Kinachosababisha jua kuonekana kuwahi kuchomoza au kuchelewa kuzama

Victor Mlaki

JF-Expert Member
May 1, 2016
3,542
3,451
Jana tarehe 16/4/2020 Mkoa wa Dar es Salaam ulishuhudia jua kuchelewa kuzama jambo ambalo liliwashangaza wengi na hivyo niliamua kufukua maarifa ya fizikia na Jiografia juu ya hali hiyo.

Kuna masuala mengi ya kifizikia na kijiografia yanayotokea Duniani ila kutokana na shughuli zetu za kila siku kuna wakati hatuangalii kabisa au hata tukiona hatuhusishi na maarifa uliyowahi kuyapata darasani au nje ya Darasa jambo linalotoa nafasi kwa baadhi ya watu kuuhusisha matukio hayo na hali za kutishia au kupandikiza imani tofauti.

Je unatambua jua huonekana limechomoza dakika mbili kabla ya jua lenyewe kuchomoza?Hali hii ipo na ni radidi lakini kubaini hilo linahitaji kuweka utayari wa kudadisi.Ni kweli jua huchomoza hunekana kuchomoza mapema zaidi ya muda wake wa kuchomoza halikadhalika jua kuonekana limezama mapema zaidi ya muda wake wa kuzama

Hali ya jua kuonekana muda ambao tunafahamu inatakiwa liwe limezama inaitwa "Dusk/ apparent sun set".Hali hii hutokana kwa kiasi kikubwa na kuakisiwa (refraction of light) kwa mwanga unapopita kutoka kwenye "medium" moja kwenda nyingine.

Mwale wa mwanga hupinda kadiri unavyopenya kwenye medium moja kwenda nyingine na hali hiyo ya kulinda kwa mwale wa mwanga hutufanya kuliona jua katika sehemu isiyo halisi "relative position".

Miale au mwale wa mwanga wa jua linapokuwa limezama unaweza kupinda na kuonekana tena katika eneo ambalo jua hutazamiwa kuwa limezama na kufanya mwanga wa jua usio katika sehemu halisi "perceived position" wakati jua lenyewe linakuwa kwenye sehemu halisi "true position" mathalani limezama.

Tuendelee kujifunza zaidi.
 
Dar Jana jua lilichelewa kuzama?
au jua lilitokeza katikat ya mawingu na kufanya Yellow/Gold clouds?

kama ni muda wa kuzama ule ulikuwa ni muda wake wa kila Siku.
Refraction of light kwenye mawingu inaweza kukuonesha sehemu isiyo halisi ya jua kutegemea na na mahali ulipo.
Unataka kusema jua lilichomoza katikati ya mawingu kama mchana na huku unaafiki lilikuwa limezama!!..
Tuendelee kujifunza zaidi.
 
.
Dar Jana jua lilichelewa kuzama?
au jua lilitokeza katikat ya mawingu na kufanya Yellow/Gold clouds?

kama ni muda wa kuzama ule ulikuwa ni muda wake wa kila Siku.
tapatalk_1587109990657.jpeg


Jr
 
Light ray's can be scattered, reflected or absorbed in the clouds. What we see is the relative position and not the actual position of the sun.
 
Kumbukeni ilianza hivi kabla ya huo mwanga kuonekana
 

Attachments

  • IMG-20200417-WA0007.jpg
    IMG-20200417-WA0007.jpg
    23.8 KB · Views: 5
Nilikuwa nasubiri majibu ya TMA na ninashukuru wameshatoa tayari naomba wale walikuwa wanakataa nilichoandika jana waje na majibu ya TMA tuone uhusiano na tofauti upo wapi.
 
Back
Top Bottom