Nitapendelea ya dhahabu na kwa juu iwe na almasi, shapes dosent matter.
Nazungumzia pete ya uchumba. Mchumba wako akitaka akusapraizi na pete siku flani, utapenda iwe kubwa au ndogo? Yaani uzito au mwonekano, sio ule ukubwa wa kulegea kidoleni au kubana sana, najua si nzuri hiyo.
Dah! yani umeua kabisaaa.Pete siku hizi ni fasheni.Na kuna watu wanajivalisha wenyewe waonekane wamechumbiwa au wameolewa.Vyovyote itavyokuwa ilimradi iambatane na penzi la kweli! Maana wapo walovika mijipete ya kifahari sasa hivi wanalia kuivua hawawezi!!
Huyo atakaye nivisha ndio atachagua iwe na shape gani iweje, jua kuwa engagement zingine huwa ni suprise, uzito na mambo ya karat ni mfuko wake tu.Vipi kuhusu uzito wake, yaani iwe na gram ngapi kwa mfano za dhahabu na hiyo almasi karat ngapi? Unapenda kuubwa au kiduuuch au saiz flani ya kati, au ya kiaje?
Vyovyote itavyokuwa ilimradi iambatane na penzi la kweli! Maana wapo walovika mijipete ya kifahari sasa hivi wanalia kuivua hawawezi!!
ile kichwa cha habari na mada zinatofautiana kidogo au mnaongelea mafumbo mwongozo pls
Nashukuru kwa wote mliojibu hadi sasa, lakini naomba mnisaidie pia kujibu haya ambayo nimekusanya kwenye majibu yenu so far:
Kuna mmoja kasema anataka awekewe birth stone. Hii ni kitu gani na nitaijuaje birth stone ya mtu fulani? Nikimuuliza siyo surprize tena.
Ingawa wapo waliosema hawajali design, lakini naamini zipo design zinazopendwa zaidi ya nyingine. Nishaurini hapo pia.
Na vipi suala la kwenda nae window shopping kwa masonara kabla ya uamuzi mnalionaje?
drphone na mwenzio Akilikichwani,are you she? mie najuaga nyie ni hes.MtuB kasema kwa akina dada tu!
Birth stone ni rahisi sana! Ukienda kwa sonara unatakiwa tu ujue mpenzi wako alizaliwa mwezi gani kwa kuwa kila mwezi una jiwe lake (I for one don't believe in these things but that is anaother topic)!!
Kuhusu window shopping si vibaya ukienda naye ili uijue ''taste'' yake vizuri....maana waweza kuingia gharama kubwa halafu hiyo pete yenyewe bado ''isimkune'' kama unavyotaka!