Kinana akomalie mabadiliko ya Kifikra CCM

Peter Stephano 809

Senior Member
Feb 29, 2020
120
162
Makamu mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi, CCM Abdulahman Kinana amewataka wanachama wa chama hicho kubadilika kuacha tabia ya kutukuza Viongozi Wakuu kwa nia ya kusaka nafasi za uongozi.

Kinana ameyasema hayo wakati akikaribishwa katika mkoa wa Dar es Salaam ikiwa ni siku chache tangu achaguliwe katika nafasi hiyo.

"Vyeo havipaswi kutufanya tujitukuze, hivi karibuni kumetokea utamaduni wa kutukuza viongozi, hili sio sawa" amesema Kinana.

Aidha amesema kiongozi akifanya kazi nzuri ndiyo itamtukuza kwa wananchi.
Kauli hii imetolewa ikiwa ni muendelezo ambapo tangu achaguliwe amekuwa akisisitiza kufanya mabadiliko ndani ya chama ili kuchochea demokrasia, haki na uwajibikaji.

Kila jambo analolisema linaweza kuwa kipaumbele kwa sasa kulingana na mwenendo wa chama cha mapinduzi lakini hili la kubadilisha fikra za wananchama linaonekana kuwa na uhitaji mkubwa kuanza nalo.

Sio jambo la kificho kuwa tangu 2015 CCM imekuwa na kawaida ya kulea wanachama wenye fikra potofu Kuuelekea uongozi hasa katika kusaka nafasi ya kuteuliwa na kuchaguliwa.

Kama alivyosema Makamu Mwenyekiti kuwa kumekuwa na dhana ya kutukuza Viongozi ili kupata nafasi.

Katika kipindi chote cha miaka sita iliyopita vijana waliojitokeza kumsifu na kumtukuza Rais pamoja na Viongozi wa juu ndio waliopewa nafasi ya uongozi na fursa nyingine kibao.

Hatuhitaji kutumia ushahidi mkubwa kwa kuwataja hao watu kwani hata Kinana anamkumbuka vizuri Ali Happi na anamfahamu vizuri kiongozi wake wa UVCCM Kenani Kihongosi.

Mwenendo wa Vijana hawa ulionekana haufai mbele ya watu walio wengi akiwemo Kinana mwenyewe lakini ndio walikuwa wanapewa nafasi na viongozi wa juu wa serikali.

Utamaduni huu wa kutukuza viongozi wakuu ndio uliompa jeuri Sabaya sasa anakaribia kutupwa Lupango mara mbili kwa kutumia vibaya madaraka ili kumfurahisha mkuu wake wa kazi.

Dhana hii ya kutukuza ndio iliyowaibua akina Kangi Lugola waliojaribu kumfananisha Rais na Yesu jambo ambalo ni kufuru katika imani ya kikristo.

Kwahiyo kama kinana amelijua hili jambo mapema anapaswa kulikomalia kwa sababu hata yeye ni mhanga ambaye aliwahi kutamkwa wazi kuwa ni miongoni mwa viongozi wastaafu wanaopaswa kushughulikiwa enzi hizo.

Ni wakati sasa wa kubadili fikra za wanaCCM kuhusu mambo mbalimbali hasa hili la uongozi.

WanaCCM watambue kuwa kupewa fursa ya kuteuliwa au kuchaguliwa ni haki ya kila mtu wala sio mapenzi ya kiongozi mkuu pekee.

Hivyo kuacha kujipendekeza na kutukuza viongozi wakuu isivyofaa.

Si hayo tu kinana anapaswa kuhimiza WanaCCM kutambua umuhimu wa ujenzi imara wa sera, hoja na itikadi kwa maendeleo endelevu ya taifa na sio utashi wa viongozi wachache wa juu.

Pia CCM irudi katika mfumo rasmi wa kuwapata viongozi na kuachana na huu wa kuwapa fursa wale wanao jipendekeza na kuwatukuza wakubwa wao hata kwenye mambo yasiyo msingi.

CCM kiwe chama huru kwa hoja kwa kila mwanachama kisiwe chama cha ndio mkuu.

Kama alivyosema Kinana kuwa CCM sio mali ya mtu mmoja hivyo hivyo kila mwanaCCM atambue hilo hii itampa fursa ya kujua wajibu na haki zake ndani ya chama na taifa kwa ujumla.

Fikra ya mwanaCCM ikibadilika basi chama kitabadilika pia kitaweza kuwa chama imara chenye kutekeleza wajibu wa kitaifa na sio watu wachache inavyotaka kuwa.

Peter Mwaihola

1649588636116.jpg
 
View attachment 2182802
Naona kama chama kimepata uhai tena, kua na kiongozi mwenye falisafa mpya ya siasa
 
Kwani unadhani bila wao kuwatukuza viongozi utapata uteuzi? Katiba yao ndo inashida,mfano kugombea ubunge kula za maoni hata ukishinda mpaka tena sijui kamati kuu ikae mara wa mwisho ndo agombee.
Waache mawazo ya wanachama wa chini yatimie.
Matusi Nape katukana sana mzee Lowasa akiwa chini ya kinana wala hakukanywa. Waache kuuingeenier vitu then vikifanyika kwa ukubwa na upande wao wanalalamika. Mfano Lowasa angelibahatika kuwa rais leo Nape na wenzake wangelikuwa wapi?
Badlisheni katiba Rais abaki kama rais na awe mjumbe tu wa kamati kuu. Tenganisheni serikali na Chama. Sasa Rais akibolonga wapi mtamwajibisha au kumhoji? Tumieni akili ndogo hamuoni South africa ANC wanavyo fanya. Bila hayo tusidanganyane Kinana kuleta mabadiliko zaidi ya kulipiza visasi tu.
 
Watu wajinga, wasio na uwezo, wanafiki, kitu pekee wanachoweza ni kuwalisha rushwa ya sifa viongozi wenye upeo duni. Hili lilidhihitika sana wakati wa awamu ya 5. Hata kukawa na watu wenye uwezo duni labisa lakini waliojaziwa mamlaka wasio na uwezo nayo.

Haitachukua miaka mingi mpaka kutangazwa kuwa uongozi wa awamu ya 5 ulikuwa wa kifashisti. Hili lilitokea hata Urusi. Kiongozi aliyesifiwa sana, Stallin, alipokuwa hai alisifiwa sana, maziko yake yakahudhuriwa na idadi ya watu wengi kuliko yeyote (kwa kumbukumbu zilizopo), mwili wake ukatunzwa, ukawekwa sambamba na mwili wa Lennin. Baada kama ya miaka takribani 10, Stallin alitangazwa rasmi kuwa alikuwa Rais muuaji, dikteta na fashisti. Mwili wake ukaondolewa ulipokuwa ukitunzwa, na kenda kutupwa sehemu isiyofahamika.

Kasi ya kuyatamka mabaya ya utawala wa awamu ya 5, tena na viongozi wakuu wa Serikali na chama, imekuwa siyo ya kawaida.
 
Back
Top Bottom