Kinana: Elimu ya Bure Mpaka Kidato cha Sita Inawezekana Kabisa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kinana: Elimu ya Bure Mpaka Kidato cha Sita Inawezekana Kabisa

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Sabi Sanda, Aug 30, 2010.

 1. S

  Sabi Sanda JF-Expert Member

  #1
  Aug 30, 2010
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 412
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Gazeti la TanzaniaDaima la Leo (30/08/2010) limemkariri Kinana akiwataka CHADEMA waeleze ni vipi wataweza kutoa elimu ya bure mpaka kidato cha sita. Naamini CHADEMA watafanya hivyo.

  Ila kwa upande mwingine naamini Kinana anafahamu fika kuwa hilo la elimu ya bure mpaka kidato cha sita linawezekana bila tatizo. Kinachokosekana ni ubunifu na utashi wa kisiasa toka serikali ya CCM.


  Naamini wote tunafahamu ya kuwa katika ngazi ya shule za msingi hakuna ada ambayo wanafunzi wanatakiwa kulipa. Ila kwa upande wa shule za sekondari ada kwa shule za Serikali ni shilingi elfu 20 kwa mwaka kwa wanafunzi wa kutwa na kwa wale wa bweni ni shilingi elfu 70 kwa mwaka.

  Na idadi ya wanafunzi wote kuanzia kidato cha kwanza mpaka cha sita kwa shule za Serikali hawazidi 1.3M na wengi ni wa kutwa. Pia tukumbuke kuwa familia nyingi zimekuwa zikipata shida sana kuweza kuwalipia ada watoto wao pamoja na michango mbalimbali.

  Na mbaya zaidi. wanafunzi wengi wanaojiunga na shule za kata hutakiwa pia kwenda na madawati kama sio kutoa mchango kwa ajili ya madawati. Hii aibu na fedheha kwa nchi yetu itaisha lini?? Hapa bado hatujazungumzia zaidi ya asilimia 35% ya wanafunzi wetu katika shule za msingi wanakaa chini.

  Hapa ni muhimu tukakumbuka kuwa kwa mwaka mmoja tu wa fedha posho za wakuu Serikalini na viongozi ni zaidi ya shilingi bilioni 215. Serikali ipunguze posho hizo kwa asilimia 45 tu tuone kama itashindikana kutoa elimu ya bure mpaka kidato cha sita. Hapa bado hatujazungumzia tena fedha nyingi zinazotumika vibaya na kuibwa Serikali kuu na serikali za mitaa---Rejea Taarifa za ukaguzi za CAG za kila mwaka.

  Kinana anaposema CHADEMA waeleze pia watalipaje mishahara ya Walimu, anakosea kwani Walimu hawajilipi mishahara yao wao wenyewe bali hulipwa na Serikali Kuu. Hoja hapa ni kufuta ada toka kidato cha kwanza mpaka kidato cha sita. Suala la mishahara ya Walimu linaingiaje?


  CCM wasione aibu. Wawe wakweli na wakubali kuwa elimu ya bure inawezekana kabisa mpaka kidato cha sita. Tatizo ni kukosekana kwa utashi wa kisiasa wa kufanya hivyo. Pia wakumbuke kuwa CHADEMA wamekwenda mbali zaidi na kuahidi kuwa Elimu mpaka kidato cha sita itakuwa ya lazima.


  Mwisho nawapongeza sana CHADEMA kwa kuja na wazo la UHURU SCHOLARSHIP FUND kwa ajili ya Wanafunzi Wetu wa Elimu ya Juu. Naamini Ilani yao ina maelezo kamilifu kuhusu Mfuko huu na pia watafafanua zaidi katika mikutano yao ya kampeni inayoendelea.
   
 2. N-handsome

  N-handsome JF-Expert Member

  #2
  Aug 30, 2010
  Joined: Jan 23, 2008
  Messages: 2,317
  Likes Received: 128
  Trophy Points: 160
  Nataka nicheke
   
 3. Plato

  Plato JF-Expert Member

  #3
  Aug 30, 2010
  Joined: Aug 28, 2010
  Messages: 421
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 33
  Nami naamini hiyo itawezekana.ccm wapumzike.si hawawezi!!
   
 4. B

  Baija Bolobi JF-Expert Member

  #4
  Aug 30, 2010
  Joined: Feb 25, 2009
  Messages: 931
  Likes Received: 697
  Trophy Points: 180
  Mbona hii nawezekana asubuhi sana. Kwa taarifa yenu tu, ufisadi wa fedha ya umma katika kila Halmashauri wa wilaya ukikomeshwa, fedha inatosha kutoa elimu ya sekondari zote wilayani. Yaani kuna kujidanganya kwingi katika uendeshaji wa seriakli ya sasa. Kuna mianya mingi ya upotevu wa fedha, na ikidhibitiwa kuna fedha ya kutosha bila hata kuhitaji ufadhili toka nje. Tanzania ya Nyerere iliwezekana, kwa nini isiwezekane sasa.
   
 5. K

  Keil JF-Expert Member

  #5
  Aug 30, 2010
  Joined: Jul 2, 2007
  Messages: 2,214
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Kulingana na report ya CAG, kwa wastani kila mwaka serikali huwa inapoteza zaidi ya 25% ya fedha za bajeti ama kwa manunuzi hewa au kuwa na receipts ambazo ziko questionable. Tukianzia na hizo hela, zinaweza kufanya mengi sana katika kuboresha mishahara ya wafanyakazi na ku-improve huduma za jamii (afya, elimu na maji).

  Wafanyabiashara wakubwa wengi wao ni wakwepa kodi wazuri sana, serikali ikihakikisha hakuna anayekwepa kodi kuna hela nyingi sana ambazo zinaweza kukusanywa na TRA na hivyo kuongeza revenue ya serikali.

  Kuna vyanzo vingi sana vya mapato ambavyo vigogo wa CCM ni wadau kwenye hizo biashara na matokeo yake wamekuwa wakigoma kupandisha ada na kodi kwenye vyanzo hivyo kwa visingizio mbali mbali. Mfano kwenye vitalu vya uwindaji na hata kwa wavuvi wanaovua samaki kwenye ukanda wa bahari ya Tanzania, wakitozwa ada kuna hela nyingi zana inaweza kukusanywa.

  Hoja ya Bwana Mgaya (Katibu Mkuu wa TUCTA) bado iko valid, kwamba bajeti ya serikali kuu kwa ajili ya watumishi wa umma, 41% ndio hulipa mishahara na 59% hulipa posho. Kwanini wasipunguze posho na kuongeza mishahara? Kuna baadhi ya ofisi wanalipana posho za vikao kwa kuhudhuria vikao ambavyo vinafanyika saa za kazi na tena ofisini kwa wahusika. Sasa kwanini mtu alipwe posho na huku akitimiza majukumu yake na tena ndani ya masaa ya kazi?

  Uwezekano wa kuboresha huduma za jamii upo na ni mkubwa na pia uwezekano wa kuongeza mishahara ya wafanyakazi wa serikali upo na inawezekana kabisa. Tatizo ni kwamba serikali iliyo madarakani ni ya wafanyabiashara ambao hawataki kulipa kodi, hawataki kulipa ada kubwa, na pia ni mafisadi wakubwa.
   
 6. Gobret

  Gobret JF-Expert Member

  #6
  Aug 30, 2010
  Joined: Jun 11, 2010
  Messages: 320
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 35
  Siamini macho yangu kama kweli Tz haiwezi kutoa elimu bure hadi kidato cha sita kwa watoto wetu ambao watakuwa wazazi na viongozi wa kesho.

  Hatuna sababu ya kuwa na serikali ambayo haina ndoto hiyo. Kwa sababu sisi tulio na Uwezo na nafasi watoto wetu watapata fursa ya kupata elimu hatuna hata wazo la kuwasaidia watoto ambao familia zao haina uwezo wa kuwapa elimu. Watanzania waliowengi wangekuwa wanaelewa hila za hawa wachache CCM wangeiweka pembeni na kuichagua CHADEMA waone kama inawezeka au haiwezekana kutoa elimu bure hadi kidato cha sita. Mimi naamini kuwa inawezekana TENA SANA.

  CHAGUA DK SLAA KWA MAENDELEO. GOD BLESS HIM.
   
 7. B

  Baija Bolobi JF-Expert Member

  #7
  Aug 30, 2010
  Joined: Feb 25, 2009
  Messages: 931
  Likes Received: 697
  Trophy Points: 180
  ======
  Perfectly analyzed. Na ndiyo maana huwezi kumsikia Kikwete katika kampeini zake akiahidi kuboresha utendaji wa serikali yake. Kwake huo ni mwiba mkali maana atawagusa mafisadi. Mimi nashangaa kuona hili suala halimkeri. Ahadi zake zote ni bure kama hataliangalia hili la utendaji serikalini. Kwa ujumla hakuna mtu anayefanya kazi kwa moyo tena huko serikalini, lakini wanalipwa mishahara mwisho wa mwezi.
   
 8. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #8
  Aug 30, 2010
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Kikwete ni mzuri kwa ahadi za ovyo ovyo! Utasikia jiji la Mwanza kuwa Califonia, nitajenga flyovers Dar es salaam, Nitajenga Daraja mto Kilombero, Nitajenga uwanja mkubwa wa ndege wa kimataifa Kibaha. Nitatengenez kiwanda kikubwa Afrika cha kusindika Mananasi pale Chalinze hebu wananchi nipeni ridhaaa....ataendelea tena Rushwa itakwisha wakati yeye mwenyewe yuko pale kwa rushwa. Na amezungukwa na wezi akina Kinana na Meli zao.

  Watanzania amkeni, wanapenda kuendelez taifa la wajinga lisilohoji hatima yake hao CCM
   
 9. Steve Dii

  Steve Dii JF-Expert Member

  #9
  Aug 30, 2010
  Joined: Jun 25, 2007
  Messages: 6,416
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 145
  Yaani hawa wasemaji wa CCM wanakera mpaka basi tu. Yaani mtu anajiita kiongozi na hajui ni kiasi gani kinatumika kwenye anasa za kunenepeshea viongozi??

  Mibillioni ya pesa inatumika kugharamia mafuta ya mashangingi, vikao virefu vya bunge lenye ku-rubber stamp kila kitu, makongamano yasiyo na tija na longolongo ya mivitu kibao ambayo badala ya kukuza hazina yetu yanaifanya inyauke kwa kasi.

  Hapo juzi wamelipia millioni nane-nane kwa mabango ya CCM kwenye magazeti... hawajui hizi ni pesa za kutosha kuweka vyandarua kwenye bweni la shule nzima ya sekondari...badala yake wanasubiri kumtuma Mh. Kikwete kwenda kujiombeleza kwa mama Bush atuletee vyandarua!! Hizo millioni nane-nane za mabango kwenye magazeti (ambayo wananchi wameyanyofoa na kuyatupilia mbali) hawajui zingeweza kutengeneza kisima cha kudumu cha maji ya chemichemi au kununua matank ya maji ya mvua kwa sekondari mojawapo mkoani??! Wangelikuwa wanafanya kazi ambazo waliwaahidi wanachi kuzifanya, leo hii wasingelikuwa wanahaha kujitangaza!!! Ama kweli kibaya cha jitembeza...!!!

  Walivyokuwa wanasoma bure wao serikali ilikuwa inatoa wapi pesa??!
  Mimi nilifikiri wanaCCM watairudi hoja ya Chadema kwa kuja na yao kubwa " Elimu ya bure mpaka Chuoni"... badala yake wanang'aa ng'aa macho kwa kujiuliza hela zitatoka wapi??...
  -- Kwa kuuza nyumba ya gavana,
  -- kwa kusimamia ipasavyo mapato serikalini, bandari na kwenye halmashauri (mnakumbuka sakata la Ubungo bus termina?l!!!).
  -- Kwa kuongezea asilimia ya kipato cha madini kutoka kwa wawekezaji,
  -- kwa kuwawezesha watanzania kuwekeza badala ya kutegemea wageni,
  -- kwa kupunguza vikao vya serikali na muda wa bunge,
  -- kwa kutumia magari yasiyo kula mafuta sana na yenye gharama kubwa,
  -- kwa kutafuta masoko ya mazao yetu ndani na nje ya nchi....
  ni msururu wa mambo ya kufanya!!! Lakini mweeeeeee...mijitu mizima imebakia kujiita miviongozi lakini kwa yale itamkayo yaonekana haifai kabisa!!!
   
 10. Pape

  Pape JF-Expert Member

  #10
  Aug 30, 2010
  Joined: Dec 11, 2008
  Messages: 5,513
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 0
  Srikali ya ccm au serikali ya Tanzania?:confused2:
   
 11. b

  buckreef JF-Expert Member

  #11
  Aug 30, 2010
  Joined: Mar 19, 2010
  Messages: 310
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Hata walioendelea sana kuliko sisi wameshindwa kutoa elimu ya bure kwa kila mtu mpaka form six ndio tuwe sisi?

  Hii ahadi haina tofauti na zile za JK kujenga viwanja vya kimataifa kila mkoa. Badala ya kutengeneza vizuri uwanja JK Nyerere wao wanakuja na ahadi mpya kila siku.

  Dr. Slaa hana uwezo wa kuitekeleza hii ahadi naamini hata yeye anajua hilo. Wanasiasa ni waongo!
   
 12. Kigogo

  Kigogo JF-Expert Member

  #12
  Aug 30, 2010
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 20,498
  Likes Received: 1,453
  Trophy Points: 280
  kwani wakati wa Nyerere tulikuwa tunasomaje bure.Huyu Kinana vipi analeta hoja zake za kishoga hapa>people meant business this time around sio ujinga ujinga waliouzoea CCM
   
 13. Kigogo

  Kigogo JF-Expert Member

  #13
  Aug 30, 2010
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 20,498
  Likes Received: 1,453
  Trophy Points: 280
  usiwe kipofu..toa mfano nchi ipi iliyoendelea imeshindwa kutoa elimu ya bure..Kwani kenya mwai kibaki kafanyaje?usiongee vitu kama huna information za kutosha
   
 14. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #14
  Aug 30, 2010
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Ni wale wale hawezi kukujibu huyo! Nitampa mifano....Belgium na UK elimu ya Msingi na sekondari ni bure unanza kulipia chuo kikuu, hata yeye huyo anajua ila anatetea kusudi!
   
 15. B

  Baija Bolobi JF-Expert Member

  #15
  Aug 30, 2010
  Joined: Feb 25, 2009
  Messages: 931
  Likes Received: 697
  Trophy Points: 180
  ======

  Ni nchi gani iliyoendelea iliyoshindwa kutoa elimu ya kidato cha sita bure?
  Kwanza, kimsingi nchi nyingi zilizoendelea hazina vidato vya tano na sita.
  Tupe mfano ili uboreshe hoja yako.
   
 16. Njowepo

  Njowepo JF-Expert Member

  #16
  Aug 30, 2010
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 9,296
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  Sio elimu bure tuu ata Afya nayo inatakiwa iwe bure if harness propery the minerals we have and other natural resources.
  Kenya wana nini mpaka wameweza kwa kuwa tumewazidi kila kitu ie interms of natural resources ie madini,mbuga etc
  Kama wao wameweza kutoa elimu bure na kuondokana na depence kwenye budget then sisi inabidi twende mbali zaidi na Afya bure
   
 17. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #17
  Aug 30, 2010
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Fool's Gold!
   
 18. Jatropha

  Jatropha JF-Expert Member

  #18
  Aug 30, 2010
  Joined: Apr 9, 2009
  Messages: 1,152
  Likes Received: 144
  Trophy Points: 160
  Tatizo walilonalo ccm ni kuwa viongozi wote wana tuhuma za ufisadi wakiwemo mwinyi, mkapa n.k hakuna wa kumnadi jakaya kikwete, ndio maan kinana anajaribu kurejesha mapigo. Mabomu yake tulikuwa tuemmuwekea kuanzia sasa tunafungulia mbwa kwa kwenda mbele kwa kuanika madhambi yake. Mtu akimwaga mbaoga wewe mwaga ugali hadi tupate watu wasafi.

  Wakongwe wote wenye madhambi wamekacha.

  Wananchi nao wanatakiwa kuanza kuwazomea wote wenye tuhuma wakijitokeza hadharani kama alivyoshauri nbaba wa taiffa "kuwa wakati mwingine kuzomea ni dawa tosha kwa watu wazima wasiojiheshimu"
   
 19. F

  Froida JF-Expert Member

  #19
  Aug 30, 2010
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 7,900
  Likes Received: 1,328
  Trophy Points: 280
  Chadema kwenye ilani yao wameweka mipango ya mara moja ndani ya siku 100,kati na ya muda mrefu kwa hiyo inawezekana kabisa kwa kutumia raslimari lukuki za nchi hii na udhibiti wa ufujaji wa mapato ya serikali,lazima chama kiwe na dira hatuwezi kusemasema tu bila kuwa na ndoto,hiyo ndiyo ndoto safi
   
 20. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #20
  Aug 30, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Nilisema Ilani ya Chadema inatisha.. natumaini mengi yaliyomo yatazidi kulazimishwa kujadiliwa.
   
Loading...