Tetesi: Kinana agoma kufika mbele ya Kamati ya Maadili ya CCM

Status
Not open for further replies.
Wakati Membe akitamba kuwa alienda mbele ya kamati ya maadili ya CCM kuwafunda na kuwaelimisha kuhusu mambo mbalimbali, Kinana amegoma kufika mbele ya kamati hiyo.

Kwa mujibu wa chanzo cha kuaminika, Kinana ameona ni kama kudharauliwa kwa kuitwa kuhojiwa mambo ambayo kimsingi ni malalamiko aliyotoa kuhusu namna alivyokuwa akipakwa matope na mtu anayejiita Cyprian Musiba. Inaelezwa kuwa aliyetakiwa kuitwa ni Musiba na siyo Kinana.

Kwa mujibu wa taarifa rasmi ndani ya chama, Kinana jana ijumaa alitakiwa kuwepo mbele ya kamati hiyo ya maadili lakini alisubiriwa hadi jioni na hakuna taarifa yoyote rasmi iliyopatikana juu ya kutokuhudhuria kwake mbele ya kamati hiyo.

Aidha hakutuma ujumbe wowote wa udhuru kuelezea kuhusu yeye kushindwa kufika mbele ya kamati hiyo kama ilivyopangwa.

Tusubiri tuone.
Taarifa za Mzee Kinana na Mzee Makamba kuitwa Ijumaa na kugoma sio za kweli. Taarifa rasmi za CCM zilikuwa ni za kumuita Kada Membe tu. Hao wengine watapangiwa siku nyingine/zingine. Na mnikariri, taarifa itatoka na watafika mbele ya Kamati ya Maadili ya CCM.
 
Samahani, lakini naamini hii ID inatumiwa na watu wengi.

Niseme tu kwamba,haya majibu yaliyowekwa hapa 'nahisi' sio mawazo ya huyo anayejulikana kwa jina hili. Lakini hizi ni 'hisia'; huenda kabadili mtindo na fikra.

Kwa mfano: Mwenye ID hawezi kamwe akaandika "Kila zana na kitabu chake baba."

Kujibu hoja: CCM zote ulizotaja hapo, ni CCM moja tu ndio imebadilishwa na kuwa "mali ya mtu mmoja"; kiasi kwamba hakuna tena mawazo mbadala ndani ya chama.
Kwa hiyo hii CCM ya Magufuli imejipambanua kabisa na hizo CCM nyingine zote ulizoziorodhesha hapo.
Ni nini ambacho hukuelewa, nostalgia inaweza kusumbua akili static lakin maisha ni dynamic. Wakati tunalalamikia ufisadi serikilini hadi kutoa list of shame, vigogo wa ikulu wakawa wanahonga mapesa kwa wasichana mitaani kama karanga, vigogo wakiwa wanajenga mahoteli huko Morogoro na sehemu nyinginezo kama uyoga kwa hela za walipa kodi, Kinana na Makamba walikuwa ndani ya SSM tena wakia na nafasi za juu sana. Huyu Makamba aliwahi kutoa matusi pale Tarime alipozomewa wakati wa kampeini za uchaguzi fulani, akijiskia kama mfalme hivi.
 
Magu kila siku analia ndani ya ccm kina majizi, kwa Nini tusianze kufikiria kuwa Hawa mapapa ndo majizi yenyewe kumbuka kikulacho ki nguoni mwako.kwa wale tulio na kumbukumbu sawa ugomvi wa magu na baadhi ya hawa wanachama wenzake ulianza baada ya mzee kuteua kamati ya kuchunguza Mali za chama.

Tunajua wapizani wamepata Cha kusema Sasa ila mtambue the real game is not started yet ccm itawala nyie kwanza mkiisha na ikakosa watu wa kula ndo tutaonana inajitafuna yenyewe.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Angeitwa kuhojiwa / kuongea na Amiri Jeshi Mkuu angeheshimu na angefata nidhamu na asingechelewa hata nusu dakika.

Kumbuka huyo ni mwanajeshi mstaafu mwenye cheo na ameshawahi kuwa Waziri wa Ulinzi na sasa ni mstaafu. Anafahamu maana ya nidhamu ni nini.

Si wewe au mwengine yeyote wa kumfundisha hayo. Amekitumikia chama zaidi ya trobo tatu ya maisha yake.

Kwa kukujuza tu, Kinana ni super bright, super intelligent.

Mwanajeshi hastaafu anapumzika tu.

Haya Bibie tumekusikia angekuwa mgalatia ungesema haya haya
 
ni nini ambacho hukuelewa, nostalgia inaweza kusumbua akili static lakin Maisha ni dynamic. wakati tunalalamikia ufisadi serilakilini hadi kutoa lis of shame, vigogo wa ikulu wakawa wanahong mapesa kwa wasichana mitaani kam karanga, viogo wakiwa wanajenga mahoteli huko Morogoro na sehemu nyinginezo kama uyoga kwa hela walipa kodi, kinana na makamba walikuwa ccm,

nitarekebisha post hii nikiwa kwenye keybord.
Huu nao ni ushahidi unaonipa shaka na ID hii.

"Data based evidence" mhusika wa ID hii ambayo hupenda kuitumia atakuwa kaitupilia mbali hadi ajiingize kwenye habari za majungu kama hizi?

Hakuna 'nostalgia' yoyote hapa kwa hizi CCM mpya; kasoro ile moja tu iliyokuwa ya wafanya kazi na wakulima kwa jitihada zake ilizokuwa ikizionyesha kwa wananchi na wananchi kuziona na kuzikubali. kuwa zilikuwa jitihada za dhati kabisa, hata kama mazingira hayakuruhusu zifanikiwe.

Hizi 'dynamism' za kuwafanya watu wawe wanyonge/mateka wa mtu mmoja hata kama zingeleta maziwa na asali, hizi akili zinazosemwa kuwa 'static' bado zingekataa utumwa huo.
 
Magu kila siku analia ndani ya ccm kina majizi, kwa Nini tusianze kufikiria kuwa Hawa mapapa ndo majizi yenyewe kumbuka kikulacho ki nguoni mwako.kwa wale tulio na kumbukumbu sawa ugomvi wa magu na baadhi ya hawa wanachama wenzake ulianza baada ya mzee kuteua kamati ya kuchunguza Mali za chama.

Tunajua wapizani wamepata Cha kusema Sasa ila mtambue the real game is not started yet ccm itawala nyie kwanza mkiisha na ikakosa watu wa kula ndo tutaonana inajitafuna yenyewe.

Sent using Jamii Forums mobile app
Pointless

Sent using Cash Money Wings
 
Yani wakina Msando na Polepole leo wanapata legitimacy ya kushughurikia issue ya Kinana & Makamba!

Sent using Jamii Forums mobile app
Ndugu hiyo ndiyo utawala wa sheria unavyotakiwa kuwa. Wewe unataka ule mfumo ambao watu fulani wanakuwa mungu watu na hata wakifanya makosa hawaulizwi? Je katiba ikibadishwa na kuruhusu rais kushtakiwa anapofanya makosa akiwa kwenye madaraka wewe si utapinga na kusema mtuy mkubwa kama rais hawezi kushtakiwa? Umeona USA rais ameshtakiwa na watu wa chini yake? Je, unataka kikundi fulani cha watu kisiguswe?
 
Ameogopa kwani anajua kosa lake. Huu ndiyo ulikuwa wakati mzuri wa yeye kwenda kuelezea upande wake wa shilingi. Kuitwa na kamati siyo kudharauliwa bali ni kusikilizwa!
Kwani wakati anachafuliwa kamati ilikuwa wapi kukemea hao viumbe?
 
Huu nao ni ushahidi unaonipa shaka na ID hii.

"Data based evidence" mhusika wa ID hii ambayo hupenda kuitumia atakuwa kaitupilia mbali hadi ajiingize kwenye habari za majungu kama hizi?

Hakuna 'nostalgia' yoyote hapa kwa hizi CCM mpya; kasoro ile moja tu iliyokuwa ya wafanya kazi na wakulima kwa jitihada zake ilizokuwa ikizionyesha kwa wananchi na wananchi kuziona na kuzikubali. kuwa zilikuwa jitihada za dhati kabisa, hata kama mazingira hayakuruhusu zifanikiwe.

Hizi 'dynamism' za kuwafanya watu wawe wanyonge/mateka wa mtu mmoja hata kama zingeleta maziwa na asali, hizi akili zinazosemwa kuwa 'static' bado zingekataa utumwa huo.
Inaweza kukuumiza sana, lakini Makamba na Kinana ni hadithi ya volume 4 sasa hivi tuko volume 5; mzee Mwinyi ambaye ndiye aliyeleta neno la serikali ya "awamu" ndiye huyo huyo aliyetuambia kuwa kila Kitabu na Zama Zake. Watu wenye busara wakishastaafu hupumzika na kuwa watoa ushuri tu, na siyo kila ushauri wao ukubalike.

Data pekee zinazohitajika hapa siyo namba bali ni facts tu: Makamba alikuwa Katibu Mkuu kwa mujibu wa Katiba ya CCM na alimalizamuda wake wa uongozi kwa mujibu wa Katiba hiyohiyo ya CCM; wakati akiwa katibu Mkuu kuna mambo aliyafanya ambayo yaliudhi baadhi ya watu na kuwafurahisha wengine. Kinana naye alikuwa Katibu Mkuu wa CCM na alimaliza muda wake kwa mujibu wa Katiba hiyo hiyo ya CCM; wakati akiwa katibu Mkuu kuna mambo aliyafanya ambayo yaliudhi baadhi ya watu na kuwafurahisha wengine. Magufuli ni mwenyekiti wa CCM aliyechaguliwa kwa mujibu wa Katiba hiyohoyo ya CCM; wakati akiwa Mwenyekiti kuna mambo ameyafanya ambayo yataudhi baadhi ya watu na kuwafurahisha wengine. Ndiyo facts na dynamics za maisha hizo; hakuna Kiongozi ambaye ni malaika; la kufanya ni kusubiri naye amalize muda wake kwa mujibu wa Katiba, afuate mwingine, ambaye naye atakuja na ya kwake.

Ni upuuzi kuwa tunazungumzia watu ambao hawaoingelei sera bali wanaongelea maslahi yao binafsi,eti tu kwa sababu ni viongozi waliostaafu, na wanapingana na mtu tunayemchukukia. Siwezi kumshangilia Makamba na Kinana eti tu kwa sababu simpendi Magufuli; no way. Magufuli ni afadhali sana kuliko jamaa hao.
 
Kwani wakati anachafuliwa kamati ilikuwa wapi kukemea hao viumbe?
Kuchafulia kwa lipi? Au kusemwa wewe ndiyo unaita kuchafuliwa! Acha watu watoe maoni yao. Uhuru wa maoni ndiyo tunaoutaka. Mkapa baada ya kuondoka madarakani alisemwa sana sana yeye na mke wake! Mwinyi hivyo hivyo!
 
Ndugu hiyo ndiyo utawala wa sheria unavyotakiwa kuwa. Wewe unataka ule mfumo ambao watu fulani wanakuwa mungu watu na hata wakifanya makosa hawaulizwi? Je katiba ikibadishwa na kuruhusu rais kushtakiwa anapofanya makosa akiwa kwenye madaraka wewe si utapinga na kusema mtuy mkubwa kama rais hawezi kushtakiwa? Umeona USA rais ameshtakiwa na watu wa chini yake? Je, unataka kikundi fulani cha watu kisiguswe?
Nyie walumumba unapofika wakati wa kutetea uji wenu huwa hambaki nyuma
 
Kuchafulia kwa lipi? Au kusemwa wewe ndiyo unaita kuchafuliwa! Acha watu watoe maoni yao. Uhuru wa maoni ndiyo tunaoutaka. Mkapa baada ya kuondoka madarakani alisemwa sana sana yeye na mke wake! Mwinyi hivyo hivyo!
Yule malaika wenu akiambiwa ukweli mnajitokeza ukoo mzima wa Lumumba na vitisho juu,hivi kwa nini lakini?
 
Hana cha kupoteza kwenye siasa za nchi hii na wala sijawahi kusikia ubin wake kwenye siasa za nchi hii.

Ila lazima awe msafi kwelikweli maana makaburi yatafukuliwa kwa lengo la kumkomoa tu.
 
Status
Not open for further replies.

Similar Discussions

Back
Top Bottom