Petro E. Mselewa
JF-Expert Member
- Dec 27, 2012
- 10,196
- 25,515
Katibu Mkuu wa CCM,Kanali Mstaafu Abdurahman Kinana anaoongoza timu ya Sekretarieti ya Taifa ya CCM pamoja na viongozi wengine wa kichama kwenye ziara za mikoani.Ziara hizo zinasemwa kuwa ni za kuimarisha chama pamoja na kukagua utekelezaji wa Ilani ya CCM ya 2010-2015.
Tayari Kinana na timu yake wameshapita kwenye mikoa mbalimbali ya Tanzania Bara. Katika mikutano yake, inaripotiwa kuwa Kinana na timu yake wanazungumzia masuala ya maendeleo,Katiba mpya na kadhalika. Inaripotiwa kuwa Kanali Kinana 'anamwaga' ahadi na kukosoa viongozi wa chama chake na Serikali ya chama chake.
Ndiyo maana ninajiuliza,Kinana anapopita anawaachia nini wananchi baada ya mikutano yake ya hadhara? Maendeleo? Hasira kwa viongozi wao wa kitaifa na kichama? Ahadi za kimaendeleo? Elimu juu ya Rasimu ya Katiba mpya?
Tutafakari wana-JF