Kinana amburuza Msigwa kortini

mawenge

JF-Expert Member
Nov 26, 2012
286
71
KATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Abdul-rahman Kinana amemfungulia kesi Mbunge wa Iringa Mjini, Peter Msigwa (Chadema), kutokana na kumtuhumu anajihusisha na ujangili na biashara haramu ya pembe za ndovu.

Kinana amefungua kesi hiyo katika Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam kutokana na kitendo cha Mbunge huyo kutoa tuhuma hizo dhidi yake kwa nyakati tofauti nje na ndani ya Bunge, pia alikataa kuzikanusha na kumuomba radhi.

Inadaiwa kuwa Aprili 21 mwaka huu Msigwa ambaye ni Waziri Kivuli wa Maliasili na Utalii alitoa tuhuma hizo kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika Shule ya Msingi Mbuguni wilayani Nyamagana mkoani Mwanza.

Aidha alizitoa bungeni wakati akiwasilisha hotuba ya Kambi ya Upinzani katika Makadirio ya Bajeti ya Wizara ya Maliasili na Utalii mwaka 2013/2014. Katika hati ya madai, Kinana anadai kuwa kutokana na tuhuma hizo ameharibiwa tabia yake, uaminifu, hadhi yake kitaaluma na weledi na kumfanya achukiwe na kudharauliwa katika jamii.

Anadai jina lake na heshima ambayo ameijenga kwa muda mrefu, vimeharibiwa na Msigwa kwa nia mbaya, pia kwa tuhuma hizo anazosisitiza kuwa ni za uwongo, licha ya kumsababishia maumivu ya kisaikolojia, pia zimemsababishia hasara ya fedha.

Anadai kuwa kabla ya tuhuma hizo alikuwa katika hatua za mwisho za mchakato wa mazungumzo ya mradi wa ubia wa kilimo cha mboga na mwekezaji kutoka kampuni ya nje, lakini tuhuma hizo zimesababisha kampuni hiyo kuvunja majadiliano hayo.

Kinana anadai kuwa sababu iliyotolewa na kampuni hiyo kuvunja mazungumzo hayo ni kutajwa kwake na mbunge huyo kuwa ni jangili anayejishughulisha na biashara hiyo.

Kwa mujibu wa hati ya madai, Mradi huo ulikuwa na thamani ya Dola za Marekani milioni nne, Hisa za ushiriki wa Kinana zilikuwa ni asilimia 25 katika kipindi cha miaka mitano hivyo anatathmini kuwa amepata hasara ya Sh milioni 350.

Kinana anaiomba Mahakama hiyo imwamuru Msigwa amlipe fidia ya Sh milioni 350 kama hasara rasmi, pamoja na fidia ya maudhi na fidia ya hasara ikiwemo gharama za kesi.

Aidha anaiomba Mahakama imwamuru amlipe riba kwa kiwango kitakachopangwa na Mahakama, tangu tarehe ya hukumu hadi malipo ya mwisho, imwamuru kufuta tuhuma dhidi yake na kumuomba radhi kwa kuchapisha katika magazeti mawili ya Kingereza na mawili ya Kiswahili yanayosambazwa nchini.

Pia Mahakama itoe zuio la kudumu kumzuia Msigwa, au wakala wake kutoa au kuchapisha taarifa zozote za kashfa dhidi yake. Katika hati ya madai amenukuu baadhi ya kauli za Msigwa, ikiwemo "Kinana (naomba waandishi wa habari mnisikie na nyie Usalama wa Taifa mkapeleke habari) hana sifa za kupita barabarani na kuwaambia Watanzania waiamini CCM. Kinana mikono yake si misafi."

"Hata kwenye Nassaco, Shirika la Meli Tanzania kuna harufu ya ufisadi ndani yake; ajibu hoja...Kinana meli zake ndizo zinazohusika kubeba pembe za ndovu nchini. hajajibu hoja hizo! Kwa siku nchi hii tembo 67 wanauawa. Hao ndio wanaokifadhili Chama Cha Mapinduzi, halafu wanakuja eti kuwashawishi Watanzania muwasikilize na kwamba Chama Cha Mapinduzi eti ni kizuri."

".Haya mambo ninayoongea ni hatari kwa sababu haya yote ni majangili ni organized Crime. Ni mtandao wa Kimafia, uko duniani kote, unaweza ukatuua lakini wabunge tumesimama tunawatetea..."


HabariLeo

Akiandika kwenye ukaurasa wake wa FACEBOOK Mbunge wa Iringa Mjini ambaye pia ni waziri kivuli wa wizara ya maliasili na utalii Mh.MCHUNGAJI PETER MSIGWA amesema kuwa amesoma habari ya KINANA kufungua mashtaka dhidi yake baada ya kumtuhumu kujihusisha na ujangili na amesema Jopo la mawakili makini lipo tayari kusimamia hilo.

Zaidi,Soma:

Mchungaji Msigwa akiri kumsingizia Kinana ujangili, amwangukia na kumwomba msamaha - JamiiForums
 
ha ha ha mimi naona kinana hapo ndo amechemka kwa sababu nacho jua jopo la mawakili nguri wa chadema watakuja na ushahidi wa kufa mtu...na kufumua mengi juu ya huyu katibu mkuu wa ccm alafu kitu kingine kumbe alikuwa na mchakato wa kuingiza wazungu wengine tena nchini kulima mboga? nacho waomba chadema na msigwa muda ndo huu wa kuisambaratisha ccm na katibu wake na mengi yawekwe hadhalani ili watanzania tujue huu wizi unafanyweje....
 
Duh! kumbe nyie mkituhumiwa mnaathirika kisaikolojia na inawauma,vp lwakatare wa watu mliyemhusisha na ugaidi mkamsweka mahabusu.......kuweni na haya ccm.....tembo wetu wanakufa kweli na meli zako ndio zinasafirisha meno ya hao tembo pls!Mr Kinana usinichefue eti umeathirika kisaikolojia.
 
Kesi imesha funguliwa baada ya makubaliano ya kikao cha viongozi waandamizi wa ccm ili kudhibiti kashfa inayotishia hadhi ya chama na katibu mkuu wake.Na mtashangazwa namaelekezo ya matokeo ya hii kesi ...
 
Well done kinana,

Hizi sifa za "kitoto" za hawa wabunge wetu lazima ziwatokee puani.

Kinana ni mtu makini sana na kwa muda aliotafakari na wanasheria wake lazima MCHUNGAJI wa chadema atajuta.
 
Tafadhal mzee kinana, kuwa na Huruma maana naona umekusudia kulamba kiinua mgongo chake cha bunge, mil 350 atazinyea wapi hasa ukizingatia Mwakalebela atapewa ubunge wake ulioahirishwa kwa makosa ya kisiasa hapo 2015!
 
Tafadhal mzee kinana, kuwa na Huruma maana naona umekusudia kulamba kiinua mgongo chake cha bunge, mil 350 atazinyea wapi hasa ukizingatia Mwakalebela atapewa ubunge wake ulioahirishwa kwa makosa ya kisiasa hapo 2015!

Alhaji Kinana ni Jangili, Haramia na ni Mwizi
 
5 Reactions
Reply
Back
Top Bottom