SautiYaMnyonge
JF-Expert Member
- May 13, 2018
- 439
- 742
Na Mwandishi wetu,
Korogwe, Tanga
Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Tanzania Bara, Abdulrahman Kinana amewataka madiwani na wabunge kukataa kupitisha miswada ya Sheria yenye kukandamiza haki na kuminya fursa ya wananchi wanyonge kujiendeleza kiuchumi.
Pia, amesema Sasa ni wakati muafaka kulitazama vyema kundi la wajasiriamali wadogo wakiwemo Machinga, mamalishe, waendesha bajaji na bodaboda ili wawekewe mazingira mazuri ya kunufaika na juhudi zao za kujitafutia kipato kujikwamua na umaskini.
Kinana ameyasema hayo leo mjini Korogwe, wakati akizungumza na wana CCM katika ukumbi wa Lembeni, akiwa katika ziara ya kukagua uhai wa Chama na kujitambulisha kwa wanachama.
"Madiwani ninyi ndio mnaosimamia sheria ndogo ndogo za Halmashauri, mkiona sheria hizo hazina uhusiano na wananchi kataeni. Mkiletewa sheria pelekeni kwanza kwa wananchi muwashirikishe kupata maoni yao, rahisisheni maisha ya watu, wasaidieni wakue."
"Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano na ninyi sheria ikija bungeni waambieni (serikali) kwa sasa hatuipitishi mpaka tukashauriane na wananchi waliotutuma," alisema.
#CCMImara
#KaziIendelee