Kinana anawaachia nini wananchi anaowapita mikoani?

Petro E. Mselewa

Verified Member
Dec 27, 2012
9,484
2,000
Katibu Mkuu wa CCM,Kanali Mstaafu Abdurahman Kinana anaoongoza timu ya Sekretarieti ya Taifa ya CCM pamoja na viongozi wengine wa kichama kwenye ziara za mikoani.Ziara hizo zinasemwa kuwa ni za kuimarisha chama pamoja na kukagua utekelezaji wa Ilani ya CCM ya 2010-2015.

Tayari Kinana na timu yake wameshapita kwenye mikoa mbalimbali ya Tanzania Bara. Katika mikutano yake, inaripotiwa kuwa Kinana na timu yake wanazungumzia masuala ya maendeleo,Katiba mpya na kadhalika. Inaripotiwa kuwa Kanali Kinana 'anamwaga' ahadi na kukosoa viongozi wa chama chake na Serikali ya chama chake.

Ndiyo maana ninajiuliza,Kinana anapopita anawaachia nini wananchi baada ya mikutano yake ya hadhara? Maendeleo? Hasira kwa viongozi wao wa kitaifa na kichama? Ahadi za kimaendeleo? Elimu juu ya Rasimu ya Katiba mpya?

Tutafakari wana-JF
 

Danny Jully

JF-Expert Member
Jul 29, 2013
4,264
2,000
Katibu Mkuu wa CCM,Kanali Mstaafu Abdurahman Kinana anaoongoza timu ya Sekretarieti ya Taifa ya CCM pamoja na viongozi wengine wa kichama kwenye ziara za mikoani.Ziara hizo zinasemwa kuwa ni za kuimarisha chama pamoja na kukagua utekelezaji wa Ilani ya CCM ya 2010-2015.

Tayari Kinana na timu yake wameshapita kwenye mikoa mbalimbali ya Tanzania Bara. Katika mikutano yake, inaripotiwa kuwa Kinana na timu yake wanazungumzia masuala ya maendeleo,Katiba mpya na kadhalika. Inaripotiwa kuwa Kanali Kinana 'anamwaga' ahadi na kukosoa viongozi wa chama chake na Serikali ya chama chake.

Ndiyo maana ninajiuliza,Kinana anapopita anawaachia nini wananchi baada ya mikutano yake ya hadhara? Maendeleo? Hasira kwa viongozi wao wa kitaifa na kichama? Ahadi za kimaendeleo? Elimu juu ya Rasimu ya Katiba mpya?

Tutafakari wana-JF

Ukimsikiliza vizuri Kinana utagundua kwamba kuna mambo yamemchosha na YANAMKERA ndani ya serikali ya CCM. Anataka mabadiliko ambayo ni magumu kuyapata akiwa ndani ya mfumo wa serikali yake. Kwa kifupi anataka kukata tawi ambalo amelikalia. Hataweza ndio maana anaishia kuendelea kutaja mawaziri mizigo!!!
 

makubazi

JF-Expert Member
Feb 15, 2013
2,048
1,195
Ooyooo halloo nahau mwenye macho haambiwi tazama na mwenye masikio haambiwi sikia hiyo ziara ni ya longo longo na domo tuu na haya tushayasikia toka awamu ya kwanza hadi laana ya leo ni hizo kwa hizo na wala hazina manufaa au tija ni uharibifu tuu wa mapato ya kodi za wananchi tena hata huruma hawana na wala hakuna msaada wowote hata kuwatupia kidogo mpunga wa kumi kumi lakini cha kuushangaza hiyo ziara ya kisanii ni gharama kubwa tena sana na mgao wao huwa mnono bab kubwa sana na ya kutisha huo mpunga wao
 

Elly B

JF-Expert Member
Jan 11, 2011
1,194
1,195
Ukimsikiliza vizuri Kinana utagundua kwamba kuna mambo yamemchosha na YANAMKERA ndani ya serikali ya CCM. Anataka mabadiliko ambayo ni magumu kuyapata akiwa ndani ya mfumo wa serikali yake. Kwa kifupi anataka kukata tawi ambalo amekikalia. Hataweza ndio maana anaishia kuendelea kutaja mawaziri mizigo!!!

Sidhani kama sura na maneno ya mtu aliyechoshwa na tabia flani flani za chama chake kama vinafanana na Kinana na Timu yake anayoandamana nayo. Nasema hayo kwa sababu nyingi lakini ni wazi:

1. Mtu ambaye yuko serious na amechoka, hawezi kupeleka ujumbe wake akiwa mefuatana na watu wasio makini kama Nape. Hiyo ni dalili tosha kwamba hata yeye hayuko serious.

2. Mtu aliyechoshwa na mwenye akili timamau hawezi kuwa hajajua kwamba katiba sahihi ni suluhisho la matatizo mengi tunayoyaona katika hii nchini. Laiti katiba ya 77 ingetoa mwongozo wa kuwajibisha viongozi wapuuzi na wezi! Sidhani kama mpaka sasa tungekuwa na majinamizi ya Ufisadi wa EPA, RADA, MEREMETA, na mengine ya aina hiyo, Laiti kama katiba ingehakikisha mamlaka ya rais yana mipaka! Sidhani kama tungeongelea migongano ya kiuongozi inayosababisha uzembe wa wabunge na bunge. Lakini leo anakuja mtu anatuambia katiba siyo mwaobaini wa matatizo ya wananchi!

3. Mtu aliyechoshwa na mambo ya chama, hangepita mitaani kunyoosha vidole kwa watendaji wa serikali yake, wakati yeye ni katibu mkuu, Mtendaji mkuu wa chama chake na ni mtu wa karibu na mwenyekiti ambaye ndiye anayeteua hao anaowanyooshea vidole. Mi naona huu ni mwendelezo wa yale maigizo ya CCM ya kulalamika kama wapinzani badala ya kuchukua hatua.

Pamoja na yote hayo, kwa anayeona vizuri, ziara za Kinana zinalenga kumsafishia njia mmojawapo wa wale mabwana wenye kambi za urais, huku zikimponda mwingine kienyeji. Lakini upande wa pili hotuba zake za malalamiko zinapelekea kuwajaza ujinga wananchi kuwa hata CCM inasimamia uadilifu, wakati kimsingi imeshindwa vibaya katika upande huo. Ndiyo maana:

i. Wale wote waliokuwa wakituhumiwa kwa ufisadi, ambao Nape na wenzake waliwabatiza majina kama magamba, pamoja na kutoa ukomo wa miezi 3, lakini miaka imepita na hakuna kilichofanyika.

ii. Ikafuata ile ziara ya Nape na swahiba wake huyo, iliyozaa misamiati ya mawaziri, mizigo. Mawaziri ambao tuliahidiwa wameitwa kujieleza NEC na watashughulikiwa. Listi ile bado ilikuwa ya kinafiki kwani bado kuna kina Hawa Ghasia wala hawakutajwa, wakti hakuna walichowahi kufanya na TAMISEMI inaharibu hakuna mfano. Mpaka leo wapo serikalini na sana wengine ndiyo wanazidi kuvurunda.

Nadhani ni vema tu, CCM ikajifunza kuweka priority za matumizi, kwa kufanya mikutano yenye tija, badala ya hii ya sasa ambayo ukiiangalia haina kichwa wala miguu.
 

Simiyu Yetu

JF-Expert Member
Apr 29, 2013
18,939
2,000
Kinana ni kiboko yenu anapiga kazi mtaumwa sana mwaka huu muone kinana anavyofanya kazi.
 

iMad

JF-Expert Member
Aug 4, 2013
1,833
0
Mimi siwapendi ccm..lkn nimeangalia kinana kuna vitu anatamani viwe lkn anashidwa..anatamani labda mawaziri au wafanya kazi wa wizara mfano ya afya wangekuwa wanapiga kambi vijijini na wananchi kutatua matatizo yao kama ni hospitali wakae na wanachi wasimamie ujenzi na ikiwezekana washiriki.kwenye ujenzi..kilimo hivyo hivyo...lkn anashindwa kujua ccm hiyo ni ile ya mwalimu..ya jembe na nyumdi..ccm hii ya watoto wa mjini akina malima,mwigulu, january, riziwan, kigwangwala, lusinde...ni ya kutafuna nchi na kugawana viposho vya buku saba saba na kina ritz na akina msalani na hawa walioibuka siku hizi kutoa matamko feki kuhusu wapinzani(ukawa)
 

Erythrocyte

JF-Expert Member
Nov 6, 2012
77,404
2,000
usisahau pia kwamba huwa ANAMWAGA CHOZI ! bila shaka katika anayowaachia kuna MAJONZI PIA !
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom