Kinachonishangaza ni kwamba amekuwa king'ang'anizi na kunizoea sana

perfect_rahym

Member
Mar 27, 2017
41
45
Waungwana hakika haijafika hata siku mbili Pale nilipo muelezea hisia zangu kuwa nafsi, moyo na macho zimemuona yeye na nimetokea kumpenda sana cha ajabu hakuwa mgumu wala japo kidogo mwenye kusita sita au laaah japo kunipa calendar kuwa nivute subira atanipa jibu siku zijazo mbeleni mana huwa siku zote mambo mazuri hayataki haraka ila alinikubalia na mate pia kunigaia

Kinachonishangaza kwenye mahusiano yetu mimi na yeye haijafika hata wiki moja ametokea kunizoea hataki hata siku ipite bila hata kumpa salamu amekuwa ni msichana king'ang'anizi kutwa nzima ni kupiga simu hanipi hata nafasi ya kufanya kazi yani kama yeye ndio ameni approach wakati ni mimi

Ninacho jiuliza je? Ana mapenzi ya dhati na mimi au ana mipango yake ambayo mimi sifahamu Ila kumpenda nampenda kweli
 
Mkuu huwezi jua labda alikupenda kwa muda mrefu ila tu alishindwa namna ya kukuanza ,
Ndomana ulipofunguka naye umempa uhuru wa kujiachia

Tusipende kuwa na mawazo mabaya kila wakati fikiria nae ni mwanadamu alafu kila mtu ana uwezo wake wa control hisia ,wengine hawawezagi kujizuia kabisaaa
 
Sasa ulitakaje. Akiweka pozi shida akifungulia moyo shida. Badala ushukuru unakuja kuanzisha mada huku jf ili watu wamsimange.
 
Yani watu kama hao nawapenda sana. Sio wale wanaojifanya hard to get
Mpe ratiba tu atakuelewa
 
Mkuu huwezi jua labda alikupenda kwa muda mrefu ila tu alishindwa namna ya kukuanza ,
Ndomana ulipofunguka naye umempa uhuru wa kujiachia

Tusipende kuwa na mawazo mabaya kila wakati fikiria nae ni mwanadamu alafu kila mtu ana uwezo wake wa control hisia ,wengine hawawezagi kujizuia kabisaaa
umeongea point sana mkuu
 
Waungwana hakika haijafika hata siku mbili Pale nilipo muelezea hisia zangu kuwa nafsi, moyo na macho zimemuona yeye na nimetokea kumpenda sana cha ajabu hakuwa mgumu wala japo kidogo mwenye kusita sita au laaah japo kunipa calendar kuwa nivute subira atanipa jibu siku zijazo mbeleni mana huwa siku zote mambo mazuri hayataki haraka ila alinikubalia na mate pia kunigaia

Kinachonishangaza kwenye mahusiano yetu mimi na yeye haijafika hata wiki moja ametokea kunizoea hataki hata siku ipite bila hata kumpa salamu amekuwa ni msichana king'ang'anizi kutwa nzima ni kupiga simu hanipi hata nafasi ya kufanya kazi yani kama yeye ndio ameni approach wakati ni mimi

Ninacho jiuliza je? Ana mapenzi ya dhati na mimi au ana mipango yake ambayo mimi sifahamu Ila kumpenda nampenda kweli
Mapenzi yananipa shidaaa shida bwanaa...ni donda lisilokuwa na tiba tiba bwaana
 
wenzio tunawasaka sana wanawake kama hao na hatuwapati we umepata unaanza kupata mchecheto...
 
Back
Top Bottom