Kinana afanya Ziara ya kushtukiza Tabora...!

TandaleOne

JF-Expert Member
Sep 4, 2010
1,644
709
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana amefanya ziara ya kushtukiza katika Mkoa wa Tabora asubuhi hii ambapo amekutana na Mkuu wa Mkoa huo Bi Fatma Mwasa na pia kukutana na viongozi wa Chama wa Mkoa ambapo alifanya kikao kidogo na viongozi hao akisisitiza juu ya utekelezaji wa Ilani na maagizo ya Mkutano Mkuu wa kufanya Mikutano ya ndani na nje na kutembelea mashina. Alisisitiza kuwa litakuwa ni jambo la ajabu ikiwa yeye kama Katibu Mkuu wa Chama katika ziara zake anatembelea na kufungua mashina kisha viongozi wa Mkoa ama eneo husika hawatembelei mashina hayo wala kufuatilia maendeleo yake.

Ndugu Kinana alitua Tabora Asubuhi hii akiwa njiani kutoka katika Mkoa wa Rukwa ambako alifanya Mkutano wa Hadhara na pia kufungua shina la Isesa wilayani Sumbawanga. Ndugu Kinana hivi punde ataendelea na Ziara yake, ambapo ataelekea Geita ambako atafanya Mkutano wa Hadhara na pia kufuatilia kero za wachimbaji wadogo pamoja na hali za waajiriwa katika migodi.

B. Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akimsalimia viongozi wa mkoa wa Tabora alipotua kwa mu.jpg C. Mkuu wa mkoa wa Tabora, Fatma Mwasa akimkaribisha Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana (kul.jpg
 
Hakuzomewa tena? Nasikia alipokuwa anazomewa kule Sumbawanga watu walikuwa wanamwita TX maana yake mtu asiye raia.
 
Katika vyeo vilivyokosa muelekeo ni pamoja na mkuu wa mkoa na wilaya! Hawa ni makada kabisa!
 
TABORA ya mkoloni ni BORA kuliko ya leo!ilikua kituo cha elimu,biashara na kilimo,usafiri wa reli!vyote vimekufa
 
VINANA wamekutana......Yeye na Rage.....hivi mkuu wa mkoa ni mtumishi wa umma au CCM? hii kitu naona haiko sahihi...na hapa ni ikulu

attachment.php
 
Mkuu ziara gani ya kushtukiza halafu anapewa na mapokezi rasmi ya DC, RC, Mazezeta yakiwa na sare tena asubuhi.

Sema Kinana amefanya ziara fupi rasmi mkoani Tabora wakati akiwa safarini kuelekea Geita.
 
Bahati mbaya sana kwa wachangiaji wa jukwaa hili, nasema ni bahati mbaya kwani hili linalotendeka humu halifunzi, halikuzi wala haliendelezi bali lina kera, linaudhi, na kupotosha. Jambo hili hasa hufanywa na pro-chadema katika jukwaa hili ambapo wengi katika wao huwa hawana kawaida wala utaratibu wa kujadili kitu kwa hoja bali hudhiaki, hukejeli na kutukana, hata katika yale ya msingi yenye kugusa utaifa wetu yatupasajo kuyajadili kwa umakini na hekima kuu.

Niliwahi kupata sema sehemu kuwa miongoni mwa jambo baya ambalo upinzani hasa chadema wamekuja nalo ni pamoja na kutuma vijana katika vyombo vya habari lakini pia mitandao ya kijamii ambapo wanapotosha, wanatukana na kukashifu viongozi wa chama na serikali. wanasambaza chuki na kufitinisha watu na makundi ya watu.

Nchi hii inayo misingi inayotulinda na kutuelekeza namna gani tuishi, ikihimiza kuheshimiana, utii na kushirikiana chini ya dhana kuu ya Ujamaa, tukijengewa misingi ya upendo na mshikamano, vitu ambavyo kwa sasa vinadharauliwa na kubezwa watu wakapanda mbegu za ubaguzi, ukanda, udini na chuki. Tulipokusudia kama Taifa kuanzisha vyama vingi wengi katika watu wliliona hili na kulihofia lakini kwa hekima za baadhi yetu walio na mamlaka wakakubali kuwa tuanzishe mfumo wa vyama vingi lakini kwa utaratibu huu tunaoenda nao tutafanya Taifa lisiwe salama.
 
Kwenda zako gamba mkubwa wewe...ni wafuasi wa chama gani wlio mabingwa wa kucharanga mapanga, kuchoma mikuki, kuteka na kuchinja wafuasi wa cdm kwenye chaguzi mbalimbali, kama sio ccm?******* kabisa hivi tukikaa kimya mnafikiri sisi *******...unaongelea amani gani hapa wewe kilaza.......mayo zako
 
Mwananchi Communications Ltd
Sisi tunampongeza kiongozi huyo wa CCM kwa kufanya ziara hiyo na kujionea mwenyewe jinsi wananchi mkoani humo wanavyoendelea kuteseka na kuishi maisha ya udhalilishaji katika nchi yao. Kinana amejionea mwenyewe jinsi Serikali ya chama chake ilivyovuruga uchumi wa mkoa huo kwa kula njama na baadhi ya wafanyabiashara na wanasiasa kuuziana viwanda vya korosho kwa bei ya kutupa. Viwanda hivyo vilitelekezwa na wamiliki hao baada ya kugundua wangepata faida kubwa kwa kuuza korosho nje ya nchi kabla hazijabanguliwa.
 
Mkuu ziara gani ya kushtukiza halafu anapewa na mapokezi rasmi ya DC, RC, Mazezeta yakiwa na sare tena asubuhi.
Sema Kinana amefanya ziara fupi rasmi mkoani Tabora wakati akiwa safarini kuelekea Geita.
nimemuona kwenye ITV Mtwara akilalamikia ufisadi kwenye korosho na gesi alafu watu anaowaambia wamechoka kupita maelezo.
Nilichojiuliza juu ya either kutoelewa au nia mbaya ya hawa jamaa (na Nape) wanalaumu kana kwamba wameiondoa CDM/CUF/NCCR nk madarakani na sasa ndio wanakuja kuleta mabadiliko wakati wenyewe ndio wameitawala hii nchi baada ya Mwalimu, wakaasisi ufisadi na wizi, wakaiba na leo wanawakashifu watz bila hata aibu!!

Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana amefanya ziara ya kushtukiza katika Mkoa wa Tabora asubuhi hii ambapo amekutana na Mkuu wa Mkoa huo Bi Fatma Mwasa na pia kukutana na viongozi wa Chama wa Mkoa ambapo alifanya kikao kidogo na viongozi hao akisisitiza juu ya utekelezaji wa Ilani na maagizo ya Mkutano Mkuu wa kufanya Mikutano ya ndani na nje na kutembelea mashina. Alisisitiza kuwa litakuwa ni jambo la ajabu ikiwa yeye kama Katibu Mkuu wa Chama katika ziara zake anatembelea na kufungua mashina kisha viongozi wa Mkoa ama eneo husika hawatembelei mashina hayo wala kufuatilia maendeleo yake.

Ndugu Kinana alitua Tabora Asubuhi hii akiwa njiani kutoka katika Mkoa wa Rukwa ambako alifanya Mkutano wa Hadhara na pia kufungua shina la Isesa wilayani Sumbawanga. Ndugu Kinana hivi punde ataendelea na Ziara yake, ambapo ataelekea Geita ambako atafanya Mkutano wa Hadhara na pia kufuatilia kero za wachimbaji wadogo pamoja na hali za waajiriwa katika migodi.

View attachment 72124 View attachment 72125

zile siasa za makundi zikifa kabisa 2015 kwa kuwanyongelea mbali mabwana mitandao wakubwa, CCM itarudi imara na hii itakua jambo zuri kwa Tanzania. CCM imara + upinzani makini=Tanzania yenye neema

Mungu ibariki Tanganyika
 
Mwananchi Communications Ltd
Sisi tunampongeza kiongozi huyo wa CCM kwa kufanya ziara hiyo na kujionea mwenyewe jinsi wananchi mkoani humo wanavyoendelea kuteseka na kuishi maisha ya udhalilishaji katika nchi yao. Kinana amejionea mwenyewe jinsi Serikali ya chama chake ilivyovuruga uchumi wa mkoa huo kwa kula njama na baadhi ya wafanyabiashara na wanasiasa kuuziana viwanda vya korosho kwa bei ya kutupa. Viwanda hivyo vilitelekezwa na wamiliki hao baada ya kugundua wangepata faida kubwa kwa kuuza korosho nje ya nchi kabla hazijabanguliwa.
mkuu, sasa Kinana ametembelea Ikulu ndogo ya Tabora, hapo ataona umasikini upi? na amesema hawezi kwenda kufungua mashina........kwenye wanatabora masikini.
attachment.php
 
Back
Top Bottom