Kinana aonja joto la urais; baada ya kubanwa na wafuasi wa chama juu ya kupata mgombea urais 2015

nngu007

JF-Expert Member
Aug 2, 2010
15,862
5,797
Ijumaa, Novemba 23, 2012 04:38 Na Bakari Kimwanga, Rukwa


*Ni baada ya kubanwa na wana CCM Sumbawanga
*Wasema wasipoteua mtu makini wapinzani watatamba
*Yeye awaondoa wasiwasi, ataka wadumishe mshikamano


KATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Abdulrahman Kinana, kwa mara ya kwanza jana alionja joto la jiwe, baada ya kubanwa kikamilifu na wafuasi wa chama juu ya kupata mgombea urasi mwaka 2015.

Hatua hiyo, inatokana na Kinana kutoa ruhusa ya wananchi kumuuliza maswali kabla ya kuanza kuwahutubia.

Wafuasi hao, walisema kama CCM itateua mtu ambaye hakubaliki ndani ya chama na jamii, basi itawawia vigumu kumnadi mbele ya vyama vya upinzani.

Akizungumza kwa niaba ya wanachama katika kikao cha ndani kilichofanyika katika Kijiji cha Isesa, Peter Lilata, alisema umefika wakati wa chama chao kuteua mgombea ambaye hana makundi wala mbinafsi mbele ya Watanzania.

Hoja hiyo ilionekana kuungwa mkono na wanachama hao, ambao walilipuka kwa shangwe mbele ya Kinana.

"Mheshimiwa Katibu Mkuu, kwa kuwa umekuja hapa leo (jana), kwa lengo la kuimarisha chama chetu… kilio chetu kikubwa kwa chama ni uteuzi wa mgombea wa urais mwaka 2015.

"Tunahitaji mgombea ambaye hatakuwa mzigo kwa chama na wananchi kwa ujumla… tunahitaji kujua namna ambavyo mnaweza kumpata mgombea ambaye hana makundi na mwadilifu kwa jamii," alisema Lilata, huku akishangiliwa.

Akijibu hoja za mwanachama huyo, Kinana aliwahakikishia wana CCM kuwa wakati ukifika watachagua mgombea urais mzuri ambaye anakubalika kwa kila mtu.

Alisema suala la uteuzi wa mgombea mwenye sifa, limekuwa ni kilio kwa wanachama wa CCM nchi nzima.

"Nimewasikia wanachama wetu, ninyi wa hapa pamoja na maeneo mengine, kilio cha wanachama wetu wengi wanataka tuchague mgombea anayekubalika, asiye na makundi, maana atakuwa na upendeleo, tuchague mtu safi, mzalendo, anayejali maslahi ya watu.

"Asiye na ubinafsi na mwadilifu. Haya si maoni yangu, ni msimamo wa chama na kupitia mkutano mkuu wa nane uliomalizika hivi karibuni pale Dodoma… jambo hili limeangaliwa kwa makini katika maazimio yetu.

"Kubwa ambalo nataka lifahamike wazi, ni kwamba chama kina utaratibu wake katika kufanya uteuzi wa mgombea wa urais.

"Wanachama wote ambao wanataka kuwania nafasi hiyo, watachukua fomu, baada ya hapo utaratibu wa kuwahoji kwa sifa zao itafanyika.

"Kisha chama kuamua nani asimame kwa ajili ya kuwakilisha chama chetu. Kwa bahati nzuri wapo wenye sifa za kutosha na chama kitaamua," alisema Kinana.

Pamoja na mambo mengine, Kinana aliweka wazi kuwa Aprili, mwaka 2015, ndiyo wakati ambao chama kitakuwa na wakati mzuri na sahihi kupata mgombea.

Alisema dhamira ya CCM ni kuhakikisha wanakwenda kwa wanachama wao kuanzia ngazi za chini.

"Tunahitaji kiongozi ambaye atahimili kasi yetu, atakuwa mstari wa mbele kutembelea wanachama na wananchi wote kwa ujumla kwa lengo la kusikiliza kero zao popote pale walipo. "Kubwa zaidi sitakuwa tayari kuona tunakuwa na kiongozi asiyejua wajibu wake…tunapima kwa utendaji na ikiwa kuna kiongozi asiyeza kwenda na kasi ya CCM, ni vema atupishe kabla ya kumtimua," alisema Kinana.

Akizungumzia suala la pembejeo za kilimo na mbolea, Kinana alimtaka Mkuu wa Mkoa wa Rukwa, Mhandisi Stella Manyanya, kutoa ufafanuzi kwa wananchi.

Pia ameitaka Serikali ya Mkoa wa Rukwa, kuhakikisha inatafuta suluhu ya shamba la Efatha kutokana na kuwepo kwa malalamiko ya wananchi kuhusu eneo hilo ambalo linadaiwa kupewa mwekezaji.

Akijibu hoja ya mbolea na pembejeo, RC Manyanya alisema juhudi zinafanyika ili kuhakikisha wananchi wanapata pembejeo kwa wakati.

Alisema tume iliyoundwa kuchunguza mgogoro wa ardhi katika eneo la Isesa, dhidi ya mashamba ya Efatha, ripoti yake imekamilika na wakati wowote itatolewa mbele ya wananchi kwa hatua zaidi.



"Nimejifunza mengi kuhusu mgogoro wa shamba la Efatha, ambalo wananchi walikuwa wanalitumia kwa shughuli za kilimo hapo mwanzoni. Ndani ya ripoti inayozungumzia mgogoro huo imefafanuliwa vizuri na tunatarajia itatoa suluhu baada ya kujadiliwa," alisema RC.

Alitumia nafasi hiyo, kutoa kilio chake kwa chama kuhakikisha mkoa huo unapatiwa fursa za kuendeleza miradi ya maendeleo ili kukuza uchumi wake.

Rushwa
Akizungumzia suala la rushwa, mizengwe katika uchaguzi, Kinana aliwataka wana CCM kuhakikisha kila uchaguzi wanahangaika kuunga mkono wagombea ambao ni watendaji wazuri na wenye maadili safi, badala ya kukumbatia wanaowapa rushwa.

"Lazima mjue mnapoamua kumchagua mgombea anayewapa rushwa, mnafanya kosa kubwa sana kwenu, maana akishapita anakuwa kiongozi wa kutetea maslahi yake na siyo yenu," alisema Kinana.

Alisema, pamoja na kuwepo viongozi wanaotoa rushwa kutafuta uongozi, lakini wananchi nao wamekuwa chanzo cha kukomaza rushwa kwa sababu mwanachama mwenzao anapojitokeza kuomba uongozi, huwa wa kwanza 'kutengeneza' mazingira ya kumtaka atoe.

Aliwataka kuacha kutungiana fitina, mizengwe na kuachana na makundi kila baada ya chaguzi kwa sababu mambo hayo yanachangia kwa kiasi kikubwa kudhoofisha mshikamano na umoja ndani ya chama.

Katika ziara hiyo, Kinana amefuatana na Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye na Katibu wa NEC, Oganaizesheni, Mohamed Seif Khatib na baadhi ya mawaziri


Mapokezi
Katika mapokezi hayo ya Kinana jana, mji wa Sumbawanga na vitongoji vyake ulitawaliwa na bendera na sare za kijani, huku magari na pikipiki zaidi ya 100 zikimsindikiza katika msafara.

Bendera

Hata hivyo katika hali isiyokuwa ya kawaida, vijana wa CCM na wale wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), nusura wapigane ngumi wakati wa ufunguzi wa tawi la CCM Isesa, baada ya vijana wa CHADEMA kuwatuhumu wenzao kuwa wamewaibia bendera.

Mabishano kuhusu bendera hiyo yaliendelea katika kipindi chote ambacho Kinana alikuwa akizungumza na wanachama wa tawi hilo.
 
hivi kumbe ni kweli ccm inazunguka mikoani kupambania kura za 2015 wakati bado hawajatimiza walau robo ya ahadi walizotoa 2010??
hakika ccm ni sawa na mbwa anayejisaida na kuila haja kubwa aliyojisaidia.

Hatari:
Weka Mbali na Tembo.
 
Wizi MTUPU wa MCHANA... Tangu lini CHAMA kinatoa VIBALI vya MIGODI??
 
Kinana anadhani watanzania ni wajinga, anafanya kama Mkwele kupita mikoani na kutoa ahadi hewa.
Mazezeta wachache wa magamba watamwelewa lakini raia wajanja na wanyonge hawadanganyiki tena.

Poor Kinana, Poor CCM.
 
Back
Top Bottom