Kinachotoea Igunga na madhara yake kwa taifa letu

Seacliff

Senior Member
Dec 1, 2010
158
152
Siku za karibuni kutatokea mabaya sana hapa Tz kwa sababu ya uzembe wa hii administration kuthibiti mambo yanayotokea sasa.

Kuna tabia ya hii awamu ya uongozi kuongoza kama vile kwa sababu wanajua hii ni term yao ya mwisho kwa hiyo hata wakiwachafulia watakaokuja, haina madhara kwao (scorched earth policy). Kwa bahati mbaya sana, viongozi wengi wa serikali ambao hawatakiwi wawe na upendeleo kwa chama chochote, wanashindwa kuona hilo na hivyo na wao wanajiunga kwenye uchafuzi. Polisi au viongozi wengine wa dola wanashindwa kujua kuwa, watakuwepo na chama chochote kitakachochukua madaraka kitawategemea wao kuongoza kwa haki na kulinda amani ya nchi.

Kwa sasa hivi raia wameshapata ile hisia kwamba majeshi yetu ni mali ya chama tawala badala ya ukweli kwamba majeshi yetu ni mali ya raia na wako pale kulinda haki zao. Ni kwanini viongozi wetu wanakubali wananchi wenzao wanyanyasike alimradi wao wanaishi vizuri? Kama kiongozi wa juu (wa chama chochote) ambaye ni raia na sio askari anaruhusiwa kupanda jukwaani kwenye mkutano wa hadhara akiwa amevaa silaha waziwazi, hii inatuma message gani kwa vijana wetu?

Kama polisi na viongozi wa serikali wameshindwa kumsihi aifiche hiyo silaha angalau kwenye shati (akiwa pale pale jukwaani) hiyo inaashiria nini kuhusu uwezo wa majeshi yetu kulinda usalama wa raia? Granted, kufuatana na sheria zetu za leo (refer: The Arms and Ammunition Act, Chapter 223, No.19 of 2007; Part II-Section 5) Mheshimiwa wetu huyu inawezekana hajavunja sheria lakini siku zote kwenye ustaarabu wowote duniani, viongozi wanategemewa wawe mfano kwa jamii. Kwa wale vijana ambao hawana uwezo wa kununua bunduki na wamekaa chini pale wanamwona kiongozi wao anatembea kibabe na bastola kiunoni, ni statement gani wameisikia toka kwa Mheshimiwa Rage? Ni kama wametangaziwa watayarishe rungu zao!! Si ajabu fujo yote inayotokea kule Igunga sasa hivi isingekuwa mbaya kama ilivyo kama serikali ingesema neno angalau moja tu kuhusu kutokufurahia kitendo hicho cha kupanda jukwaani na silaha ya moto.

Na hii haina maana kuwa ni vijana wa CCM peke yake wanaiga hili jambo. Wote Tanzania wanaambiwa "tumia na onyesha nguvu yako". Imagine kama hali itabaki hivi hadi uchaguzi mkuu. Kama by-election ya jimbo moja imeleta zogo kubwa namna hii, imagine majimbo yote Tz yakiwa kwenye uchaguzi (in 2015). Imagine kwenye miji mikubwa ambapo wenye uwezo wa kununua na kumiliki silaha (legally and illegally) ni mara mia ya hapo Igunga.

Nilishasema huko siku za nyuma kwamba mwanzo wa vita vya wenyewe kwa wenyewe kule Rwanda ulikuwa wakati watu walivyoanza kuonekana wanatengeneza na kukusanya mapanga na uongozi ukakaa kimya kwa sababu waliokuwa wanafanya hivyo walikuwa watu "wanaofanana" na uongozi wenyewe na wakawakalia kimya. Kama viongozi wangekataza hilo, vita hii ingeepukika au at least isingefikia pale ilipofikia.

Viongozi wetu watekelezaji serikalini walioteuliwa na Raisi (mfano PS kwenye ministries, DPP, RCs, DCs, etc) wana uwezo wa kutosha kielimu lakini kimawazo wamebaki kwenye mfumo wa chama kimoja. Wanashindwa kuelewa kuwa wanasiasa watabadilika kila miaka mitano lakini wao wanatakiwa wajenge sera zenye kujali haki na mipango ya kudumu kwenye maeneo yao ya kazi kwa sababu wajibu wao, ingawa unaweza ukabadilishwa kama chama tawala kikibadilika, lakini mabadiliko mengi yatategemeana na long term programmes walizoweka kwenye maeneo yao. Hatuwezi kumlaumu mwanasiasa wa chama chochote akipigia debe chama chake na kusema ndio bora, hiyo ni kazi yake. Lakini viongozi kama askari na jeshi, wana kazi ya kutulinda sisi na kuturekebisha tunapovunja sheria, hatutakiwi kuwaogopa eti kwa sababu tumechagua kukubaliana na chama fulani.

Kila siku natamani kama viongozi wetu wa vyama na serikali wangeweza kuwa na ujasiri wa kuongoza kwa haki wakijua kwamba wote tuna haki ya kuishi kwenye hii nchi na tunataka tujenge kwa ajili ya watoto wetu kama vile waliotutangulia walivyojitahidi kwa uwezo wao kujenga kile tulichokikuta.
 
Back
Top Bottom