Kinachonikera kwenye mjadala wa katiba mpya...

Bishanga

JF-Expert Member
Jun 29, 2008
15,323
10,050
Ni huu mwenendo wa kuangalia maslahi ya watu binafsi na vyama vyao badala ya ku focus kwenye mustakabali wa nchi,utaona mtu anatoa povu kisa rasimu imemgusa pabaya,inahusu? .......mara oh kwenye serikali tatu CUF itakuwa strong Zanzibar na CHADEMA bara, mara sijui kundi la Mzee Sitta litagombea urais wa bara au muungano,mara sijui eti Mzee Slaa agombee muungano,mara lowassa/membe itakuwaje sasa........

This is utter nonsense, individuals tupo leo kesho tutakufa,vyama vipo leo kesho vitakufa ( mifano hai ni KANU,UNIP,DP ya Kibaki na vingine vingi tu),mwisho wa siku kinachobakia ni nchi.

Jamani tujadili mustakabali wa nchi yetu tuone ni Katiba ipi itasimamia utaratibu wa kutuvusha toka kwenye lindi la umaskini. Katiba ni mkataba kati ya watawala na watawaliwa, tuangalie ni kwa jinsi gani watawala Katiba itawabana ili wafanye kile kitakachokuwa cha manufaa kwa watawaliwa na sio kuneemesha mijitumbo yao.

Ndugu zangu tukichezea hii fursa we should as well kiss maendeleo bye bye na siku moja tutaishia kusema bora tungekopi na kupesti ya nchi fulani jirani.

Nawasilisha,
Bishanga Abashaija

Nakala aione Mzee Sinde.........kazi yako bado ni mbichi kabisa from what i am seeing........watu watakupinga sio kwa sababu ya ubaya wa unachokisema ila kwa sababu kisu kimegusa mfupa!
 
Vipengele vingi kwenye rasimu ya katiba vimedokeza sana kuhusu mambo ya Siasa kuliko sekta nyingine yoyote
 
Pamoja na mambo mazuri mengi yanayongelewa na wataalamu mbalimbali kuichambua Rasimu ya Katiba, ninachokiona ni ushabiki zaidi ya hoja na mantiki katika Siasa.

Muujiza mojawapo nitakaoushangaa sana ni pale CHADEMA watakapochukua position ya Kupinga Rasimu na CCM wakaungana nao!!!

Ujinga mmoja mkubwa wa baadhi ya viongoi wa Chama changu cha Mapinduzi ni kuogopa kivuli cha CHADEMA, pale CHADEMA wanapotake a certain stand wao wanaenda opposit ili tu waonekane hawako na CHADEMA hata kama ni kwa Maslahi ya Kitaifa. Na hili limeshuhudiwa bayana katika Bunge la sasa (Ingawa Jambo hili halikuwepo kwa kiasi kikubwa wakati wa Bunge lililopita).

Hebu tusubiri tuone, mimi ningependa kuona hoja zaidi ya ushabiki katika hili la katiba Mpya.
 
Back
Top Bottom