kinadada tu: ati hawara wa kakako naye utamwita wifi? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

kinadada tu: ati hawara wa kakako naye utamwita wifi?

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Mtu B, Jul 5, 2010.

 1. M

  Mtu B JF-Expert Member

  #1
  Jul 5, 2010
  Joined: Dec 2, 2008
  Messages: 921
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Nimekuta ugomvi mkubwa kati ya mtu na wifi yake. Ni kwamba kabla hajaoa, huyo kaka mtu alizaa na mwanamke flani hivi, kisha hazikuiva kwa hiyo hakumuoa. Sasa ana mke wa ndoa na wana watoto. Mkewe kamkuta dada wa mumewe akizungumza kwa bashasha na mzazi mwenza huyo huku neno 'wifi' likitumika kama ndio uhusiano baina yao; huyu akiongea anasema 'wifi hivi na vile' mwenzie hali kadhalika. Mke wa ndoa ameumizwa sana na hali hiyo, akalianzisha na wifi yake kuwa "iweje huyu naye wamwita wifi ilhali si mke wa kakako? Au tuambizane kabisa, kakako ana wake wawili?" Dada nae kaja juu "unataka nimwiteje?" Basi ugomvi mtindo mmoja almanusura watoane macho.

  Sasa nawauliza akina dada, mtu kama huyo anastahili kuitwa wifi au la? Na kwa hiyo aitweje basi? Uzoefu wenu kinadada ambao kaka zenu wana watu wa namna hiyo, huwa mnawaitaje hao kinamama?
   
 2. M

  Mtu B JF-Expert Member

  #2
  Jul 5, 2010
  Joined: Dec 2, 2008
  Messages: 921
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Kipi cha hovyo hapo?
   
 3. Mom

  Mom JF-Expert Member

  #3
  Jul 5, 2010
  Joined: Oct 13, 2009
  Messages: 708
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  kazi ipo, lakini huyo dada mtu nae inawezekana alimwita wifi kumkomoa mwenzie au? ingekua m huyo mke wala nisingewamind maana kwani si mi ndie mke kama thats what matter!
   
 4. Mkeshahoi

  Mkeshahoi JF-Expert Member

  #4
  Jul 5, 2010
  Joined: Jan 4, 2009
  Messages: 2,494
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 145
  Nahic Chaimen wa UWTz , Bi Lion atalijibu kwa mapana na marefu... asifika katika nyanja ya ndoa!!
   
 5. Safina

  Safina JF-Expert Member

  #5
  Jul 5, 2010
  Joined: Jun 18, 2009
  Messages: 498
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kama ambavyo kuna msemo unasema: Mtalaka hatongozwi, upo mwingine: Uwifi/ushemeji haufi, ina maana hata kama kakangu ameachana na aliyekuwa mpenzi wake, neno wifi huwa linabaki pale pale, hiyo haimaanishi kuwa kaka bado anamahusiano na huyo bibie. Halafu huyu bado wana mahusiano kwani kuna damu yao pale. Kwa sababu sasa huyo mtoto hasimwite shangazi yake shangazi kama huyu mama mdogo hatiki wifi mtu amwite wifi wa zamani wifi.
   
 6. Safina

  Safina JF-Expert Member

  #6
  Jul 5, 2010
  Joined: Jun 18, 2009
  Messages: 498
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ni kipi cha hovvo hapa edwinito, Huyo wifi mtu wa zamani kumwita wifi? Mke mtu kukasirika? Au mleta mada kuleta hii mada?
   
 7. M

  Mtu B JF-Expert Member

  #7
  Jul 5, 2010
  Joined: Dec 2, 2008
  Messages: 921
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Wewe ungeshauri huyo dada mtu mwiteje mzazi mwenza wa kakake? Au tuseme, upande mwingine, mwanamke aliyezaa na mtu ambaye si mumewe anapaswa kuwaitaje dada za huyo mzazi mwenzie?
   
 8. M

  Mtu B JF-Expert Member

  #8
  Jul 5, 2010
  Joined: Dec 2, 2008
  Messages: 921
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Dada Safina naona kilichosababisha ugomvi ni kuwa huyu mke wa ndoa kakasirika sana kusikia kuna mtu mwingine anayeitwa wifi mahali pake, ambapo anajijua kuwa wifi yao kwa huyo kaka ni yeye tu, sasa ameumia na kukasirika kusikia huyo pia aitwa wifi, ingawa anamfahamu toka zamani kuwa ndiye aliyezaa mtoto wa kwanza na mumewe. Na pia amechukulia kama dada mtu anashabikia huo 'uwifi' ambao unapaswa kuwa haramu. Pengine kungekuwa na neno mbadala haya yasingetokea.
   
 9. M

  Mtu B JF-Expert Member

  #9
  Jul 5, 2010
  Joined: Dec 2, 2008
  Messages: 921
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Dada Safina naona kilichosababisha ugomvi ni kuwa huyu mke wa ndoa kakasirika sana kusikia kuna mtu mwingine anayeitwa wifi mahali pake, ambapo anajijua kuwa wifi yao kwa huyo kaka ni yeye tu, sasa ameumia na kukasirika kusikia huyo pia aitwa wifi, ingawa anamfahamu toka zamani kuwa ndiye aliyezaa mtoto wa kwanza na mumewe. Na pia amechukulia kama dada mtu anashabikia huo 'uwifi' ambao unapaswa kuwa haramu. Pengine kungekuwa na neno mbadala haya yasingetokea.
   
 10. Mom

  Mom JF-Expert Member

  #10
  Jul 5, 2010
  Joined: Oct 13, 2009
  Messages: 708
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  uwifi na ushemeji haufi lakini ebu nikupe mfano, rafiki yangu wa kike ana kaka ambae kabla hajaoa alizaa na binti mmoja na familia nzima inafahamu hilo. sasa huyu mzazi mwenzie na kaka ni jirani na wamezoeana kuitana wifi lakini mke wa kaka akiwepo wanamuita mama nanihii, ikajatokea rafiki yangu kakorofishana na mke wa kaka sasa akawa anamfanyia makusudi akijua mke wa kaka anasikia anamwita yule mzazi mambo wifi hujaja cku nyingi mama amekukumbuka.... na yule mke si akawa anamind mpaka ugomvi ukawa hauishi anamtuhumu mume anaendeleza mahusiano na mzazi mwenzie na mume akajibu kwa kiburi ana mtoto wangu!
   
 11. Mama Brian

  Mama Brian JF-Expert Member

  #11
  Jul 5, 2010
  Joined: Feb 7, 2010
  Messages: 321
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  mie nadhani ningekuwa mimi wala nisingemind wamwite huyo mzazi mwenza wifi wasimwite its ok madamu anayejulikani ni mke wa ndoa ni mimi. Hapo nadhani huyo wifi alifanya makusudi kutaka kumkomoa huyo wifi yake wa ukweli manake mawifi nao wanamambo, angempuuzia tu wala asimind huyo wifi mtu angejiona ovyo kwamba kachemka.
   
 12. M

  Mtu B JF-Expert Member

  #12
  Jul 5, 2010
  Joined: Dec 2, 2008
  Messages: 921
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Duh hii naona ilikuwa na ajenda ya kukomoa zaidi! Binafsi ningekuwa mimi nisingefurahia kusikia dada zangu wakimwita 'wifi' mtu ambaye si mke wangu, especially kama kauli hiyo itamuumiza mke wangu. Lakini jamaa anaongezea petroli kwenye moto, huyo labda keshamchoka hata huyo mkewe!
   
 13. FirstLady1

  FirstLady1 JF-Expert Member

  #13
  Jul 5, 2010
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 16,575
  Likes Received: 543
  Trophy Points: 280
  Wifi na shemeji huwa haifi hata siku moja ...
   
 14. T

  Tata JF-Expert Member

  #14
  Jul 5, 2010
  Joined: Dec 3, 2009
  Messages: 4,737
  Likes Received: 657
  Trophy Points: 280
  Naomba ufafanuzi hapa. Hivi mtu kama huyo, yaani mwanamke aliyezaa na kaka, anapaswa aitweje na madada wa huyo kaka mhusika?
   
 15. M

  Mtu B JF-Expert Member

  #15
  Jul 5, 2010
  Joined: Dec 2, 2008
  Messages: 921
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  ingekuwa wewe ndio huyo mke wa ndoa halafu wifi yako kafanya hivyo, ungekubali kuwa ni sawa kuwa wifi yako anaona anao mawifi wawili kwa kakake mmoja wakati unataka itambulike ni wewe tu? unashauri aitweje, bado ni wifi au kuna jina mbadala?
   
 16. M

  Mtu B JF-Expert Member

  #16
  Jul 5, 2010
  Joined: Dec 2, 2008
  Messages: 921
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Haswaa ndicho ninachouliza hapa maana waswahili wanasema 'ukiona mwenzio ananyolewa wewe tia maji'. Mimi dada zangu wana tabia ya kumfanyia utani msichana aliyekuwa girlfriend wangu tulipokuwa chuo, nikienda kwa dadangu mmoja huyo lazima aniambie 'nimemwona wifi kapendeza huyo!' Lakini huwa tunacheka tu maana ni utani tu na pia sikuzaa nae. Ila kusema kweli nikishaoa sitapenda kusikia comments za hivyo na tena zaidi sitapenda mke wangu asikie wengine wakiitwa wifi wakati siyo.
   
 17. Mom

  Mom JF-Expert Member

  #17
  Jul 5, 2010
  Joined: Oct 13, 2009
  Messages: 708
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  mawifi wenye akili atamwita wifi lakini atatafuta means ambayo itasaidia kuondoa kuumizana! ingekua ni kwako je dada wa mzazi mwenzio utamuadress vipi pale mnapokutana njiani ww ukiwa may be na rafiki zako?
   
 18. SMU

  SMU JF-Expert Member

  #18
  Jul 5, 2010
  Joined: Feb 14, 2008
  Messages: 7,933
  Likes Received: 2,085
  Trophy Points: 280
  Ooops...kumbe kina dada tu!
   
 19. Safina

  Safina JF-Expert Member

  #19
  Jul 5, 2010
  Joined: Jun 18, 2009
  Messages: 498
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kama ni mimi ningeona poa tu, kwa sababu kuonyesha kukasirika ndo kunampa hata huyo wifi mtu anayefanya makusudi mwanya wa kuludia kumwita wifi mara kwa mara kwa nia ya kumfanya mwenzake ajisikie vibaya. Bila shaka huyo muolewaji ndiye wifi pekee kwa sababu huyu mwingine si kaitwa tu lakini hamna kinachoendelea. Na kama kipo kinachoendelea mimi nitajiona bado mshindi kwa sababu yeye alianza, akaacha na bado tena anatamani matapishi yake aliyoyaacha nikaolewa mimi. Kifupi nisingeona kama ni big deal kwa sababu hata ukikasirika kama anamwita wifi hataacha kumwita na kama bado anaendelea na mahusiano na kaka mtu hata nikikasirika hawataachana kwa sababu mimi nimekasirika huyu mwenzangu kuitwa wifi. Cha msingi ni huyu dada kujiamini na kuona yeye ndiye bora zaidi ya huyo wifi wa zamani hata kama wamezaa, maana angekuwa yeye ndiye bora angeolewa yeye na sio kuzalishwa, kuachwa na hawa mawifi kuendelea kumpa kichwa kwa kumwita wifi. Mawifi wengine bwana sijui huwa wanataka nini? Kuwalusha wenzao roho tu, na hasa wakijuwa kwamba huwa unarushika roho kirahisi ndo basi utaipata.
   
 20. Edson

  Edson JF-Expert Member

  #20
  Jul 5, 2010
  Joined: Mar 7, 2009
  Messages: 9,202
  Likes Received: 722
  Trophy Points: 280
  my wife wangu huwa akikuta na mzazi mwenzangu wa zamani, wanapiga stori na kula tano kama kawa.
  hawana noma kabisa. so inategemeana na ntu na ntu.
   
Loading...