GENTAMYCINE
JF-Expert Member
- Jul 13, 2013
- 63,350
- 127,291
Aliyekuwa Mtangazaji wa Wasafi Media Diva kaamua Kufunguka makubwa
Mimi siyo wakwanza kuacha kazi Wasafi Kisa Mishahara ni wengi pia wanao lalamika lakini ndo hivyo hawana pakwenda.Huyo Aaliya wiki iliyo pita Kaomba kazi Crown Fm Kwa Alikiba na hiyo yote ni kutokana na njaa, ni video nyingi za watangazaji wa hapo Wana omba pesa za nauli kurudia nyumbani Kwa sababu Mishahara haitoki.
Kuna wengine hapo Wanadai Mishahara ya miezi Saba.George Ambangile na Ahmed Abdallah wameacha kazi kisa Mishahara, wameona Wana pata majina makubwa lakini mfukoni hamna kitu wakaona ni Bora waishi bila kazi kuliko Kila siku unaaga unaenda kazini halafu hakuna unacho kiingiza.
Chanzo Taarifa: Miss Platnumz
Vijana mnaoingia katika Fani hii Sisi Wabobezi na Kaka zenu tukiwa tunawaonya juu ya Media Houses za Tanzania muwe mnatuelewa tafadhali. Tatizo lenu huwa mnapenda Umaarufu wa haraka kwa Watu kwa Kudanganywa na Mikataba Minono Hewa na hawa Wamiliki wa Media.
Halafu kama kuna Kosa kubwa la Kiufundi mmelifanya ni kukimbilia kuacha Kazi wakati bado hamjapata Kazi mpya. Watu wenye Akili huwa hawafanyi hivi bali mlitakiwa muendelee Kuvumilia Msoto wa Wasafi Media huku taratibu mkitafuta Kwingineko. Nawahurumia hamna Kazi sasa huku mkiwa na Wake zenu Warembo hasa.