Kinachoua lounge na bar nyingi Dar ni huduma mbovu kwa wateja

Majuzi hapa JF Kuna mdau alipost kuhusu tips lounge kukosa wateja..leo mida ya saa kumi jioni nilienda lounge moja maarufu Sana dar ambayo kwa weekend ukichelewa kidogo unakosa parking au utapata tabu Sana kupata parking.

Nilipofika nilikaa kwenye Kochi huku nikiwa busy na simu lakini hakuna muhudumu aliyekuja baada Kama ya dk 20 Hadi nilipofanya jitihada za kumwita mmoja aliyekuwa anapita..,baada ya kunihudumia second round nikampa fedha hakurudushi chenji zaidi ya saa moja na nusu baadaye nikampata akarejesha. Then nikamwita mwingine nikasema nataka mtu wa chakula naye kapotea moja kwa moja hata hajamwita mtu wa chakula...duuh..nikasema hizo zote scenario tatu zimetokea kwangu, je ni wangapi wamepitia haya nayopitia.?

Je hizi bar na lounge zikiona watu wanajaa usiku wa manane wanadhani wamemaliza kila kitu.?

Sitataja hiyo lounge coz isije ikaonekana naiharibia biashara .
Na wakikozea wanaaanza kukuomba omba pesa
 
DSM viwanja na Samaki samaki ya Masaki na Maison tu vinginge vyote ni utopolo.
 
Pale Malaika Pub ya mjini Shabiby, nishakula mchemsho wa kuku kama mara 2 bila kulipa.
Muhudumu anakuletea chakula, kisha humuoni tena akirudi mpaka baada ya masaa au lisaa..watu nyomi, naanzaje kumtafuta.
Nikapita zangu hivi... Na maji makubwa ya baridi
Mungu hapendi
 
Pole sana, siku nyingine itisha manager...
Meneja mody kwa macheni pale nilikua nae karibu.
Basi nikitia mguu tu anapanga meza wahudumu na mbususu mpya anaweka.
Hapo mezani badae nawaita watu wangu ni vyombo tu mpk kunakucha.
Ukiongea na meneja kazi imeisha.
 
Back
Top Bottom