N'yadikwa
JF-Expert Member
- Aug 10, 2014
- 6,825
- 9,528
Moja ya sababu kubwa inayochangia foleni majira ya asubuhi na jioni kwenye barabara nyingi za Dar es salaam ni ufinyu wa VITUO VYA DALADALA.
Kusema kweli VITUO VYA DALADALA jijini Dar es salaam ni vifinyu sana kiasi kwamba havitoshelezi DALADALA angalau 5 kuegesha kwa pamoja ili kushusha abiria.
Mbali na ufinyu huo pia, ipo tabia ya baadhi ya madereva wa daladala kupenda kupakilia abiria nje ya vituo hasa MWANZO na MWISHO wa kituo sehemu ambayo ni nje ya kituo suala hili husababisha msongamano mkubwa wa magari mengine kwa kuwa daladala hilo kufunga upande mmoja wa barabara kama ni double lane.
Changamoto nyingine ni Madereva wa DALADALA kupakia abiria maeneo ambayo siyo vituo. Kusema ukweli wenzetu wa Polisi kwenye eneo hili la kuwadhibiti madereva wanaopakia abiria maeneo yasiyo vituo wamelifumbia macho.
Hapa nawaza kwamba kama Traffic Police wakifanya kazi yao vema foleni itapungua pakubwa... Madereva wa daladala wadhibitiwe kufuata sheria na wawazoeze abiria kupanda gari kwenye vituo ili kupunguza foleni.