Kinana akubali ufisadi unaofanywa na CCM? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kinana akubali ufisadi unaofanywa na CCM?

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Dopas, Sep 24, 2010.

 1. D

  Dopas JF-Expert Member

  #1
  Sep 24, 2010
  Joined: Aug 14, 2010
  Messages: 1,151
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  WanaJF tumesikia habari mbalimbali ambazo zilionesha njama za kifisadi za CCM dhidi ya mali za umma au/na dhidi ya vyama vya upinzani, mfano wa Salma na Ridhiwani-matumizi mabaya ya fedha ya umma-ndege ya serikali.

  Mara nyingi tuhuma hizi alipoambiwa meneja wa kampeni ya CCM Abdulrahaman Kinana aling'aka na hata kulazimika kufoji risiti-jambo ambalo litamgharimu siku si nyingi uchunguzi ukikamilika.

  Nashawishika kusema kuwa Kinana anakiri kwamba tuhuma zote dhidi ya CCM sio 'good news' kwa watanzania.

  Kwa hakika ufasadi wa mali za umma kama wa familia ya JK, mafisadi wengine wa CCM hauwezi kuwa 'good news' kwa watanzania. Pia Mhariri wa gazeti la 'ccm' kuitangazia nchi rais wa awamu ya tano kabla wananchi hawajapiga kura sio 'good news' kwa watanzania. Kwa Ujumla hizo ni mbinu za mafisadi ambao kiongozi wao kwa sasa ni Kinana anayehakikisha mbinu zao hizo zinafanikiwa.

  Soma sehemu ya habari hii toka gazeti la mwananchi, 24/09/2010.


  Meneja kampeni wa CCM, Abdulrahman Kinana jana alikataa kuzungumnzia tuhuma zilizoelekezwa kwa chama hicho akieleza kuwa gazeti hili, halitendi haki kwa CCM.

  "Lakini ninyi (Mwananchi) you never have good news for CCM (hamna habari njema kwa CCM) kila siku mkipiga simu ni habari mbaya, mnaandika habari mbaya tu za CCM, nzuri hamzioni," alihoji.

  "Mara Mama Salma kafanya hivi, mara Ridhwani kafanya vile, why can't you be carrier of good news? Always you carry bad news? (wakati wote ni mabaya tu, hamwezi kuandika mema ya CCM?
  "Tafadhali waulizeni Daily News suala hilo."
   
 2. K

  Keil JF-Expert Member

  #2
  Sep 24, 2010
  Joined: Jul 2, 2007
  Messages: 2,214
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Hiyo editorial ya Daily News inaonekana imewaumiza CCM na ndio maana Kinana ameshindwa kutoa kauli yoyote. Reading between the lines CCM na serikali inaonekana hawajui watafanya nini ili ku-control damage. Hili swala likifika NEC na MCT, Daily News wanaweza kupigwa slap na hivyo CCM watakuwa wamepoteza magazeti ya kutolea propaganda.

  On top of that, International Community wamesoma habari hiyo na inazidi kuiweka CCM mahali pabaya zaidi mbele ya Jumuiya za Kimataifa. CHADEMA wafuate ushauri wa Jaji Makungu (Makamu Mwenyekiti wa NEC) wapeleke malalamiko yao NEC na pia walishitaki gazeti hilo Baraza la Habari (MCT) kwa kuenda kinyume na taaluma ya uandishi wa habari.

  Hata kama mzunguko wa gazeti hilo ni mdogo sana, mimi nataka nione NEC watafanya nini. Ku-lodge malalamiko NEC kunaweza kufanya na mtu yeyote wa CHADEMA bila kuathiri Kampeni za CHADEMA.
   
 3. M

  Mutu JF-Expert Member

  #3
  Sep 24, 2010
  Joined: Mar 30, 2008
  Messages: 1,333
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Sasa dailynew ndio wa kuuliza na vyombo vingine vya habari?
   
 4. pascaldaudi

  pascaldaudi JF-Expert Member

  #4
  Sep 24, 2010
  Joined: Mar 25, 2009
  Messages: 534
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Kachemkaaaaaaaaaaaaaaa kinana, kwani DAILYNEWS ni gazeti la CCM??????????????????????????, au ni la sisiemu hatufahamu?
   
 5. IsayaMwita

  IsayaMwita JF-Expert Member

  #5
  Sep 24, 2010
  Joined: Mar 9, 2008
  Messages: 1,123
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Mzee Kinana anajua hali ilivyokuwa ngumu, natambua ni jinsi gani asivyolala, akili yake umwambia, hebu hawa CHADEMA wakishinda mimi Kinana nitakwenda wapi? kisha hujifariji tutafanya lolote lile.

  Mzee Kinana asisahau kuwa huko ndipo tulipo na sasa tunataka kuwapa watanzania haki yao.
   
 6. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #6
  Sep 24, 2010
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  ndio maana yake --- Daily News ndio kampeni meneja wa CCM and Kinana confirmed it

  Duh
   
Loading...