Kinadada tu: ipi bora kati ya kubwa na ndogo?

Mtu B

JF-Expert Member
Dec 2, 2008
919
51
Nazungumzia pete ya uchumba. Mchumba wako akitaka akusapraizi na pete siku flani, utapenda iwe kubwa au ndogo? Yaani uzito au mwonekano, sio ule ukubwa wa kulegea kidoleni au kubana sana, najua si nzuri hiyo.
 
Ndogo ni bomba sana.I mean nyembamba yenye madoido ya kuacha vinafasi.
Teh teh teh ! isije ikawa unataka kumsapraiz mchumba ako yupo humu JF afu hajashtukia dili. Isije ikawa wewe Lily flower!
 
Nitapendelea ya dhahabu na kwa juu iwe na almasi, shapes dosent matter.

Vipi kuhusu uzito wake, yaani iwe na gram ngapi kwa mfano za dhahabu na hiyo almasi karat ngapi? Unapenda kuubwa au kiduuuch au saiz flani ya kati, au ya kiaje?
 
sitajali ni kubwa au ndogo, ya bati au shaba......cha muhimu iwe na jiwe la tanzanite kwa juu
 
Iwe size ya kati, Gold na birth stone juu yake kama mie jiwe la Emerald.
 
Vyovyote itavyokuwa ilimradi iambatane na penzi la kweli! Maana wapo walovika mijipete ya kifahari sasa hivi wanalia kuivua hawawezi!!
 
Nazungumzia pete ya uchumba. Mchumba wako akitaka akusapraizi na pete siku flani, utapenda iwe kubwa au ndogo? Yaani uzito au mwonekano, sio ule ukubwa wa kulegea kidoleni au kubana sana, najua si nzuri hiyo.

ila hili swali lako limekaa namna fulani hivi.....
 
Vyovyote itavyokuwa ilimradi iambatane na penzi la kweli! Maana wapo walovika mijipete ya kifahari sasa hivi wanalia kuivua hawawezi!!
Dah! yani umeua kabisaaa.Pete siku hizi ni fasheni.Na kuna watu wanajivalisha wenyewe waonekane wamechumbiwa au wameolewa.
Kwa mtizamo wangu kuvaa pete ni heshima kubwa sana(i mean wanaovaa pete huwa wanaheshimiwa zaidi)
 
zote ya ndoa na ya uchumba ziwe saizi ya kati tu, zinazovutia, na uwa la ya uchumba lisiwekubwa sana sijui km unaelewa inatakiwa uone mfano halisi siyo imagination.
All the Best!!
 
Vipi kuhusu uzito wake, yaani iwe na gram ngapi kwa mfano za dhahabu na hiyo almasi karat ngapi? Unapenda kuubwa au kiduuuch au saiz flani ya kati, au ya kiaje?
Huyo atakaye nivisha ndio atachagua iwe na shape gani iweje, jua kuwa engagement zingine huwa ni suprise, uzito na mambo ya karat ni mfuko wake tu.
 
Vyovyote itavyokuwa ilimradi iambatane na penzi la kweli! Maana wapo walovika mijipete ya kifahari sasa hivi wanalia kuivua hawawezi!!

yes mama umenena, kweli wewe mwanajamii..................

nimewahi kuona kwa macho angu mwanmke akivua pete zote mkononi na kumrudishia mumewe ka sababu akiziona anakumbuka siku walipofunga ndoa na anjuta sana kuolewa na yule mwanume............... yah, ddhahabu, almasi, tanzanite, emarard etc ni takataka tu, chagueni upendo wa dhati.........

hebu chukua wine hapo niletee bili huku kwa heshima ya maoni haya.........

ngoja nimuite mpenzi wangu aje kukusoma sasa hivi........ apate darasa lililoenda shule.........
 
ile kichwa cha habari na mada zinatofautiana kidogo au mnaongelea mafumbo mwongozo pls
 
Nashukuru kwa wote mliojibu hadi sasa, lakini naomba mnisaidie pia kujibu haya ambayo nimekusanya kwenye majibu yenu so far:

Kuna mmoja kasema anataka awekewe birth stone. Hii ni kitu gani na nitaijuaje birth stone ya mtu fulani? Nikimuuliza siyo surprize tena.

Ingawa wapo waliosema hawajali design, lakini naamini zipo design zinazopendwa zaidi ya nyingine. Nishaurini hapo pia.

Na vipi suala la kwenda nae window shopping kwa masonara kabla ya uamuzi mnalionaje?
 
Birth stone ni rahisi sana! Ukienda kwa sonara unatakiwa tu ujue mpenzi wako alizaliwa mwezi gani kwa kuwa kila mwezi una jiwe lake (I for one don't believe in these things but that is anaother topic)!!

Kuhusu window shopping si vibaya ukienda naye ili uijue ''taste'' yake vizuri....maana waweza kuingia gharama kubwa halafu hiyo pete yenyewe bado ''isimkune'' kama unavyotaka!
 
True love begins when nothing is looked for in return.
This is an engment ring made of pearl
 
Birth stone ni rahisi sana! Ukienda kwa sonara unatakiwa tu ujue mpenzi wako alizaliwa mwezi gani kwa kuwa kila mwezi una jiwe lake (I for one don't believe in these things but that is anaother topic)!!

Kuhusu window shopping si vibaya ukienda naye ili uijue ''taste'' yake vizuri....maana waweza kuingia gharama kubwa halafu hiyo pete yenyewe bado ''isimkune'' kama unavyotaka!

Hapo umeshanisaidia pia, inawezekana mtu mwenyewe pia akawa haamini hayo mambo ya birth stones, halafu nikaishia kuja kueleweka vibaya. Lakini unaonaje nikijaribu kumsababisha azungumzie msimamo wake juu ya jambo kama hilo pia? Mie pia siamini chochote juu ya mawe kama hayo, lakini sioni shida kumnunulia kama anataka.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom