Domy
JF-Expert Member
- Dec 12, 2011
- 4,700
- 1,086
Wanabodi
Wananchi mkoani mbeya na hasa jijini mbeya na wilaya za mbozi,momba,tukuyu na kyela wamehamasika sana baada ya kutangazwa jina la ndugu kinana kuwa katibu mkuu wa CCM.Mazungumzo mengi ya wananchi wa mkoa huu ni kuhusu ziara zinazoendelea za ndugu kinana mikoani.
Wananchi wa mbeya wana hamu katibu mkuu huyo wa CCM atembelee mkoa huu ili kujionea hali halisi ya mkoa huu kisiasa ambapo CCM ilishakufa kabisa katika maeneo ya wilaya nilizotaja na kuja kumuonyesha kwamba uteuzi wake kuwa katibu mkuu hauwezi kufufua matumaini ya wanaCCM wa mkoa huu wa Mbeya mkoa ambao wananchi wake karibu asilimia 90 ni wanamabadiliko.
Vile vile wananchi wa mkoa huu wana maswali mengi ya kumuuliza ndugu Kinana kuhusiana na tuhuma juu yake kwamba anajihusisha na ujangili.ushahidi wa tuhuma hizo ni pamoja na meno ya tembo yaliyokamatwa Hong kong yakiwa kwenye meli anayoimiliki.
Wananchi wa mkoa huu wamechukizwa sana na jinsi viongozi wa CCM wanavyoendelea kuitafuna nchi hii baada ya kashfa za ufisadi za Richmond,meremeta,kagoda,deep green(EPA) Kutofanyiwa chochote na sasa hii ya Ujangili wa kutisha ikiwemo kutorosha wanyama hai.hivyo ndivyo ndugu kinana anavyosubiriwa mkoani hapa.
Nawasilisha!