Kinana asubiriwa kwa hamu na wananchi mkoani mbeya.

Domy

JF-Expert Member
Dec 12, 2011
4,700
1,086
Wanabodi

Wananchi mkoani mbeya na hasa jijini mbeya na wilaya za mbozi,momba,tukuyu na kyela wamehamasika sana baada ya kutangazwa jina la ndugu kinana kuwa katibu mkuu wa CCM.Mazungumzo mengi ya wananchi wa mkoa huu ni kuhusu ziara zinazoendelea za ndugu kinana mikoani.

Wananchi wa mbeya wana hamu katibu mkuu huyo wa CCM atembelee mkoa huu ili kujionea hali halisi ya mkoa huu kisiasa ambapo CCM ilishakufa kabisa katika maeneo ya wilaya nilizotaja na kuja kumuonyesha kwamba uteuzi wake kuwa katibu mkuu hauwezi kufufua matumaini ya wanaCCM wa mkoa huu wa Mbeya mkoa ambao wananchi wake karibu asilimia 90 ni wanamabadiliko.

Vile vile wananchi wa mkoa huu wana maswali mengi ya kumuuliza ndugu Kinana kuhusiana na tuhuma juu yake kwamba anajihusisha na ujangili.ushahidi wa tuhuma hizo ni pamoja na meno ya tembo yaliyokamatwa Hong kong yakiwa kwenye meli anayoimiliki.

Wananchi wa mkoa huu wamechukizwa sana na jinsi viongozi wa CCM wanavyoendelea kuitafuna nchi hii baada ya kashfa za ufisadi za Richmond,meremeta,kagoda,deep green(EPA) Kutofanyiwa chochote na sasa hii ya Ujangili wa kutisha ikiwemo kutorosha wanyama hai.hivyo ndivyo ndugu kinana anavyosubiriwa mkoani hapa.

Nawasilisha!
 
asisahau kuvaa helmet maana ABHANAFYALE wale ni balaa
hawachelewi kumpopoa..amuulize USTADH JK na sheikh NAHODHA
Jamaa wale hawatakakgi ujinga ujinga wala hawataki masihala wanataka ukweli na ndo maana ni wawazi sana na wachapa kazi sana kama DR MWAKYEMBE,PROF.MWANDOSYA,muingereza PHILIPO MULUGO,GODFREY ZAMBI
 
Umemsahau first lady alirushiwa makopo ya maji mwanjelwa na kurushiwa mawe tunduma.
 
asisahau kuvaa helmet maana ABHANAFYALE wale ni balaa
hawachelewi kumpopoa..amuulize USTADH JK na sheikh NAHODHA
Jamaa wale hawatakakgi ujinga ujinga wala hawataki masihala wanataka ukweli na ndo maana ni wawazi sana na wachapa kazi sana kama DR MWAKYEMBE,PROF.MWANDOSYA,muingereza PHILIPO MULUGO,GODFREY ZAMBI
Umemsahau Le General SUGU!!!
 
Mmekosa la kusema, mmeanzisha uzushi kuhusu ujangili na bla bla nyingi. Nakwambia magwana hakuna rangi mtakosa kuiona. Na sasa mnapandikiza watu wa kuzomea na kupopoa mawe. you will be treated accordingly like any other criminals.
 
Aibu mnaajiri watu kwa ajili ya kuzomea kweli mmekosa kazi siasa haziendi hivyo nieleleze mbeya kuna majimbo mangapi na nyie mmeshinda mangapi na ni asilimia ngapi mbona hata asiyeenda shule hamuwezi kumdanganya.
 
Mbunge kama Mulugo unaweza kujivunia,Uchawi ndio kazi yenu kubwa, na sasa tumeshajua pesa za kununua majimbo mnakozitoa hili la ujangiri tulikuwa hatujajua sasa mtaisoma namba mwaka 2015.
 
Aibu mnaajiri watu kwa ajili ya kuzomea kweli mmekosa kazi siasa haziendi hivyo nieleleze mbeya kuna majimbo mangapi na nyie mmeshinda mangapi na ni asilimia ngapi mbona hata asiyeenda shule hamuwezi kumdanganya.

We vipi? kuna mbunge ccm aliyeshinda au unaongelea wizi wa kula kuhonga vibibi tsheti na pombe. Haukua uchaguzi bali uchafuzi.
 
Wanabodi

Wananchi mkoani mbeya na hasa jijini mbeya na wilaya za mbozi,momba,tukuyu na kyela wamehamasika sana baada ya kutangazwa jina la ndugu kinana kuwa katibu mkuu wa CCM.Mazungumzo mengi ya wananchi wa mkoa huu ni kuhusu ziara zinazoendelea za ndugu kinana mikoani.

Wananchi wa mbeya wana hamu katibu mkuu huyo wa CCM atembelee mkoa huu ili kujionea hali halisi ya mkoa huu kisiasa ambapo CCM ilishakufa kabisa katika maeneo ya wilaya nilizotaja na kuja kumuonyesha kwamba uteuzi wake kuwa katibu mkuu hauwezi kufufua matumaini ya wanaCCM wa mkoa huu wa Mbeya mkoa ambao wananchi wake karibu asilimia 90 ni wanamabadiliko.

Vile vile wananchi wa mkoa huu wana maswali mengi ya kumuuliza ndugu Kinana kuhusiana na tuhuma juu yake kwamba anajihusisha na ujangili.ushahidi wa tuhuma hizo ni pamoja na meno ya tembo yaliyokamatwa Hong kong yakiwa kwenye meli anayoimiliki.

Wananchi wa mkoa huu wamechukizwa sana na jinsi viongozi wa CCM wanavyoendelea kuitafuna nchi hii baada ya kashfa za ufisadi za Richmond,meremeta,kagoda,deep green(EPA) Kutofanyiwa chochote na sasa hii ya Ujangili wa kutisha ikiwemo kutorosha wanyama hai.hivyo ndivyo ndugu kinana anavyosubiriwa mkoani hapa.

Nawasilisha!

Wasomi kwa uhalamia sawa na uji kwa mgonjwa, hukumbuki jinsi mbaula(FIAT) walivyokuwa wanauwawa matingo kisa mgao.
 
mbaya zaidi walipomteua Katibu mkuu hawakujua kama siri itafichuka,China ni nouma wametuonyesha njia watanzania!!!!
 
Back
Top Bottom