Kinachotokea znz ni Hatari sana Lazima tuwe makini! (Jicho la tatu) | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kinachotokea znz ni Hatari sana Lazima tuwe makini! (Jicho la tatu)

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Borakufa, May 28, 2012.

 1. Borakufa

  Borakufa JF-Expert Member

  #1
  May 28, 2012
  Joined: May 26, 2011
  Messages: 1,503
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Ndugu zangu watanzania!

  Hoja ya jumuia ya uamusho ilikuwa hawautaki muungano! Lakini tayari rais wa jamuhuri ya muungano alikwisema muungano haujadiliki lakini pia cc ya ccm ilikwishasema muungano lazima uwe wa serikali mbili siyo vinginevyo!!! Hili ni bomu kwa zanzibar na Tanganyika.

  Kilichotokea zanzibar juzi na jana ni jambo kubwa! lakini rais wa Jamuhuri ya muungano yupo kimya!! kama haitoshi rais wa zanzibar yupo kimya pia kama hakijatokea kitu vile!!! Yani katika hali tete kama hii ya vita vya kidini vinavyotengenezwa kwa utaalamu wa hali ya juu viongozi wetu wamenyamaza na kutuacha wananchi tufikirie vyovyote vile na kuamua tutakavyo.

  Nionavyo mie (natiririka)

  Kwa kuwa viongozi wetu hawa walioshindwa! wanajua wazi kuwa adui wetu namba moja katika taifa hili ni wao na mafisadi wao kila siku wao wamezamia na majasusi (usalama wa ccm) wao katika kuibua mbinu ambayo itabadilisha mtazamo wetu wa kuachana na kupambana na wao na mafisadi wao tugeukiane na kuanza kupambana kama waislamu na wakristo!!!
  Kwa kiasi fulani mbinu wanazo jaribu kupika zinaanza kuzaa matunda!! na kama kweli zitafanikiwa 100% basi taifa linaloitwa Tanzania litafutika kabisa!!
  Haiwezekani mtu kama JK alivyolinyonya taifa hili yeye na familia yake, marafiki na mashwahiba zake wakubali kirahisi kuliona taifa hili likirejea katika utawala wa kuheshimu sheria!! kwa sababu kukubali kufanya hivyo watakuwa wamejipiga kitanzi wao wenyewe kwa madhambi waliowadhurumu wananchi watukufu wa taifa hili.

  Wanchofanya mafisadi hawa ni kucheza na zama! lakini wakijua fika nyuma wanafanya kitu hatari kwa mstakabali wa taifa letu hili pendwa.

  Kiongozi wa Uamsho kakamatwa! wafuasi wake wanaandamana kupinga yeye kukamatwa! kama walivyoandamana wana wa arusha kupinga kukamatwa kwa viongozi wao wa cdm 05.01.2011 kulikopelekea watu 3 kuuwawa! Iweje kanisa lichomwe! kuna uhusiano gani hapa jamani!!! (Hebu tufikirie)

  Majasusi wa watawala mafisadi na mbinu zao wamelichoma kanisa makusudi ili kuivuruga hoja nzima ya uamsho ya kuukataa muungano wa aina hii huku wakiiendeleza mbinu yao ile ya siku zote ya udini!!! Wakristo waislamu tutwangane wao waendelee kuipora nchi!!! (Watch out!!!)

  Viongozi wa uamsho wamekataa wao kuusishwa na kuchomwa kwa kanisa sababu si agenda yao hiyo! Majasusi wa watawala mafisadi wamelifanya hilo ili tu asasi hii ionekane ni mbaya na hatari na ipigwe marufuku kwa sababu tu wao wana matakwa yao ya kuendela kuitesa nchi hii!

  Yatubidi sasa kama wenye nchi! wajitokeze watu wenye busara watakaotuongoza ili kuepuka hali ya hatari kama hii!

  So Sad! Luv u Tanganyika & Zanzibar


   
Loading...