MsemajiUkweli
JF-Expert Member
- Jul 5, 2012
- 13,171
- 23,975
Nimekuwa nikijiuliza maswali mengi kuhusu msafara wa Rais Magufuli.
Kwa watu ambao wana fikra pana na wamebahatika kuwa katika msafara wa Rais Magufuli lazima pia watakuwa wanajiuliza maswali mengi.
Ukiachilia mbali uwingi wa wananchi wanaojitokeza barabarani mpaka wengine wanaamua kwa nguvu kusimama kati kati ya barabara na kufunga barabara ili gari la Rais lisimame lakini ndani yake kuna hoja za msingi ambazo kama taifa tunapaswa kujiuliza.
Wananchi wa Mkoani Tanga baada ya kuiona gari ya Rais Magufuli waliamua kusimama mbele ili kuhakikisha haendelei na safari yake.
NOTA BENE:
Kutokana na kukosa watu wengi wenye fikra pana Sitashangaa kuona wachangiaji wengi watajikita kwenye dhana kuwa wananchi hawawezi au wanaweza kusimamisha msafara wa Rais badala ya kuangalia hoja zangu nje ya dhana hizo kama ninavyojaribu kubainisha katika mada.
Madhumuni yao makuu ni kutaka Rais Magufuli atatue matatizo yao achilia mbali kuongea nao. Ukisikiliza matatizo yao unagundua mengi yamesababishwa na utendaji wa Serikali za Mitaa na sio Serikali Kuu.
Ieleweke kuwa Serikali za Mitaa ni vyombo vya wananchi ambavyo kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania huundwa, huendeshwa na huwajibika kwa wananchi.
Dhumuni la kuwapo kwa Serikali za Mitaa ni kupeleka madaraka kwa wananchi. Hii ni kwa kuwa wananchi ndio chimbuko la mamlaka yote katika nchi yeu.
Katiba inaelekeza pia kwamba vyombo vya Serikali za Mitaa vitakuwa na haki na mamlaka ya kushiriki na kuwashirikisha wananchi katika kupanga na kutekeleza shughuli za maendeleo na utoaji wa huduma sehemu zao na chini kote kwa jumla.
Ikumbukwe kuwa, baada ya Wajerumani kuja na kukuta utawala wa serikali za wenyeji uliamua kuweka mawakala wake.
Mwingereza alipokuja, yeye akaamua kuhalalisha utawala wa wenyeji kwa Sheria Na.72 ya mwaka 1926.
Baada ya kupata uhuru, Mwl. Nyerere alifuta tena Serikali za Mitaa mwaka 1972 na kuanzisha mfumo wa Madaraka Mikoani.
Mwaka 1982, Mwl. Nyerere aliamua kurudisha tena serikali za mitaa lakini pamoja na kuendelea kuboreshwa tunashuhudia matatizo mengi yakijitokeza hasa kwa wananchi wanyonge wa vipato.
Kila mwaka taarifa ya Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) inaonyesha matumizi mabaya ya fedha, watumishi na mali za halmashauri kwenye serikali za mitaa. Wananchi wanaporwa ardhi za vijiji, huduma duni za kijamii na umangimeza.
Nini kifanyike ZAIDI ili tuboreshe Utawala wa Serikali za Mitaa hasa ikichukuliwa kuwa kuanzia mwaka 1990 kumeanza kufanyika uboreshaji wa Serikali za Mitaa lakini matatizo yanazidi kuongezeka?
Je, ni wakati tena wa kufuta utawala wa serikali za mitaa?
Kama taifa, tunakosea wapi hasa ikichukuliwa tuna viongozi mbali mbali waliopewa majukumu ya kutatua matatizo ya wananchi kutoka kijijini mpaka Taifa?. Tuna viongozi wa Vitongoji, Mitaa, Vijiji, Kata, tarafa, Madiwani, Wabunge, Wakuu wa Wilaya, Wakuu wa Mikoa, Mawaziri, Waziri Mkuu, Makamu wa Rais na Rais wa Tanzania.
Ni vyema ieleweke kuwa Serikali za Mitaa si wakala wa Serikali Kuu bali ni serikali kamili zenye mamlaka chini ya Sheria ndiyo maana zimepewa ‘’bunge’’ lake la kutunga sheria ambalo linaitwa Baraza la Madiwani.

VIDEO: