa za kushiriki katika maendeleo yao binafsi na ya nchi kwa ujumla.

Tuwakimbize watu hawa kwa kuwa ni wabinafsi, wanatumia gharama kubwa kuagiza samani za ndani, kuwa serekali kubwa isiyo na tija, kuwa na sheria kandamizi, kuendesha magari ya anasa kila mwaka wakibadili, kusafiri kwa ndege kwenda mikoani na kuwadhihaki watanzania waliodanganyika.
 
Una Point kubwa!!!!!,

Mshahara wa mbunge na waziri mmoja ni karibu na mishahara ya waalimu wa jimbo zima. Safari moja ya rais nje ya nchi ni zaidi ya mishahara ya waalimu wote nchi nzima kwa mwaka mmoja!. kamisheni ya 10-20% ya contract moja ya serikali na BAE systems au ujenzi wa barabara moja inaweza kuwa zaidi ya mishahara wa waalimu wote nchi nzima kwa mwaka mmoja. Tax holiday ya kampuni moja ya madini ni zadi ya mishahara ya waalimu wote Tanzania kwa miaka mitano.

It is a matter of setting right priorities!!!!!!!!!!!!!!!
 
Watanzania wepesi wa kusahau au tumelogwa? Miaka ya nyuma mbona iliwezekana kuanzia shule ya msingi hadi chuo kikuu elimu ilikuwa bure na ilikuwa unapewa masurufu ya njiani pamoja na kulipiwa nauli kwenda na kurudi nyumbani.
 
headline_bullet.jpg
Ataja kodi zitakazogharimia huduma hizo



SlaaBukombe%283%29.jpg

Mgombea urais kupitia Chadema, Dk. Willibrod Slaa



Mgombea urais kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Dk. Willibrod Slaa, amendeelea kusisitiza kuwa iwapo atapata ridhaa ya kuiongoza serikali, huduma za elimu na afya zitalipiwa na serikali.
Dk. Slaa alisema fedha za kulipia huduma hizo zitatokana na msamaha wa kodi ya mafuta ambayo ni Sh. bilioni 700 kwa mwaka.
Aidha alisema wataondoa mashangingi kwa viongozi wa serikali ambayo hutumia gharama kubwa ya mafuta na kupunguza mshahara kwa rais kwa asilimia 20 na wabunge na taasisi zingine kwa asilimia 15.
Alisema hayo wakati akihutubia mkutano mkubwa wa kampeni uliofanyika katika soko la Mbauda, jijini hapa.
Wakati akiwa mjini hapa, msafara wa Dk. Slaa ulizongwa na mamia ya wananchi waliotaka kusalimiana naye ambao walifunga barabara na kuwapa kazi ya ziada polisi na askari wa kikosi cha kutuliza ghasia (FFU) ambao walilazimika kuwatawanya wananchi kwa busara.
Msafara wa Dk. Slaa ambao ulitokea hoteli ya Impala kupitia barabara ya Sokoine kuelekea Mbauda, ulilazimika kusimama kwa muda katika makutano ya mtaa wa Azimio baada ya wananchi kufunga njia.
Akiwahutubia wananchi hao, waliokuwa na shauku kubwa ya kumsikiliza, Dk. Slaa alisema zipo fedha zilizotengwa kwa baadhi ya kampuni kwa ajili ya kunusuru uchumi mwaka jana ambazo aliahidi kuwa atazitaja baada ya kuzifanyia kazi kwa kina.
"Ninawajuwa kwa majina, nitawataja baada ya kuyafanyiakazi," alisema Dk. Slaa.
Awali akiongoea katika mkutano huo, mwanzilishi na muasisi wa Chadema, Mzee Edwin Mtei, ameeleza kushangazwa na kasumba ya kulindana ndani ya Chama Cha Mapinduzi
Aidha alisema inashangaza watu ambao walituhumiwa na kufukuzwa kazi leo hii wanapigiwa debe kwamba ni viongozi wazuri…nasikia furaha kusikia haya kwa sababu najua watu wanahitaji mabadiliko na wakati wa mabadiliko ni sasa,” alisema.
Alisema ana imani kubwa na Dk. Slaa, ambaye anawania urais kupitia Chadema, kwa kuwa ni mchapakazi, mwaminifu na mwenye uwezo wa kusimamia rasilimali za taifa ili ziwanufaishe wananchi wote.
Wakati huo huo, Mgombea ubunge katika jimbo la Monduli, Mollel Silanga, ameeleza kutishiwa kuuawa na wapinzani wake wa kisiasa na kueleza kwamba madiwani wake akiwemo wa Kata ya Islalei ametoroka kwa siku nne mfululizo akihofia kuuawa.
Akizungumza kwa kutumia neno la Mungu, alisema tangu alipoingia kwenye mchakato wa kuwania ubunge katika jimbo la Monduli, amekuwa akifuatwa ili ajiondoe na kutishiwa kuuawa.
“Nimepeleka taarifa kwa vyombo vyote vya sheria, ulinzi na usalama lakini sijapata msaada mkubwa, nipo katikati ya kushinda ubunge, kuhongwa au kuuawa, nahitaji sana sala zenu,” alisema.
Mbali na jimbo la Monduli lenye upinzani mkali, Jimbo la Arusha mjini nalo lina mpambano mkali kati CCM na Chadema ambapo CCM imemsimamisha Waziri wa Mazingira, Dk. Batilda Buriani anayechuana vikali na Godbless Lema wa Chadema.



CHANZO: NIPASHE JUMAPILI

haya tena Mpeni kura Mzee Dk.Slaa elimu na afya bure wayaaaaaaaaaaaaaaa huyu anafaa kuwa Kiongozi wetu
 
Mbona hii nawezekana asubuhi sana. Kwa taarifa yenu tu, ufisadi wa fedha ya umma katika kila Halmashauri wa wilaya ukikomeshwa, fedha inatosha kutoa elimu ya sekondari zote wilayani. Yaani kuna kujidanganya kwingi katika uendeshaji wa seriakli ya sasa. Kuna mianya mingi ya upotevu wa fedha, na ikidhibitiwa kuna fedha ya kutosha bila hata kuhitaji ufadhili toka nje. Tanzania ya Nyerere iliwezekana, kwa nini isiwezekane sasa.

Tena iliwezekana vizuri sana tukilipiwa na serikali hata nauli. Nilitoka Mkoa wa Ziwa Magharibi kwenda kusoma Bagamoyo Seko kwa gharama za serikali, kuanzia nauli, masomo, madaftari, karatasi na vitabu, malazi na chakula hadi gharama za toilet papers. Wakati huo hata tulikuwa hatujaanza kuchimba madini yetu, mbuga zetu za hifadhi ya taifa zilikuwa bado hazijajulikana sana ughaibuni pia serikali ilikuwa bado inatoa ruzuku kwa mashirika ya umma!! Serikali ya Dk .Slaa yenye utashi haiwezi kushindwa kutimiza ndoto zetu hizi!

NDIYO, CHADEMA WANAWEZA.
 
Wakati wa jk nyerere iliwezekana vipi?rwanda ambayo imesifiwa kwa kutimiza masharti ya millenium wameweza vipi?sera ya ccm ni kudidimiza elimu au kuiua elimu kwa kiini macho cha sekondari za kata{majengo}ili umtawale binaadamu bila matatizo mnyime elimu hii ndio sera ya ccmmungu ibariki tanzania
mbona hii nawezekana asubuhi sana. Kwa taarifa yenu tu, ufisadi wa fedha ya umma katika kila halmashauri wa wilaya ukikomeshwa, fedha inatosha kutoa elimu ya sekondari zote wilayani. Yaani kuna kujidanganya kwingi katika uendeshaji wa seriakli ya sasa. Kuna mianya mingi ya upotevu wa fedha, na ikidhibitiwa kuna fedha ya kutosha bila hata kuhitaji ufadhili toka nje. Tanzania ya nyerere iliwezekana, kwa nini isiwezekane sasa.
 
Ndugu zangu Akina kinana wanatia kinyaa. Malengo yao ni kuhakikisha nchi hii inamilikiwa na wachache wenye elimu bora na wale wenzangu ambao wana uchumi mbovu, wafilie mbali au kuendelea kuwa mbumbumbu.

Katika gazeti la Mwanahalisi uk.2 kuna malipo ya CCM kwa serikali kutokana na kukodi nduge ya Salma ili afanye kampeni. Katika habari hiyo, gharama ya kukodi ndege ni US$ 3,000 kwa saa sawa na Tsh 4,600,000! Sawa na Tsh 22,950,000 kwa siku. Tukumbuke kuwa CCM kwa sasa inatumia ndege 4 (1 Salma na 3 JK); so kwa wastani kwa siku wanatumia Tsh 91,800,000. kama wangetumia ndege moja tu kwa ajili ya JK basi tungekuwa tunaseve 68,850,000 kwa siku. Ndege hizo hutumia Tsh 2,065,500,000. :crutch:
Hizo ni kwenye ndege. Kuna sourses nyingi sana kama kwenye madini, kodi kwa wafanyabiashara wakubwa, Exchange on foregn currency, Unnecesary expenditures n.k. Zaidi ya hayo Jaji Mfulila katika gazeti la Mwananchi Jumatatu anasemaa "Hao wanaosema haiwezekani, mbona kwetu iliwezekana?" Kwa maana Hao (wazee wetu including Mkapa, Mwinyi, Jk, Majaji wote ni watanzania wenye haki sawa na sisi) waliweza kusoma bure; kwanini kizazi hiki isiwezekane kama siyo ubinafsi?

TAFAKARI CHUKUA HATUA
NI HAKI YA KILA MTANZANIA KUSOMA MPAKA MWISHO WA UWEZO WAKE KUJIENDELEZA; VIONGOZI WASIWE VIKWAZO VYA MAENDELEO YETU:eek2:


 
Hawa nia yao ni kuona kuwa watoto wao pekee ndio wanaopata fursa ya kupata elimu ili baadaye wao (watoto wao) waje wawe watawala wa nchi hii.
Ni rahisi, kwanza unawanyima elimu wanayostahili waliowengi halafu unapitisha sheria inayokataza mtu ambaye hana shahada angalau moja kuwania uongozi (udiwani, ubunge, utendaji wa vijiji, kata, etc).
Pili unatumia vyombo vya maamuzi vya chama kuhakikisha kuwa wagombea wote wanapita kwenye chekechekeo lao hivyo kuwafanya wote wanaotaka uongozi kukiabudu kikundi hiki cha watawala na kwa kufanya hivyo unahakikisha kuwa viongozi wote waliopo ni watiifu kwa kikundi cha watawala ambao wanatokana na kundi dogo la watawala. Mfano sasa kundi hili linaundwa na Lowasa, Rostam, Mkapa, Chenge, Kiwete, Makamba, Mullah, na wengine wa aina hiyo. Na hawa ndio wanaoamua nani agombee wapi, bila kujali anakubalika ama la kwani wanapesa, vyombo vya habari na vyombo vya ulinzi kuhakikisha kuwa wanayemtaka (hicho kikundi cha majangili) anapita hata kama wananchi hawamtaki
 
Hawa nia yao ni kuona kuwa watoto wao pekee ndio wanaopata fursa ya kupata elimu ili baadaye wao (watoto wao) waje wawe watawala wa nchi hii.
Ni rahisi, kwanza unawanyima elimu wanayostahili waliowengi halafu unapitisha sheria inayokataza mtu ambaye hana shahada angalau moja kuwania uongozi (udiwani, ubunge, utendaji wa vijiji, kata, etc).
Pili unatumia vyombo vya maamuzi vya chama kuhakikisha kuwa wagombea wote wanapita kwenye chekechekeo lao hivyo kuwafanya wote wanaotaka uongozi kukiabudu kikundi hiki cha watawala na kwa kufanya hivyo unahakikisha kuwa viongozi wote waliopo ni watiifu kwa kikundi cha watawala ambao wanatokana na kundi dogo la watawala. Mfano sasa kundi hili linaundwa na Lowasa, Rostam, Mkapa, Chenge, Kiwete, Makamba, Mullah, na wengine wa aina hiyo. Na hawa ndio wanaoamua nani agombee wapi, bila kujali anakubalika ama la kwani wanapesa, vyombo vya habari na vyombo vya ulinzi kuhakikisha kuwa wanayemtaka (hicho kikundi cha majangili) anapita hata kama wananchi hawamtaki

THE CITIZEN
Capitation policy 'highly flawed'
Friday, 24 September 2010

By Florence Mugarula

The primary school students' capitation grant which was introduced under the capitation grant policy in 2002 has failed to serve its purpose, a survey conducted by Uwazi-Twaweza has established.

Addressing reporters yesterday, the Uwazi-Twaweza managing director, Mr Rakesh Rajani said that the primary school capitation grant needs serious changes to enable students benefit from the policy.

Uwazi is part of Twaweza, a new citizen-centered initiative, focusing on large-scale change in East Africa region.

Mr Rajan said this when revealing the report of a survey on capitation grant. He said the $10 (about Sh14,000) grant a year to each primary school pupil was not enough to buy books and other academic materials and that its value has declined by over 35 percent since it was established about nine years ago.

"It has been established that there was a need to make changes in the whole system so that there could be positive improvement in the education sector," said Mr Rajan.

The analysis report shows that the policy was introduced in order to replace the revenues lost to schools because of the abolition of fees and to improve the quality of education by making real resources available at the school level.

According to the report, at least Sh80 billion was allocated in 2009/10 fiscal year under the Primary Education Development Programme (PEDP) but still there were no enough improvement which reflect the allocated funds.

The report established that the allocation of Sh14,000 ($10) to each pupil has never been adhered and only Sh4,189 has been actually provided for each pupil.

The report reads also that the amount was not enough to the extent that even if it was released in full, it was too small to cover the cost of learning materials.

It added that the actual capitation grant disbursements were less than what was allocated in the budget, and thus it was so unpredictable for proper planning.

The report establishes that the amount allocated in the budget for capitation grants has systematically been lower than the amount stated in the PEDP policy adopted by cabinet.

According to the report, in 2007/08 the shortfall in capitation grant was Sh4,481 per pupil as government allocated Sh5,519 per pupil.

Mr Rajan said that there was a need to revise the policy and allocate more money to enable the implementation of different school programmes.
Commenting on the problems that hinder the development of primary school education in the country, Mr Rajan said the analysis has established also that the allocated money was not delivered on time thus delaying implementation of development programmes.

He added that there was no transparency among teachers, government officials and wananchi in general on the capitation grant.

But the PEDP coordinator from the ministry of Education and Vocation Training, Mr Benedict Mtui told The Citizen that the delay or timing of cash depend on the response of the donors.

According to Mr Mtui, the government always asks for cash from different areas and that it becomes difficult to allocate fund to a particular school if there is no response from the source.

"We fail to provide money on time, and sometimes we offer less amount because we are also receiving money from donors, so some give us on time and other delay or nothing at all therefore that is how this problem happen," said Mr Mtui.

Commenting on the transparency on allocating and using of the fund, Mr Mtui said the reports were published in the government gazette but currently all reports were exposed on the ministry of Finance and Economic Affairs website.

The Uwazi-Twaweza Research analyst, Ms Rose Aiko said the present price for the book was between Sh3,500 and Sh5,000 and that the 40 percent of Sh10,000 which is currently offered by the government was not even enough to buy a single book.

She said, in order to foster education sector, the government must increase the amount of capitation grants to primary school pupils.
According to Twaweza, at least sh 13,000 were needed to each pupil just for buying books alone.


WAKUBWA HII NDIO HALI HALISI YA UTEKELEZAJI ILANI YA CCM YA 2005 PAMOJA NA SERA ZILIZOTUNGWA NA SERIKALI YENYEWE YA CCM HUSUSAN KATIKA SEKTA YA ELIMU.

SERIKALI YA CCM ILIJIPANGIA SERA YAKE YA ELIMU KUWA KAMA IFUATAVYO:- The Education and Training Policy adopted in 1995 sets the policy for the education sector in Tanzania.
The Education sector has a vision for Tanzania to be:
"a nation with high level of education at all levels; a nation which produces the quality and quantity of educated people sufficiently equipped with the requisite knowledge to solve the society's problems, in order to meet the challenges of development and attain competitiveness at regional and global levels".

The mission of the Ministry of Education and Culture in this regard is over achingly to:
"Realise Universal Primary Education (UPE), eradicate illiteracy and attain a level of tertiary education and training commensurate with critical high quality human resources required to effectively respond to the development challenges at all levels".



WAKATI AMBAPO SERIKALI ILIAHIDI KATIKA SERA YA PRIMARY EDUCATION DEVELOPMENT PROGRAMME (PEDP) ILIYOPITISHWA NA BARAZA LA MAWAZIRI (2002) NA SERIKALI YA KIWETE KUAHIDI KUENDELEA KUTEKELEZA AHADI HIZO ILIPOINGIA MADARAKANI MWAKA 2005, KUWA KILA MWAKA SERIKALI ITAMTENGEA KILA MWANAFUNZI WA SHULE YA MSINGI HAPA TANZANIA DOLA $10 ZA KIMAREKANI SAWA NA SHILINGI 10,000 (2002) AU SHS 14,000 (2010) (KUTOKANA NA KUSHUKA KWA THAMANI YA FDHA YA KITANZANIA) KAMA MATUMIZI YA MWANAFUNZI HUYO KUPATA ELIMU YA MSINGI.

KATIKA YA BAJETI YA 2007/8 SERIKALI YA KIKWETE ILIMTENGEA KILA MWANAFAUNZI SHILINGI 5,519/= TU, KATI YA SHILINGI 10,000/=.FEDHA ILIYOTENGWA INATOSHA KUNUNUA KITABU KIMOJA CHA KUFUNDISHIA KWA BEI ZA MWAKA HUO.

KATIKA BAJETI YA 2009/10 SERIKALI YA KIKWETE ILITENGA KIASI CHA SHILINGI BILIONI 80 TU KWA AJILI YA ELIMU YA MSINGI SAWA NA SHILINGI 4,189/= TU KWA KILA MWANAFUNZI BADALA YA SHILINGI 14,000/=. KIASI HICHO NI PUNGUFU NA KILE KILICHOTENGWA KATIKA BAJETI YA 2007/8 KWA SHILINGI 1,330/= KWA KILA MWANAFUNZI ILIHALI GHARAMA ZA KILA KITU KILICHATAKIWA KATIKA KUMUELIMISHA MWANAFUNZI ZILIONGEZEKA MARADUFU

NDUGU ZANGU JE HUKU NDIO JAKAYA KIWETE ANAKOITA UTEKELEZAJI WA SERA BORA ZA CCM NA AHADI NA ILANI YA CCM YA 2005?

NDIO MAANA CCM WANAKATAA KUINGIA KWENYE MIDAHALO KUKWEPA KUULIZWA MASWALI JINSI WALIVYOSHINDWA KUELEKEZA RASLIMALI ZA TAIFA KUWANUFAISHA WANANCHI WENGI NA BADALA KUNUFAISHA KIKUNDI KIDOGO CHAA WATEULE NDANI YA CCM.

BADALA YA WAGOMBEA WA UPINZANI NA WANANCHI KUCHEZA NGOMA ZA CCM NA KIKWETE ZA KUTOA NA KUPOKEA AHADI MPYA; NI VYEMA WAGOMBEA WA UPINZANI NA WANANCHI WAKAJIELEKEZA KATIKA SERA ZA CCM ZILIVYOTEKELEZWA KATI YA 2005 HADI 2010 KWA KUWA UTEKELZAJI HUO ULIFANYIKA KWA KUTUMIA RASLIMALI ZA TAIFA. HII ITATUSAIDIA KUPATA MAFUNZO MAZURI JUU YA UWEZO WA CCM NA VIONGOZI WAKE KUSIMAMIA UTEKELZAJI WA SERA, ILANI NA AHADI WANAZOTOA SASA.

KWA KUANZIA TUPITIE SERA ZA ELIMU ZA CCM KAMA ZINVYOONEKANA HAPO HAPO JUU NA TUTAFAKARI YALIYOJITOKEZA KATIKA TAARIFA YA UTAFITI KUHUSU SEKTA YA ELIMU KATIKA GAZETI LA CITIZEN; NA TAARIFA YA UTAFITI MWINGIONE KUWA ZAIDI YA 50% YA WANAFUNZI WANAOMALIZA DARASA LA SABA HAWAJUI KUSOMA NA KUANDIKA KISWAHILI, HISABATI NA KIINGEREZA.

KWA HALI HII, JE NI KWELI KUWA CCM NA KIKWETE WANATEKELEZA AHADI, SERA ZAO, ILANI YA CCM YA 2005 KWA UFANISI WA KUTOSHA? AU WANANCHI TUNATAKIWA KUBORESHA USIAMAMIZI WA RASLI MALI ZA TAIFA HILI KWA KUONGEZA UFANISI WA BUNGE LA JAMHURI YA MUUNGANO LENYE JUKUMU YA KUISIMAMIA SERIKALI ILIYOKO MADARAKANI JINISI INAVYOTUMIA RASLI MALI ZA TAIFA?

WANANCHI WANA MCHANGO MKUBWA SANA KATIKA UBORESHAJI WA USIMAMIZI WA RASLIMALI ZA TAIFA KWA KUPUNGUZA IDADI YA WABUNGE WA CHAMA TAWALA NDANI YA BUNGE NA KUONGEZA IDADI YA WABUNGE KUTOKA KAMBI YA UPINZANI KWA KUWAPIGIA KURA KWA WINGI ZAIDI TAREHE 31 OKOTOBA 2010 KATIKA KILA JIMBO LA UCHAGUZI.

UKO NDIO KAMPENI ZA UCHAGUZI MKUU WA 2010 ZINATAKIWA KUELEKEA ILI RASLIMALI NYINGI ZINAZOTUMIKA KATIKA MCHAKATO HUU ZIWEZE KUWA NA TIJA KWA WANANACHI NA TAIFA HILI, BADALA YA KUTUMIKA KUWAPATIA WANANCHI BURUDANI YA BONGO FLEVA NA AHADI MPYA ZISIZOTEKELEZWA.

 
Back
Top Bottom