KINANA: CCM inatawala na itatawala kwa muda mrefu kwa sababu ya "demokrasia" iliyoko ndani ya CCM

View attachment 2304117

KINANA ATAJA SABABU CCM KUKAA MADARAKANI MUDA MREFU AKIZUNGUMZA NA WANA CCM KATAVI

MAKAMU Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi(CCM) Abdulrhman Kinana ametaja sababu tatu za kwanini Chama hicho kimekaa madarakani kwa muda mrefu na moja ya sababu ni uwepo wa demokrasia ya uhuru watu kujieleza na kutoa maoni yao.

Kinana ametoa sababu hizo leo Julai 25,2022 alipokuwa akizungumza na wana CCM Mkoa wa Katavi wakati wa kikao cha ndani wa wanachama hao wakingozwa na viongozi wa Chama na Serikali ngazi ya Mkoa.

Akizungumza kwenye kikao hicho Kinana amesema kuna watu wamekuwa wakijiuliza kwanini Chama hicho kimedumu muda mrefu.”Sababu ya kwanza lakini kuna demokrasia ndani ya CCM, watu wana uhuru wa kueleza na kutoa mawazo bila hofu bila woga.

“Vikao vya Chama watu wote ni sawa, hata Mwenyekiti wetu wa CCM Taifa kwenye kikao yeye na wajumbe ni sawa.Hivyo kitu cha kwanza ni demokrasia unatoa nafasi watu kusema, kutoa maoni.Sababu ya pili uhuru wa kuchagua na kuchaguliwa.

“Ndio maana kila kipindi watu wanachagua na kuchaguliwa, kila baada ya miaka mitano nafasi imeisha, nafasi zote zinagombewa hakuna usultani wala ufalme.Hata mimi nawashukuru wajumbe kunichagua kwa kura nyingi. Nafasi yangu ina uzuri na ubaya, anayeteua ni mmoja na anayetengua ni mmoja , asiporidhika huna pauliza, huwezi kushtaki wala kuhoji.Kwa hiyo Chama hiki sifa yake kubwa ni haki ya kuchagua na kuchaguliwa,hakuna mwenye haki miliki.”

Awali akizungumza na wana CCM hao kwenye kikao cha ndani, Kinana amewapongeza wananchi wa Mkoa wa Katavi kwa kazi kubwa ya kuleta maendeleo ambayo wamekuwa wakiifanya na kwamba mkoa huo umepokea Sh.bilioni 295 kwa ajili ya kutekeleza miradi ya maendeleo na fedha hizo ameambiwa zimetokana na makusanyo ya mapato mbalimbali ya mkoa.

“Nimepokea taarifa kuhusu namna fedha za maendeleo zinavyotumika vizuri na nataka nieleze hapa Rais Samia Suluhu Hassan anafanya kazi kubwa na nzuri ya kuleta na maendeleo , Rais wetu sio msemaji sana lakini ni mtu wa vitendo,”amesema Kinana huku akitumia nafasi hiyo kueleza namna akina mama walivyowachapa kazi, wanawake ni mahodari lakini ndio wanalea familia.

Aidha ametumia nafasi hiyo kuwashukuru wabunge kwa kazi nzuri ambayo wanaifanya kwani wamekuwa na mchango mkubwa katika kuomba fedha wanapokuwa bungeni kwa kujenga hoja na wamekuwa wakipata fedha hizo ambazo ndizo zinatumika kufanya maendeleo hayo.

“Leo nimetembelea jimbo moja la Nsimbo, Mbunge wa lile jimbo amafanya kazi nzuri sana na nimemwambia ameotesha mizizi kwenda chini itakuwa ngumu kiong’oa lakini naamini na wabunge wengine nao wanafanya kazi nzuri.Pia nawapongeza madwani, watumishi wa umma , wakurugenzi wa halmashauri kwa kazi nzuri mnayofanya.

“Tunathamini kazi zenu, mnafanya kazi katika mazingira magumu na hamna majukwa ya kujitetea. Tunawashukuru mnafanya kazi nzuri sana na sisi tukipata majukwaa tutawasemea,tukiona mahali pameharibika tutasamehe, sio kila mahali unachukua hatua na sisi ni binadamu kuna mahali tunaweza kukosea.

“Madiwani pia tunawashukuru kwa kazi mnayofanya, hawana mshahara lakini wamekuwa wakipata posho ndogo ndogo, CCM tunafanya kazi kwa kujitolea, hata mimi najitolea ukiondoa hii nafasi ya Makamu Mwenyekiti nafasi hii haina mshahara.”
Mfu anapotabiriwa maisha mareeeefu🙃🙃
 
Na umezaliwa umeikuta ccm inatawala nchi,na mpaka leo wale maadui wa 60s bado wapo na wametamalaki zaidi na wamezaa cousin wao anayeitwa Rushwa, ujinga, umasikini na maradhi, tembelea huku kwetu lingusenguse ndio utaelewa bado sana!,na waambie ccm wa level playing field then uitishwe uchaguzi mkuu, ccm bila vyombo vya ulinzi na usalama ni chama mfu.
Ushuzi wa mbaazi za babati 🤣
 
CCM ilishinda 2005 pekee huku kwingine ni majanga
Relax mkuu, sijasema kuwatoa ccm mimi sio dikteta, ninachotaka ni uchaguzi huru wenye matokeo huru,chaguzi zote zilizofanyika wakati wa vyama vingi, ccm wamepata push kubwa kutoka vyombo vya usalama na facts zipo na history itakuja kuhukumu hili
 
Kinachoshangaza mkiambiwa muweke mazingira sawa na ya kidemokrasia wakati wa uchaguzi hamtaki, lakini baada ya uchaguzi mnaanza kujisifu
 
Sioni uhalali wa CCM kujigamba kwamba wanadumu sababu ya demokrasia nk.

Uwanja wa kuwania kushika madaraka sio wa haki hata kidogo.

Natoa mifano miwili hapa itokanayo na kauli za auwaliopata kuwa viongozi wakuu au wapo hadi sasa.

Mmoja alisema ukitaka biashara zako ziende vizuri uwe CCM. Na kweli jaribu kuwa tofauti ushughulikiwe na TRA nk.

Au

Wakurugenzi wanaambiwa upewe madaraka na rasilimali na jimbo liende upinzani haikubaliki.

Au unadikia pigieni upinzani lakini CCM itaunda dola.

Hivi mnaobeza upinzani mambo hayo mnayapuuzaje.

Isitoshe nani kazaliwa kuwa CCM au CHADEMA nk. Nani mwenye wajibu wa kujenga upinzani imara.

Kwangu mimi CCM wasitambie mtu waendelee kutimiza wajibu wao kimyakimya. Wasije pitiliza hadi kumshika kipofu mkono. Waache tambo.

1.
 
Sasa yuko wapi wa kuitoa CCM?

JE? NI HAWA NCCR
JE? NI HAWA TLP
JE? NI HAWA CUF
JE? NI HAWA ACT
JE? NI HAWA CHADEMA
Hayupo wa kuitoa CCM kati ya vyama hivyo.

CCM itajifanyia SUICIDE yenyewe. Tunza hiyo Kwa MATUMIZI ya badae.
 
Sioni uhalali wa CCM kujigamba kwamba wanadumu sababu ya demokrasia nk.

Uwanja wa kuwania kushika madaraka sio wa haki hata kidogo.

Natoa mifano miwili hapa itokanayo na kauli za auwaliopata kuwa viongozi wakuu au wapo hadi sasa.

Mmoja alisema ukitaka biashara zako ziende vizuri uwe CCM. Na kweli jaribu kuwa tofauti ushughulikiwe na TRA nk.

Au

Wakurugenzi wanaambiwa upewe madaraka na rasilimali na jimbo liende upinzani haikubaliki.

Au unadikia pigieni upinzani lakini CCM itaunda dola.

Hivi mnaobeza upinzani mambo hayo mnayapuuzaje.

Isitoshe nani kazaliwa kuwa CCM au CHADEMA nk. Nani mwenye wajibu wa kujenga upinzani imara.

Kwangu mimi CCM wasitambie mtu waendelee kutimiza wajibu wao kimyakimya. Wasije pitiliza hadi kumshika kipofu mkono. Waache tambo.

1.
Kama unaamini haya njoo CCM tujenge nchi yetu
 
Kuna vyama Mimi nimezaliwa, nimesoma, nimeajiriwa mwenyekiti bado ni yuleyule,

Mrema
Lipumba
Mbowe

Hahaha CCM mbele kwa mbele yaani

Ni mpaka mtakapojifunza demokrasia ni zaidi ya kuchagua au kuongoza na mtu mwingine! Ninyi ndio huwadanganya wananchi kuwa demokrasia ni kura yao! Lakini kura hiyo hiyo ndio huibwa, kuminywa nk! Mnawadanganya mia kuwa wakishapiga kura - demokrasia yao imekamilishwa na wakipigia vyama vingine kura wanaambiwa wakawaombe hao maendeleo!!

Mrema, Lipumba na Mbowe wamekuwa kwenye uongozi miaka mingi. Na chaguzi halali kwa mujibu kwa katiba zao zimewaweka walipo. Kama walivochaguliwa wenyeviti CCM mara walipopata nafasi ya kuwa Rais.

Demokrasia ni zaidi ya uchaguzi!!!
 
Sina hakika na hizo sababu zake ila nachojua CCM bado ina miongo kadhaa madarakani..
 
Back
Top Bottom