Kinachozeesha mwili ni akili

clearmind

JF-Expert Member
Dec 26, 2013
424
724
Kwa muda sasa nimekuwa nikitafakari sana kwamba huenda kama binadam asingekuwa na shughuli nyingi sana zinazohitaji ubongo wake kufikiri kwa kina sana ili kupata majibu au matokeo ya kile anachokifanya, basi angedumu kwa muda/miaka mingi sana bila kuzeeka. Nina mifano michache hapa:

Nina rafiki mmoja ambae kabla ya kuajiriwa miaka mitatu nyuma alikuwa kijana kabisa wala huwezi kumfikiria kuwa na umri mkubwa kwa namna yoyote ile. Baada ya kupewa majukumu mazito ambayo mara nyingi yanahitaji matumizi makubwa ya akili, ameanza kuota mvi kwa haraka sana ndani ya mwaka mmoja tu na sura yake sasa inaonesha ni mtu wa makamo ilihali ni kijana mdogo tu.

Mfano wa pili, narejelea, muonekano wa Barack Obama kabla ya kuwa rais na baada ya kuwa rais(kama picha zilizowekwa mtandaoni ni sahihi). Mfano wa mwisho, nimewahi kuangalia pia picha za Kikwete kabla ya urais na muda mfupi baada ya kuwa rais.

Ndugu wanajamvi, kuna uwezekano jambo hili likawa na uhalisia? Kwa wakristo, rejea kwa manabii, mitume na wafalme wa zamani katika biblia miaka walioishi. Huenda kudumu kwa muda mrefu kulichangiwa na namna walivyoishi, yaani hawakuhitaki kuumiza kichwa sana kufikiria kuishi maisha yenye uhitaji wa mikiki mikiki ya akili.
 
Kisayansi ubongo ni sehemu ya mwisho kuzeeka, mara nyingi ubongo huanza kuzeeka kuanzia miaka 90 na kuendelea

Kiungo cha kwanza kuzeeka hua ni moyo na kinaanza ukifikisha miaka 30, na hapa ndipo wanamichezo wengi ndipo wanapoacha au viwango vyao kupungua.
Oooh dah ahsante kwa somo mkuu. Namna ya kuulinda moyo usizeeke je
 
Hyo namba moya
Mbona kwangu ni rahisi sana mkuu unakwama wapi

Mchicha, nyanya, vitunguu, mafuta ya mawese, chumvi mboga tayari kwa kuliwa ugali wa dona mixer udaga

SIMPLE KIHIVYO YAANI NA LIFE NI TAMU BALAA HAKUNA MAGONJWA WALA MWILI KUJISIKIA UCHOVU WA MARA KWA MARA

Ninachomaanisha vikorombwezo vingi sivitaki kwenye msosi wangu ndio maana huwa sina utaratibu wa kula harusini ama kwenye tafrija
 
Siri ya kutoonekana mzee na pia kuwa na nguvu za kiume ni hii

1: Kula vyakula vya asili na vipikwe kimaskini.

2: Kufanya kazi, kuwa na furaha na kulala angalau saa 8 kwa siku.

3: Kutokutumia kilevi na bidhaa zote za tumbaku
nakazi pia na mazoezi kidgo sio mbaya
 
Kwa muda sasa nimekuwa nikitafakari sana kwamba huenda kama binadam asingekuwa na shughuli nyingi sana zinazohitaji ubongo wake kufikiri kwa kina sana ili kupata majibu au matokeo ya kile anachokifanya, basi angedumu kwa muda/miaka mingi sana bila kuzeeka. Nina mifano michache hapa:

Nina rafiki mmoja ambae kabla ya kuajiriwa miaka mitatu nyuma alikuwa kijana kabisa wala huwezi kumfikiria kuwa na umri mkubwa kwa namna yoyote ile. Baada ya kupewa majukumu mazito ambayo mara nyingi yanahitaji matumizi makubwa ya akili, ameanza kuota mvi kwa haraka sana ndani ya mwaka mmoja tu na sura yake sasa inaonesha ni mtu wa makamo ilihali ni kijana mdogo tu.

Mfano wa pili, narejelea, muonekano wa Barack Obama kabla ya kuwa rais na baada ya kuwa rais(kama picha zilizowekwa mtandaoni ni sahihi). Mfano wa mwisho, nimewahi kuangalia pia picha za Kikwete kabla ya urais na muda mfupi baada ya kuwa rais.

Ndugu wanajamvi, kuna uwezekano jambo hili likawa na uhalisia? Kwa wakristo, rejea kwa manabii, mitume na wafalme wa zamani katika biblia miaka walioishi. Huenda kudumu kwa muda mrefu kulichangiwa na namna walivyoishi, yaani hawakuhitaki kuumiza kichwa sana kufikiria kuishi maisha yenye uhitaji wa mikiki mikiki ya akili.
Mbona walimu hawazeeki?
 
Ni kweli
 
Kufikiri tu peke yake sio mbaya, ila kustress-kufikiri ndio itakuwa inazeesha maana mtu binafsi (self) inasumbuliwa. Zile aina ya fikra fulani za kiudadisi ambazo hazina mgandamizo na mkazo zile hazizeeshi, zile unaliangalia tu jambo kama lilivyo ili kulijua na kulielewa tu wewe kama mtazamaji flan iv. Actually huo udadisi wa kitoto 'unajanisha' unakufanya urudi kuwa mtoto.

Sifa kubwa ya mtoto ni kujifunza na mtu mzima akiishi kwa kujifunza kama mtoto hazeeki mapema. Uthibitisho WAALIMU hasa wa shule za msingi wale wanaoimba a,e,i,o,u,na watoto kila siku!!
 
Yaani akili ndo ubongo wenyewe sasa unafanya kazi ,usiombe kuchosha akili yako kwa kazi unaweza kuumwa mwili mzima .

Bado ukiwa na stress akili Inakuwa haifanyi kazi acha tu ,unaanza kupoteza Nuru usoni mara makunyanzi kama mzee, mwisho wa siku akili haiwazi mambo ya maana inawaza mambo ya masononeko mpaka unakufa .

Hata tunapofany kazi tusiwe ile serious sana akili inahitaji kupumzika hata kufurahi, kazini kama kutatua changamoto za wateja na risky za hapa na pale haziishi ,mara kufokewa mara kutia hasara ..Unaweza kosea kazi ukaharibu na kuleta hasara so unakuwa kiakili unakuwa na mawazo fulani.

Ushauri hata kama kazi yako una unapata pesa kidogo jifundishe kuspend ,kama sio mleni nenda hata tour moja kila likizo jichange kidogo, weekend kula Bata utulize akili.
 
Back
Top Bottom