• Mpendwa mteja, tunakusihi jitahidi kuosha mikono kwa maji safi na sabuni mara kwa mara na kwa siku chache hizi jaribu kutulia nyumbani kuepusha maambukizi ya #CORONAVIRUS

Kinana awakera mawaziri, baadhi wapanga kumkwepa!

  • Thread starter Kilimanjaro moja
  • Start date
K

Kilimanjaro moja

Member
Joined
Nov 30, 2012
Messages
67
Points
0
K

Kilimanjaro moja

Member
Joined Nov 30, 2012
67 0
HARAKATI mpya za Chama Cha Mapinduzi (CCM) zinazoratibiwa kwa ukaribu na Katibu Mkuu wake Abdulrahaman Kinana, katika kukabiliana na nguvu za Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) zimeonekana kuwatibua baadhi ya mawaziri, Tanzania Daima Jumapili limeelezwa.

Kitendo cha hivi karibuni cha Kinana kuandamana na mawaziri mikoani kujibu kero za wananchi, kimewakera wanasiasa hao hasa kutokana na kile walichodai kulazimishwa na wenzao kukutana na kadhia ya kuzomewa.

Kutokana na hilo, baadhi ya mawaziri sasa wanafikiria namna ya kuongozana na katibu mkuu huyo katika mikutano na hafla mbalimbali za kichama.

Baadhi ya mawaziri waliozungumza na gazeti hili wanaona kuwa kitendo cha Kinana kuongozana na baadhi yao na kuwataka wajibu kero za wananchi, ni kuwalazimisha kwenda nje ya utaratibu wao wa kazi.

Kutokana na hilo, baadhi ya mawaziri sasa wamepanga kukwepa kuongozana na Kinana kwa visingizio mbalimbali, ikiwemo kubanwa na kazi nyingi wizarani.

Mbali ya sababu hizo, mawaziri hao waliozungumza na gazeti hili kwa nyakati tofauti wanadai kuwa mbinu hiyo ya kuongozana na Kinana kwa upande wao haiwajengi kisiasa zaidi ya kuwaharibia.

Baadhi wanaona kwamba mbinu hiyo haitawasaidia kisiasa, hasa katika majimbo yao, kutokana na kero nyingi zinazowakabili wananchi wao, huku wapinzani wakizitumia kama mtaji wa kisiasa hali ambayo imesababisha kuzomewa mara kwa mara.

"Kwa mfano mimi katika jimbo langu, hata uchaguzi wa 2010 nilinusurika tu, kuna mambo mengi hatujafanya, wananchi wana kero ya maji, dawa, miundombinu, huku wapinzani wanapita wanasema sisi ni mafisadi, sasa leo hii nikipanda jukwaani hata kama niko Mtwara wananchi wangu si lazima watasikia nimezomewa.

"Siku nikirudi jimboni kwangu si nitazomewa mara mbili?…Sasa kipi bora, nikazomewe au nibaki niendelee na kazi zangu wizarani?…Nikishindwa bora niende kwa wananchi wangu mimi kama mimi," alisema mmoja wa mawaziri hao.

Aidha, mmoja wa mawaziri ambao inasemekana kwamba alikwepa kuongozana na Kinana pamoja na viongozi wengine wa chama wakati wa ziara ya hivi karibuni jijini Arusha, alisema yeye hakwenda kwa sababu alibanwa na kazi wizarani.

Waziri huyo ambaye hakutaka jina lake liandikwe gazetini, alisema wanaosema kwamba alikwepa ni waongo na kusisitiza kuwa atakapotakiwa kufanya hivyo, atafanya kama atakuwa hajabanwa na majukumu kazini kwake.

"Mimi sio kama wengine, mimi jimboni kwangu sina matatizo makubwa…hata 2010 nilipita bila upinzani mkali…sasa leo niogope nini?...Nitakapotakiwa na chama changu nitakwenda, ingawa na mimi nimesikia baadhi yetu wanalalamika…lakini na wananchi nao waelewe kwamba sisi tunafanya kazi, wasibakie kuzomea," alisema waziri huyo.

Mawaziri waliokumbwa na dhahama ya kuzomewa ni Christopher Chiza wa Kilimo, Chakula na Ushirika, Hawa Ghasia (Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa - Tamisemi) na naibu wake, Aggrey Mwanri..

Hoja ya mawaziri hao kwamba, mbinu hiyo haiwasaidii kisiasa, hasa katika majimbo wanayotoka ilidhihirika pale Ghasia ambaye pia ni Mbunge wa Mtwara Vijijini alipozomewa wakati wakiwa katika ziara ya mkoani Mtwara.

Kuzomewa kwa Ghasia kulikuja baada ya mwananchi mmoja kumshutumu yeye na Mbunge wa Mtwara Mjini, Asnein Murji kwamba waliruhusu gesi kupelekwa Dar es Salaam wakati wananchi wa mkoa huo hawajafaidika nayo.

Pamoja na hilo, kuna habari kwamba CCM hivi sasa inaangalia namna bora ya kuwatumia mawaziri hao kutokana na kile kinachoonekana kuwa mkakati wa kuwatumia umegonga mwamba hasa kutokana na zomezomea zilizowakumba.

Alipotafutwa Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC), Itikadi na Uenezi CCM, Nape Nnauye, kuzungumzia taarifa hizo, alisema hawezi kuzungumza mpaka awafahamu hao wanaolalamika.

Alipoulizwa kama utaratibu wa kuambatana na mawaziri ni wa chama au ni wa serikali, Nape pia alikataa kujibu swali hilo akisema: "acheni fitna zisizo na msingi."

Hata hivyo Nape baadae alizungumza na gazeti hili akisema kuwa ziara hizo ni utaratibu wa chama kufuatilia maendeleo ya utekelezaji wa ilani.

Katika maelezo yake, alisema kuwa baadhi ya mawaziri waliozomewa Mtwara waliomba wenyewe kuongozana kwenye mikutano ya Kinana kwenda kujibu kero zinazowakabili wananchi.

Aliwataja mawaziri hao kuwa ni Ghasia na Chiza ambao alisema kuwa waliwakuta huko huko Mtwara.

Nape alisema kuwa walilazimika kumuomba Mwanri kwa ajili ya kwenda kujibu hoja za masuala mbalimbali ya mitaa.

Alisema kwa upande wake anaamini kuwa, watu wanaofikiri hivyo lengo lao ni kuvuruga baada ya kuona mafaniko ya CCM yaliyopatikana kutokana na ziara hizo.

Septemba mwaka huu, Waziri Mkuu, Mizengo Pinda kwa mara ya kwanza naye alikumbana na kadhia hiyo ya kuzomewa kwenye mkutano wa hadhara jijini Mwanza, kisha msafara wake kupopolewa mawe.

Pinda alikaririwa akisema kuwa kitendo hicho kimemtisha na kusema upo uwezekano mkubwa wa viongozi wengine wa kitaifa kuanza kukumbana na hali hiyo, na kusema kuwa lazima kero zinazowasibu wananchi zitatuliwe kwani hali hiyo siyo nzuri kutokea kwa kiongozi wa taifa kama yeye.

Mbali ya Pinda, itakumbukwa kuwa hali hii ya zomea zomea pia iliwahi kuwakumba mawaziri mwaka 2007 wakati walipoamua kupita katika mikoa mbalimbali nchini kutetea bajeti.

Mawaziri hao pamoja kutumia kiasi cha shilingi bilioni 2.5 kutetea bajeti hiyo ambayo ilikosolewa vikali na wabunge wa upinzani kuwa haimsadii mwananchi wa kawaida, lakini bado walishindwa kuzima munkari wao.

Hivi karibuni, CHADEMA kupitia kwa Katibu Mkuu wake, Dk. Willibrod Slaa ilisema kuwa mpango wa viongozi wa CCM wakiwamo mawaziri kuanza ziara mikoani, hauwezi kukisaidia chama hicho kujiimarisha kisiasa wala kuathiri kasi yao ya kujipanua nchi nzima.

Chama hicho kilisema CCM hawatafanikiwa kwa kuwa zimejitokeza tuhuma nzito ambazo hazijajibiwa na serikali yake kwa Watanzania, hivyo kuwafanya wananchi kukosa imani nayo.

 
Nduka

Nduka

JF-Expert Member
Joined
Dec 3, 2008
Messages
8,523
Points
2,000
Nduka

Nduka

JF-Expert Member
Joined Dec 3, 2008
8,523 2,000
Kiwanda cha Mbowe kimetoa bidhaa mpya. Kazi kwenu makamanda.
 
Nyasirori

Nyasirori

JF-Expert Member
Joined
May 3, 2009
Messages
297
Points
500
Nyasirori

Nyasirori

JF-Expert Member
Joined May 3, 2009
297 500
Hii ndiyo sababu ya kuhitaji kuwa na mawaziri wataalamu katika nyanja watakazopewa na si wanasiasa wanaotokana na ubunge.
 
50thebe

50thebe

JF-Expert Member
Joined
Mar 10, 2011
Messages
2,227
Points
2,000
50thebe

50thebe

JF-Expert Member
Joined Mar 10, 2011
2,227 2,000
"Kwa mfano mimi katika jimbo langu, hata uchaguzi wa 2010 nilinusurika tu, kuna mambo mengi hatujafanya, wananchi wana kero ya maji, dawa, miundombinu, huku wapinzani wanapita wanasema sisi ni mafisadi, sasa leo hii nikipanda jukwaani hata kama niko Mtwara wananchi wangu si lazima watasikia nimezomewa.

"Siku nikirudi jimboni kwangu si nitazomewa mara mbili?…Sasa kipi bora, nikazomewe au nibaki niendelee na kazi zangu wizarani?…Nikishindwa bora niende kwa wananchi wangu mimi kama mimi,"
alisema mmoja wa mawaziri hao.

Hapo kwenye nyekundu jamaa kaharibu kabisa, Ndio kusema mpango huu wa CCM kujinadi kwa wananchi kupitia mawaziri wa serikali tayari ushakwama, tena unapingwa toka ndani kwenyewe...Bila shaka CHADEMA inahusika hapa.
 
THE GREAT CAMP

THE GREAT CAMP

JF-Expert Member
Joined
Jun 29, 2012
Messages
766
Points
0
THE GREAT CAMP

THE GREAT CAMP

JF-Expert Member
Joined Jun 29, 2012
766 0
Badilisha heading yako.Haiendani na ulichoandika ndani. Mimi nilidhani jamaa(Kinana) kuna maudhi kayafanya kwa hao mawaziri. Kumbe ni wananchi kuzomea na kupopowa mawe?. Hao mawaziri wanavuna walichopanda, huo ndiyo ukweli wenyewe.Tena mimi nadhani wanavyozunguka na kinana ndiyo wanapata picha halisi ya watanzania walivyo sasa siyo kusubiri masimulizi ya uongo ofisini.That's what going on the ground. Kama wangekuwa wamefanya mambo mazuri kwa wa TZ kuzomewa na kupigwa mawe kungetoka wapi?
 
ROBERT MICHAEL

ROBERT MICHAEL

JF-Expert Member
Joined
Oct 23, 2012
Messages
4,912
Points
2,000
ROBERT MICHAEL

ROBERT MICHAEL

JF-Expert Member
Joined Oct 23, 2012
4,912 2,000
ukweli unajulikana, vitu vinaonekana wazi hakuna chochote kilichofanyika huko, juzi tu nimetoka mkoa wa lindi , wananchi wengi kule hawataki stakabadhi ghalani maana wanakopwa, kingine kilichonishtua nikiwa liwale mbunge wao kule analaumu wananchi wao kuhusu kuwachagua viongozi wao wa vyama vya ushirika kwa hyo yy hayupo kwenye lawama ya wanachi kukopwa korosho zao. hao hao viongozi wa vyama vya ushirika wengine madiwani wao CCM.
 
M

MpendaTz

JF-Expert Member
Joined
May 15, 2009
Messages
1,721
Points
1,250
M

MpendaTz

JF-Expert Member
Joined May 15, 2009
1,721 1,250
[/LEFT]
Hapo kwenye nyekundu jamaa kaharibu kabisa, Ndio kusema mpango huu wa CCM kujinadi kwa wananchi kupitia mawaziri wa serikali tayari ushakwama, tena unapingwa toka ndani kwenyewe...Bila shaka CHADEMA inahusika hapa.
Alaa! Sasa hivi kila kitu kinachoenda ovyo nchini kinasababishwa na CHADEMA?
 
Ronal Reagan

Ronal Reagan

JF-Expert Member
Joined
Nov 4, 2010
Messages
4,834
Points
2,000
Ronal Reagan

Ronal Reagan

JF-Expert Member
Joined Nov 4, 2010
4,834 2,000
Hakuna waziri mzalendo hapo. Kwa nini hawaoni huruma kutafuna kodi za wananchi kwa faida zao kichama?
Ningemheshimu waziri yeyote ambaye angesema anapinga kufanya hivyo kwa sababu ya utumiaji mbaya wa rasilimali muda na fedha (ambavyo ni vya umma).
 
Ryaro wa Ryaro

Ryaro wa Ryaro

JF-Expert Member
Joined
Oct 4, 2010
Messages
2,661
Points
1,225
Ryaro wa Ryaro

Ryaro wa Ryaro

JF-Expert Member
Joined Oct 4, 2010
2,661 1,225
Hii inaweza kuwa ni kweli "JK alishaweka wazi kuwa shida yake ilikuwa awe rais tu basi, lakini sio kuumiza kichwa na shughuli za urais " ndio maana yeye kwa sasa hapati kuangaika na kero zinazowakabiri Wabongo.
 
50thebe

50thebe

JF-Expert Member
Joined
Mar 10, 2011
Messages
2,227
Points
2,000
50thebe

50thebe

JF-Expert Member
Joined Mar 10, 2011
2,227 2,000
Alaa! Sasa hivi kila kitu kinachoenda ovyo nchini kinasababishwa na CHADEMA?
Hukuona Mwenyekiti Kikwete povu lilivyomtoka juzikati kule Dodoma kwenye mkutano mkuu wa CCM? kama hukuona, hata simulizi hukupata? Chadema kuhusika kwenye hizi mambo ndio kauli mbiu ya chama twawala siku hizi.
 
englibertm

englibertm

JF-Expert Member
Joined
May 1, 2009
Messages
9,253
Points
2,000
englibertm

englibertm

JF-Expert Member
Joined May 1, 2009
9,253 2,000
ukitaka uchukiwe na watu uwe mkweli
 
N

ndandawamalenja

JF-Expert Member
Joined
Nov 1, 2012
Messages
372
Points
0
N

ndandawamalenja

JF-Expert Member
Joined Nov 1, 2012
372 0
Magamba hawana cha kuwaambia wananchi, ndio maana mawaziri wao wanazomewa. Mawaziri wachache sana wanaoweza kusimama kifua mbele na wasizomewe. Mfano Jembe Pombe Magufuli (tumembadilisha jina)
 
Grand Master Dulla

Grand Master Dulla

JF-Expert Member
Joined
Jul 20, 2012
Messages
392
Points
225
Grand Master Dulla

Grand Master Dulla

JF-Expert Member
Joined Jul 20, 2012
392 225
magamba wamekwisha.
 
Omutwale

Omutwale

JF-Expert Member
Joined
Feb 4, 2008
Messages
1,432
Points
1,250
Omutwale

Omutwale

JF-Expert Member
Joined Feb 4, 2008
1,432 1,250
mcfm40

mcfm40

JF-Expert Member
Joined
Nov 2, 2010
Messages
4,337
Points
2,000
mcfm40

mcfm40

JF-Expert Member
Joined Nov 2, 2010
4,337 2,000
Kwa hiyo Chadema ikiwa kwisheny ndio maisha bora yatapatikana kwa kila mtanzania? Chadema ndio inawazuia kuwaleteta watanzania maendeleo?

CDM kwishney sasa hivi propagander inapigwa from within
 
BADILI TABIA

BADILI TABIA

JF-Expert Member
Joined
Jun 13, 2011
Messages
31,232
Points
2,000
BADILI TABIA

BADILI TABIA

JF-Expert Member
Joined Jun 13, 2011
31,232 2,000
kinana mzee wa meno ya tembo hana dili
 

Forum statistics

Threads 1,403,288
Members 531,177
Posts 34,419,811
Top