Kinachowaponza wasanii ni kitendo cha kutangaza hadharani kuwa CCM ilikuwa inawalipa

Nibozali

JF-Expert Member
Oct 15, 2016
572
1,055
Kama mtakumbuka Mara kadha wasanii Wa bongo movies/fleva wamekuwa wakijitokeza kwenye media wakidai kulipwa au kutokulipwa na chama cha mapinduzi kipindi kigumu cha kampeni mwaka 2015.

Wengi wao wamekuwa wakithibitisha kuwa walilipwa stahiki zao na kwamba wale wanaodai kuwa hawajalipwa wana chuki binafsi

Ni wapi wasanii hawa wanakosea?

1. Wanataka kuuaminisha umma Wa watanzania na dunia kwa ujumla kuwa ule utitiri Wa wasanii kuipigia kampeni ccm kipindi kile cha kampeni ilikuwa kwa sababu ya malipo mazuri waliyopewa/kuahidiwa.

2. Na kama walifanya kazi hiyo kwa ahadi ya kulipwa na nzuri zaidi wameshalipwa kama wanavyodai, nini kingine wanachodai kutendewa na serikali tofauti na RAIA wengine, kwani kila kukicha wanalialia kwenye media kuwa chama kimewasahau/ hakiwajali wakati walifanya kazi kubwa kipindi cha kampeni

Imefika kipindi nyie wasanii uchwara Wa kibongo mumuache rais wetu afanye kazi kwa amni na chama change kizidi kupendwa
 
Back
Top Bottom