Masinki
JF-Expert Member
- Dec 18, 2014
- 695
- 460
Neno "Mwelekeo" ndio sababu kuu ya Vyama vya upinzani kutokubalika na kuaminiwa kupatiwa Nchi na watanzania.
Uchaguzi wa mwaka 1995 upinzani chini ya NCCR Mageuzi ilibaki kidogo kuchukua nchi chini ya Augostino Lyatonga Mrema, kabla ya watanzania kushtuka dakika za mwishoni baada ya Baba wa Taifa Mwl. Julius K Nyerere kutoa speech kali iliyoonesha Mwelekeo wa CCM na utofauti upinzani ambao walikuwa hawana, KAZI ikaishia kwenye Sanduku la kura ambalo lilimpa ushindi hayati Benjamin W Mkapa wa Chama cha Mapinduzi.
Mwaka 2000 Chama cha wananchi CUF chini ya Profesa Ibrahim Haruna Lipumba kiliibuka kuwa na agenda kali na kukubalika Kwa kiasi na baadhi ya wananchi lakini shida ikabaki palepale Mwelekeo wao kisiasa ni upi? Hadi kutosha kupewa Nchi? Jibu hili lilichakatwa na watalaam ikaonekana bado sio Chama sahihi cha kuchukua Nchi Kwa sababu Nchi sio Miguu kila mtu awe nayo ni zaidi ya hiyo.
Mwaka 2005 Chama cha wananchi tena kilikuwa bado kina nguvu kidogo na hapo hapo CHADEMA wakawa wanaibukia chini ya Freeman Aikael Mbowe aliyekuwa mgombea wao wa Urais na mshindi wa Tatu katika kinyang'anyiro hicho walipimana ubavu na Chama pendwa cha CCM chini ya Jakaya Mrisho Kikwete aliyekuwa anapendeka Sana na wananchi Kwa kipindi hicho kama ilivyo ada CCM ilishinda dhidi ya upinzani tatizo likawa lile lile Mwelekeo wao ni upi?
Mwaka 2010 CHADEMA wakawa na slogan yao ya People's Power na agenda nzuri tu za kukemea Rushwa,ubadhirifu wa Mali za umma na mengine mengi yaliyogusa nyoyo za watanzania chini ya Mtu mwenye Mwelekeo kidogo ya kiuongozi na shupavu wa siasa hapa Nchini Dkt. Wilbroad Peter Slaa ilibaki hivii kupewa Nchi lakini je? Dkt. Wilbroad Peter amezungukwa na watu wa aina gani? Ndio lilikuwa swali muhimu Kwa watanzania!!! Ikajulikana Dkt. Slaa ni mwadilifu lakini kazungukwa na mafisi!! Kazungukwa na Chama ambacho wengi wao wanatiliwa mashaka lakini pia hawana Nia na Mwelekeo mzuri na Taifa hili hapo Sanduku la kura likatoa jibu.
Mwaka 2015 ulikuwa ni kituko zaidi Kwa CHADEMA walimleta mtu Yule waliyekuwa wanawaimanisha ni fisadi mkubwa Nchini na aliyekataliwa na CCM pamoja system zote za Nchi kutokana na history background yake ya kisiasa sio mwingine ni Edward Ngoyai Lowassa!!! Kwa wananchi alionekana Lulu na mkombozi wa matatizo yao lakini wananchi hao hao wakawa na maswali Lowassa ni Nani?? Wakamshangilia dakika za lala salama za kampeni wengi wao wakagutuka wakarudi kuangalia documents na wasifu wa kila mgombea hatimaye mioyo yao ikasema hapana nyumbani ni CCM chini ya Jiwe Dr John Magufuli,, Lowassa akazikwa rasmi kwenye Sanduku la kura sababu ni zile zile Mwelekeo wao ni upi?
Mwaka 2020 CHADEMA Kwa mara nyingine wamejitutumua wakamleta mtu waliyedhani ni mwiba mkali,mtu aliyeponea mauti Kwa risasi Zinazosemekana 16,mwanaharakati na mtu mbishi kuwahi kutokea ambaye kinywa chake kimejaa matusi Kwa viongozi aliokuwa anaenda kuwastaafisha majukumu ya Nchi,vyombo vya ulinzi na usalama ambao kama angeshinda wangeenda kumlinda Kwa mioyo yao yote sio mwingine ni Mwanasheria Tundu Antiphas Lissu,kilichotokea kila mtu anajua watanzania walimfuata katika mikutano yake lengo likiwa ni moja Tu kuona ukuu wa Mungu basi the rest is history, Sanduku la kura lilitoa majibu sababu ni zile zile Mwelekeo wao ni upi??? Nani anapenda kuuzwa mchana kweupe??. TL awe Rais???thubutu!!!! Huwezi kuchagua Giza wakati Nuru bado IPO!!! Wapinzani bado Sana mjipange na mkubali kushirikiana na serikali ili iwape semina ya namna ya kuongoza Nchi!!!
Masinki,mtanzania