Kinana awataka viongozi kuwa wanyenyekevu

peno hasegawa

JF-Expert Member
Feb 24, 2016
12,818
21,420
Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara, Abdulrahman Kinana amewataka viongozi kuepuka utukufu, badala yake wajikite katika utumishi akisema masuala ya itifaki yanawaweka mbali na wananchi.

Amesema si vema viongozi kubanwa na itifaki na kujali utukufu heshima na hadhi ya husika kuliko mchango wake kwa wale anaowaongoza.

“Namshukuru Profesa Chijoriga (Marcelina -Mkuu wa Shule ya Uongozi ya Mwalimu Nyerere) kwa kunialika, umeomba radhi umenialika kwa muda mfupi. Lakini mimi sio mtu ninayejali sana itifaki, kwa sababu ni adui wa wananchi na maendeleo.

“Kwa hiyo ukinialika kwa mdomo, barua au ujumbe mfupi sawa, muhimu kwangu umeniita na nitaitika wito, kwa sababu kazi tuliyo nayo tuliopewa nafasi ya uongozi ni utumishi, ukijali itifaki utajali utukufu badala ya utumishi,” amesema.

Kinana ametoa kauli hiyo leo Jumatano Oktoba 12, 2022 wakati akifungua mdahalo wa kumbukizi ya Mwalimu Nyerere uliofanyika katika Shule ya Uongozi ya Mwalimu Nyerere Kibaha mkoani Pwani.

Kwa mujibu wa Kinana, masuala hayo ndio yaliyofundishwa na Hayati Nyerere kuwa wanyenyekevu, kujali watu, kutojisikia, kutojali na kuthamini cheo chako, heshima yako pamoja na hadhi yako.

“Ukitaka kujua hadhi na cheo visivyo na thamani angalia siku utakayoondoka kwenye cheo hadhi yako ilivyo,” amesema Kinana.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Taasisi ya Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere, Paul Kimiti amesema taasisi hiyo imepanga kujenga makumbusho ya mwasisi huyo pamoja na viongozi wengine waliopigania Uhuru wa Taifa hili.

“Pia na viongozi wetu waliopo katika madaraka tutaweka kumbukumbu katika jingo moja kubwa. Nimeshazungumza na viongozi wa mkoa wa Dodoma na wapo tayari kutatafutia eneo, hatutaki utani katika hili.

“Tutakuwa na bustani yenye picha viongozi wote na kila mtu atakuwa na maelezo yake. Tutakuwa na bustani yenye shamba darasa ya mafundisho kwa sababu hayati Nyerere alipenda kilimo na tunataka watu wajifunze kilimo cha kisasa,” amesema Kimiti.

Kimiti amesema kutakuwa na bustani za mabwawa ya samaki, akibainisha kuwa wanataka ifike mahali kila Mtanzania ajifunze masuala ya viongozi waliopita kama Hayati Nyerere, Ali Hassan Mwinyi, Abeid Aman Karume ili kuweka historia ya bora ndani ya Taifa.

Chanzo: Mwananchi
 
Comped Kinana fika huko Hai ukajionee vituko vya uchaguzi mkuu wa CCM ulivyo buruzwa na viongozi wa CCM mkoa na kwenye wilaya. Usipo wahi Hai, M6.bowe anawahi huko kuvuruga jimbo.
 
Back
Top Bottom