Kinana Anatukumbusha Kifo Cha Horace Kolimba

Mwanahabari Huru

JF-Expert Member
Mar 9, 2015
14,243
34,898
Ni miaka kama ishirini hivi imepita,pale aliyekuwa katibu Mkuu wa ccm ndg Horace Kolimba aliposema" ccm imepoteza mwelekeo''

Mameno haya yalimfanya aitwe Chimwaga kuhojiwa, lakini kabla ya kujieleza alipatwa na umauti akafariki.

Kinana juzi wakati anahutubia mkutano wa kuhitimisha ziara zake zilizokula fedha ya chama,alisema mambo mengi,ambayo yanaonesha chama hiki kimeishiwa mbinu!

Mambo hayo ni:

* serikali ya ccm kila siku inasema iko mbioni,mbio hizo zitaisha lini?

* serikali ya ccm wabunge wake ni wa hovyo,wanaunga mkono hoja dhaifu,

* serikali ya ccm imepitisha sheria nyingi zinazowanyanyasa wananchi,

* serikali ya ccm imekuwa ikiwatesa bodaboda sasa mwiko,

* serikali ya ccm, wabunge wake na mawaziri hawajawahi kufanya ziara kumi tu mikoani,

* serikali ya ccm inalea mafisadi!

Wakati akisema hayo!
Mugombea urais kupitia chama hicho alibwaga manyanga kwa kuzitupa chini fomu za kuomba kuteuliwa, baada ya kuchoshwa kuombwa rushwa!

Inashangaza sana.Katibu Mkuu huyu alikuwepo wakati Wabunge wake wakitetea Escrow,alikuwepo wakati ccm ikiwafukuza wafabiaahara wadogowadogo ( machnga) jijini Mbeya,Mwanza na Dar) ,

Alikuwepo wakati wabunge wa ccm wakiunga mkono kuyakanyaga maoni ya Rasmu ya katiba ya warioba huku akiwa Kule morogoro mjini aliwaita wapinzani kuwa wao ni waroho wa madaraka! Hakuona wakati ule anaona sasa!

Najua anatapatapa,Lakini alikuqa pembeni mwa ubavu wa Jk wakati wakiunga mkono hoja hizo,alishindwaje kusimama kwenye vikao vya chama kama shuja kuwaonya na kuzuia ujinga huo? Angefanya hivyo tungemwita shujaa!
Leo anarukumbusha tu kauli za baba wa Taifa;

* serikali dhaifu haikusanyi kodi,itabaki kukimbizana na wauza pipi ba karanga barabarani!

Mwanasiasa dhaifu,anapoishiwa hoja anaweza kujinasibisha kwenye udini au ukabila!

Watanzania wanahitaji,wanahitaji mabadiliko,wasipoyaona ndami ya ccm,watayatafuta nje ya ccm!

Watanzania,ccm imeyumba,imeishiwa utashi wa kulinda afya, elimu na usalama wao,tunaendelea kuwa maskini huku wanaosimama jukwaani wana miaka karibu 21 hawajui Mwananchi anayeishi kijiji cha Lupembe atasomeshaji,atatibiwaje,ataongezaje kipato chake?
Tuwakatae Oktoba!
 
Haya yote yanaimulika serikali legelege ya chama cha mafisadi na hapa walipotufikisha Watanzania tunasema imetosha!!!!!!!

Tunawashukuru!
 
UKAWA huu ndio wakati wetu kuchukua nchi japo tujiandae kwa vita maana magamba hayatokubali kuachia nchi kirahisi kama tunavyodhani.
 
Watanzania bwana kwaiyo unataka tuongozwe na malaika au maana ndio yupo perfect.
 
Nimesha hama Rasmi CCM... niko CDM tokea niliyoyaona Lowassa aliyofanyiwa...

Moyo wangu, ndugu, marafiki na watu wengi Watanzania, wameshindwa kuvumilia uonevu uliofanywa na CCM dhidi ya Lowassa... hatuwezi vumilia tena...Sasa ni wakati wa maamuzi magumu...kwa vitendo

Ni UKAWA tu kura.. tuache maneno, jtatu nitakuwa rasmi na kadi mpya ya CDM...!!!

Dr. Slaa tunakutegemea sasa.... hakuna mwingine
 
Watanzania walishafanya mamuzi sikunyingi sana kuwa ni Dr. Slaa october nikutekeleza tuu
 
Nimesha hama Rasmi CCM... niko CDM tokea niliyoyaona Lowassa aliyofanyiwa...

Moyo wangu, ndugu, marafiki na watu wengi Watanzania, wameshindwa kuvumilia uonevu uliofanywa na CCM dhidi ya Lowassa... hatuwezi vumilia tena...Sasa ni wakati wa maamuzi magumu...kwa vitendo

Ni UKAWA tu kura.. tuache maneno, jtatu nitakuwa rasmi na kadi mpya ya CDM...!!!

Dr. Slaa tunakutegemea sasa.... hakuna mwingine
Wewe ni mtu wa ajabu sana. Yaani unahama chama kwa sababu tu Lowasa kakosa ugombea wa CCM!! Sasa wewe tukuite ni mfuasi wa sera za chama au mfuasi wa mtu mmoja ndani ya chama?
 
mnagawana pesa wakati wananchi hawana dawa mahospitalini ,maisha magumu Hakika oktoba mtatutambua yaani CCM mnatugeuza ss mbuzi wa kushangilia hewa na hatupati kitu miaka yote huku ninyi mkinufaika na familia zenu na kugawana rasilimali za nchi,CCM mtambue haikubaliki ,haikubaliki ,haikubaliki kwa namna yoyote ile.Tuonane oktoba ili tuheshimiane.
 
Back
Top Bottom